Namuombea msamaha mkuu jamaa huwa namuona ni mkali kwenye kila kada atakuwa kateleza tu?
Ngoja apate somo kidogo Benki kuu wanatoa maelekezo kwa benki zote ili kupunguza au kuongeza mzunguko wa pesa
kwa kuconrol
- Riba
- Benki lazima iwe na kiasi ambacho iitakideposit kiasi BOT kama mteja anavyodeposit benki ili kujifinance ikitokea mambo yameenda mrama
- Ni lazima kutoa mikopo kwenye project kubwa hasa za kiviwanda
- Kuwa tayari kuongeza kiasi na amana BOT ikitokea kuna mfumuko wa bei ili kupunguza mzunguko wa pesa
- banks kupunguza kukopesha ikionekana mzunguko wa hela ni mkubwa kuliko uzalishaji.(Hili nalifafanua hapa chini)
Hili limetokea hawamu hii watu walikuwa wanakopa sana lakini wananunulia magari, wanajenga na kufanya mengineyo ikitokea muda wa kulipa unakaribia kuisha mtu anaingia benki nyingine kukopa ili alipe mkopo wa zamani. Kumbuka unapokuwa na collaterral kubwa ndivyo kiasi chako cha ukopaji kinavyokuwa kikubwa.
Kumbuka mwanzo alikopa kiasi fulani kutokana na udhamini kuwa mdogo ila baada ya kuongeza mali uwezo wa kukopa unakuwa mkubwa hivyo deni la mwanzo linalipika kirahisi na maisha yanasonga.
N.B Sijatoa mbinu ya kukopa