Bank tellers ni wezi wa kimya kimya, kuweni makini

Wahuni sana hao jamaa! Wanatunza noti bandia za kubambikia wateja wao
Teller anatakiwa akipokea note bandia toka kwa mteja ai punch pale pale mbele yake, asimrudishie mteja wala asiiweke bila kuitoboa mbele yake mteja kusudi asije akapewa mteja mwengine
 
..hii ni sawa kabisa
 
Bulk cash, ipo kwenye bundles, either zilofungwa na strips au zile za kwenye nylon from BOT. Kama hizo utahesabu vipi?

na cash ya hivo case ya kuwa na less notes unazipata mara ngapi?
 
Kumbe ndio maana tunao withdraw 20k wanachelewa kutuhudumia na hata wakikupa nikama wanakutupia,Asante Kwa kutufungua mijicho mkuu
20K unatoa kwa teller sio kwenye ATM? Why?

jee unajua kama withdraw bank ndani unachajiwa zaidi kuliko kwenye ATM?
 
NARUDIA TENA NA TENA BANK KUNA WIZI UNAENDELEA KUWENI MAKINI.

Nimeenda kuweka hela kidogo tu Leo, Nikatoa kama kawaida vibunda vitatu vya 10k,5k na 2k

Nimehesabu mara mbili mbili, nikafika kwakua nawajua Teller walivyo nikampa hela dirishani Nikawa makini SANA naangalia siangaliii pembeni namkodolea

Kaweka hela kwenye mashine ikahesabuu fungu la kwanza, Ikahesabu Fungu la Pili na La Tatu.

Akaniambia Bado 5,000 imepelea kwenye lile fungu la 5,000 nikamwambia Rudia kuhesabu,Akachukua zote akaweka Juu ya Mashine zikahesabu kweli imemiss 5000.

Nikamwambia NAOMBA HIZO HELA...

akazichukua hela kafungua Dirisha kanipa Nikazihesabu kwa mkono pale pale Dirishani, Hela zote Zimetimia.

Nikaziweka kama tunavyofunga hela mtaani 5000 moja unaikunja na 5000 mwenzake inakua 10,000

Nikazichukua nikamwambia Chukua HELA hizi hapa Zimekamilika.

Nikagundua WIZI mwingine either ni makusudi au bila kujua Zile mashine kuna Muda zinashika NOTI Mbili zina count kama noti 1.

Usikubali kuhesabiwa HELA kwa mashine akakuonyesha, Chukua Hela zako Hesabu kwa Mkono.

Kama una uhakika 100% hela zako ulizihakiki na yeye anakwambia mashine imehesabu zime miss, Chukua HELA hesabu hapo hapo dirishani kwa Mkono.

BANK wizi hauishi kuna njia nyingi sana wateja tunaumizwa.
 
Na teller nae analazimika kutumia machine maana ndio anaamini ipo accurate na inamsaidia ku detect note fake, hapo chacha!!!
 
Wale ni majambazi, waliwahi iba 20,000 kwenye hela nilizopewa nipeleke CRDB Vijana, Teller 03 alikuwa kijana na shati jeupe akaiiba, mwaka 2011

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Ushuhuda!

Kwenye bulungutu la elfu mbili mbili nishapigwa kabisa tena na benki kubwa tu!

Siku niliyoshangaa zaidi ni kukuta noti kipande ya elfu 10 katika bulungutu la 1M. Tena ilikuwa benki maarufu kabisa nchini!
Kwa matukio hayo mawili siku hizi nakomaa kuhesabu kabla sijaondoka hata ziwe bukubuku 😏😏
 
Ukipewa noti chakavu kuwa makini sana.
Na za bandia zinamixiwa humo humo au zilizoharibika kabisa kwa matumizi ya jamii.
 
No matter what!! Pesa yoyote ninayopewa popote, hata iwe imetoka kwa ATM machine lazima niihesabu. Unless kama imehesabiwa nikiona.
 
C ununue machine

Sent from my FRD-L19 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…