Bar zilizofungiwa zatakiwa kulipa Faini Milioni Tano 5M kila moja ili ziruhisiwe kufanya biashara

Lazima kuna watu wamepata mwanya wa kupiga pesa, si bure........waziri aingilie kati kuona ni namna gani hiyo sheria inatumika, vinginevyo kuna kuonea watu kujenga mazingira ya rushwa.
Watu hawatatoka patupu hapa
 
Kwa sisi waathirika wa kelele tunaona adhabu ni ndogo sana.....yaani ilifika kipindi mtu kulala unavizia...

Yaani mtu inakuwaje unaona kawaida kustarehe kwako kuwe kero Kwa wenzako......??

Hizi adhabu zimechelewa sana......
Watu tunapaswa kuheshimiana....haifai jamii ya watu kuishi kama wanyama wa porini.........
 
 
Nchi inataka kuwa kama kongo

Ova
 
Yani kisa mtu unamadaraka unanyanyasa watu na biashara yao wakati unamkuta yeye kiosk hajawahi fungua, huu ni uhuni, ndo maana majitu ya namna hii ,Rais aliyaita mastupidi, nami nasema stupid,

Watu wanapambana tengeneza ajira kama sector binfsi alafu mtu mmoja kisa ni mkurugenzi wa NEMC ,analeta ustupidi hapa , ndo maana maajari yanawatafuna
 
Haya ni maoni ya wananchi sio NEMC. NEMC ku-impose adhabu kali ni kuonyesha userious wa jambo lenyewe. Unajua wewe huishi chako ni chako au mitaa ya Rain bow ungejua inamaanisha nini.
 
Mimi nadhani walitakiwa wawalime barua ya onyo kisha wakae na kamati elekezi kwa gharama za mwenye Pub wazungumzie namna watasolve hilo tatizo Pub iendelee kuwapo na raia wasipate shida. Sio kufunga kiwanja cha bata ambacho raia wanaenjoy maisha.
 
Isiishie Dodoma tu,unaweza kukuta ni visa wamegongana kwenye mambo flani tena ya kijinga tu,sasa wanakomeshana maana ma Bar yanayopiga mziki wa juu usiku ni mengi sana...
 
Haya ni maoni ya wananchi sio NEMC. NEMC ku-impose adhabu kali ni kuonyesha userious wa jambo lenyewe. Unajua wewe huishi chako ni chako au mitaa ya Rain bow ungejua inamaanisha nini.
Tunataka sasa makanisa yafungwe maana wananchi tumelalamika sana juu ya kelele,
Lakini lini NEMC wamewaita wahusika na kutoa onyo , mbadala wake unakimbilia kufunga biashara na kutaka fain,

Kwamba kwa kua wananchi wamelalamika basi kisa unarungu nikufika nakufunga ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…