Bank tellers ni wezi wa kimya kimya, kuweni makini

Pesa yako kwanini usihesabu
Unahesabu tu .....
Pesa yako lazima ujitoe ufahamu mzee la sivyo utawafaidisha wengine

Ova
ntajaribu siku maana bank wanafanya sisi hatujielewi.

Hela ikichakaaa hawaiweki kwenye counter machine wanahesabia mikono.

halafu wao wanatoa burungutu used kweli kuna siku ntatenga muda kwa ajili yao naamini ntanuniwa hiyo siku
 
Mwanangu Mimi ndio siwezi kwasababu kwa siku natoa mara tatu au mbili na natoa millioni 20 nitaweza kukaaa na kuesabu kweli
shida ndio inapoanzia hapo bank katika hili wanaonea wateja, kweli buku buku mbili sio kitu ila wasitulazimishe sasa
 
Mi kuna siku hapo UDBS Miaka ya Nyuma kidogo nilipeleka mpunga sikuendakuchukua ila nilipeleka kuweka , nilipeleka m3.5 na nilihesabu vyema na kujiridhisha vizuri kwamba hela ilitimia, wakati niko na bank nishamkabidhi zile hela na akaweka kwenye counting mashine , ghafla nilipigiwa simu maana sikuwa nimezima, nilisahu kuzima hii ni kawaida wengi huwa tunaona sio na wakati mwingine tunapuuza tu. Ile najikunja kuchukua simu mfukoni either nistishe call kwa muda, kumbuka hela nishakabidhi benchi la bank teller anahesabu na kimashine chake, nilivyomalizana na simu ile bank teller ananiambia umeandika kuweka M3.5 lakini hela hazijafika, zipo million tatu laki nne na themanini , nilichoka japo nilijua pale pale kuwa nimeingizwa corridoni baada tu y ile simu.

Bank teller baadhi sio waaminifu, tuwe makini .
 
Siyo tu kwenye maburungutu, muda mwingine wanakupiga wakati wa kuhesabu.

Ukiwapa wanazidondosha chini kwa aujanja halafu anakuambia imepelea inabidi uongezee.

Umakini unahitajika.
hiyo ishawahi mkuta mtu wangu wa karibu ana walikua wote wadada muweka hela na mpokeaji (teller) kapewa anasema hela haijakamilika dada kamwambia hizo hela zimehakikiwa na watu zaidi ya wawili.

Teller anabisha akaambiwa angalia huko chini na mtu akaangalia akaikuta akasema eti hakuiona wakati inadondoka anaomba samahani.
 
Huo Mchezo wanao sana na ni tabia zao unaweza ukadhani hapati marupu rupu pale ila washenzi wale wanatupiga hela sana.

Ukimpa hela muangalie mwanzo mwisho ukijifanya unawaamini kitakukuta kitu siku.
 
Huo Mchezo wanao sana na ni tabia zao unaweza ukadhani hapati marupu rupu pale ila washenzi wale wanatupiga hela sana.

Ukimpa hela muangalie mwanzo mwisho ukijifanya unawaamini kitakukuta kitu siku.

Sahihi mkuu
 
Sijajua kama Ina ulazima sana wa kutumia bank kama vp jioni mda wa kufunga office weka kwenye float asubuhi unazama ATM

Wabongo wababaishaji sana!

Kuna kipindi nlikuwa nikienda kuexchange aisee nlikuwa Naona kipengele kuanza kuhakiki baadae nkapata watu wa kufanya nao exchange kwa rate nzuri na uhakika hata wakikosea wanarekebisha haraka
 
Kupigwa Elfu moja au elfu mbili nacho ni kitu cha kulalamika, kufungulia uzi?
Isitoshe, wafanyakazi wote wameruhusiwa kula kwa urefu wa kamba zao.
 
hebu nielekeze tena kama umeniacha hivi
 
Suala sio kuibiwa hayo maburungutu mnayapata wapi nduguzqngu😂😂 Jana nimepoteza buku 5 nimemwaga nguo karibia zote 😀
Anyway hesabuni Hela vizuri
daah😅

Naelewa inavyokua unapotafuta hela uliyokua unaitegemea.

Nimeshawahi poteza Jero kipindi kile Jero za NOTI

Nilitafuta ile hela nilirudi njia niliyopita hadi eneo nililohisi nimeidondosha kweli nikaenda nikaikuta.

Nilijikubali sana ile siku
 
Hapa si suala la kazi ya bank taller, ni suala la tabia ya wizi. Bank hazina shida ni ww umekutana na mwizi kama mwizi mwingine tu sababu tunaotoa pesa bank ni wengi na si mara zote tunaibiwa.

Ni kuongeza umakini tu na una haki ya kumwambia hesabu kwenye mashine nione kuwa zimetimia ndo unipatie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…