ni biashara halali chache sana zinaweza kulipa kwa kiwango hicho.....na hizi chache utakuta risk pia ni kubwa sana. Kilimo kwa mfano kinaweza kulipa faida kubwa lakini risk ya kupoteza pia ni kubwa mno.
Ku fix sh 20m na kupata riba ya sh 1.6m kwa kila mwezi, ni sasa na kusema riba ya 96% kwa mwaka. Hakuna benki yoyote inayoweza kulipa kwa kiwango hiki. Jiulize tu, wao watawekeza kwenye nini ili wapate ribs/faida ya zaidi ya 96% kwa mwaka?
Anyway, ni mjadala mzuri. Unapoweka fixed deposit ni muhimu pia kuzingatia mfumko wa bei. Usipokuwa makini inaweza kuwa hujapata faida yoyote maana thamani ya ile hela uliyo fix baada ya mwaka itakuwa imepungua. Inflation rate kwa sasa wastani wa 5% (oopps, ngoja nicheki NBS nsije fungwa!). So shilingi 100 ya sasa itakuwa sawa na sh 95 baada ya mwaka mmoja! Au kwa lugha nyingine, utahitaji sh 105 baada ya mwaka mmoja kununua kitu kinachouzwa sh 100 sasa hivi.