Bara la Afrika kuja na Sarafu yake itakayoitwa Afro au Afric (Afro currency au Afric currency)

Mfano mdogo.
1. Sisi hapa East Africa tunafanya biashara baina yetu zenye masilahi ya kuinua uchumi?
2. Tanzania tunaweza kufanya uwekezaji kwenye nchi za Afrika na uwekezaji gani?
Sasa utafanya uwekezaji gani kwenye nchi za Afrika mashariki kama hauna Dollar? Wakenya wenyewe wanatushinda uchumi kwa sababu wanaingiza Dollar nyingi kutushinda... Na usichanganye mambo kwamba eti kisa Uganda na Kenya na Tanzania tunatumia Shillings basi ndio tunatumia sarafu mmoja.... Ugandan shillings, Kenyan shillings na Tanzanian Shillings ni sarafu tatu tofauti kabisa japo zinafanana neno shillings.

Utawekeza nchi gani Afrika bila kuwa na Dollars? Nani atakayeyakubali mashilingi yako yasiyoweza kuuzwa popote duniani... Dollar inauzika popote duniani ndio maana lazima uwe na Dollar... Sasa tukiwa na sarafu ya Afrika lazima itakuwa juu kwa sababu nchi yoyote ya nje ya Afrika ikitaka kufanya biashara na nchi yoyote ya Afrika basi ni lazima inunue kwanza sarafu ya Afrika ili iwe rahisi kufanya manunuzi barani Afrika
 
Mnajidanganya bure.
Hivi nyie mnaijua Afrika na asili yake au mmevimbiwa?
Afrika ni mtumwa wa kila mtu mweupe.
Issue ni kumkataa huyo mtumwa then tuanze upya.
Mkoloni gani atakubali tuwe na sarafu yetu?.
Kwa akili hizi za Kiafrika za Royal Tour?
Sasa kwani mkoroni ndio Muafrika... Mkoroni mwenyewe hakutaka tuwe na uhuru lakini tuliupata... Hakuna kinachoshindikana tukishikamana tukawa na kauli moja
 
Suala siyo dollar. Suala ni
1. Uzalishaji mdogo wa nchi. Mahindi hapa walikuwa wananunua wakenya lkn serikali ilipiga marufuku
2. Sisi afrika hatuna mifumo mizuri ya upokeaji na utumaji hela.
Kuna kazi nyingi za online ambazo unawezafanya na mtu akakulipa, ila changamoto kwenye suala la malipo. Unaishia kuona hela hiyo. Zimeshanipita hela nyingi sana mpk inauma.
Mimi naona siyo dollar.
 
Kwani hii ndiyo mara ya kwanza kuongelewa? Kwenye ukanda tu hakuna hivi kungekuwa na matumaini East Africa tungekuwa tayari, sahizi watu wanapinduana .

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
Hakuna umoja ukanda huu kwa sababu ya watu wanaamini kwenye kushindwa... Wakenya mbona wako tayari, ila Wabongo ndio hawataki... Pia mfano ni humu tu kwenye huu mjadala si umeona Wabongo walivyokuja wanasema haiwezekani mara hatuwezi... Alafu bado unataka jibu kwa nini Afrika mashariki hatuna sarafu, kuwa na sarafu haitaji mjadala ni kuamua tu, ila bado kuna vikwazo vya watu wasiojua umuhimu wa sarafu kazi yao ni kupinga bila kuwa na sababu za msingi .. mtu anakuja anasema tu haiwezekani, ukimuuliza kwa nini anakosa jibu, anaanza kuleta mambo ya siasa, sijui ufisadi... Sasa ufisadi si ni jambo la mtu binafsi, na ufisadi umeanza tangu binadamu wa kale
 
Kwanini Kenya wana dollar nyingi kuliko sisi?
Tatizo siyo Dollar tatizo
1. Umasikini
2. Teknolojia ndogo
3. Uzalishaji mdogo
4. Mifumo mibovu ya upokeaji na utumaji hela.
China anatumia dollar?
 
Tanzania yenyewe imeshindwa kuendesha bandari zake, kusimamia huduma ya mawasiliano (TTCL) na kutoa huduma ya ndege. Itaweza kuwekeza Kenya?
Ni jibu hili swali kwanza.
Una huduma yoyote unayotoa mtandaoni kwa mataifa mbalimbali?
 
Umezungumzia Kenya na Tanzania... Wakenya ni lazima watumie sarafu zetu wakiwa wanunua vitunguu kwa sababu pia ni rahisi kuzirudisha kwa sababu ya muingiliano wa biashara kwetu... Hivyo hizo shillings zetu kuna namna zinarudishwa Bongo kwenye mzunguko wa biashara... Lakini mtu kutoka Ghana achukue shilingi yako aende nayo gani anairudishaje Bongo, kule itaenda kumuozea tu atapata athara, kwa sababu hakuna mtu mwingine atakayenunua kwa hiyo shilingi yako, mnaijeria hawezi kuuziwa kitu na mtu kutoka Ghana kwa hiyo shillingi yako... Hivyo kwa mtu kutoka Ghana lazima akulazimishe mtumie Dollar ili naye akirudi na Dollar Nchini kwao basi akitaka kuziuza kwa mwingine iwe rahisi... Lakini tukiwa na Sarafu moja ya bara la Afrika hakuna sehemu ya Afrika utakayoshindwa kwenda kufanya nayo biashara kwa sababu pesa ni hile hile.

Mwisho umemaliza na Siasa sijui uongozi... Hayo ni mambo ya Nchi binafsi... Hata Marekani kwenyewe kwenye Dollar kuna hayo matatizo ya rushwa na mauaji kila kukicha... Hayo matatizo uliyoaandika mwishoni yanahusu nchi usika, ufisadi wa Sudani sio ufisadi wa Tanzania, ufisadi wa Nigeria sio ufisadi wa Kenya... Hapo kila nchi inajitegemea... Mbona ulaya kuna rushwa na bado Euro inafanya vizuri
 
Ushawahi kufanya online business?
 
Sasa kwani mkoroni ndio Muafrika... Mkoroni mwenyewe hakutaka tuwe na uhuru lakini tuliupata... Hakuna kinachoshindikana tukishikamana tukawa na kauli moja
Nadhani huijui historia vizuri.
Baada ya uchumi wa Ulaya kuyumba due to the effects of WW1 na WW2 Uingereza kipindi hicho kiranja mkuu akaamua kuanza kuachia makoloni yake na kuwashawishi wengine waachie.
Ndio maana Nyerere alipewa UHURU ingawa malofa anawadanganya kuwa kaupigania.
Makoloni waliona yanawapa hasara.
Baadhi ya wakoloni kama Ureno uwekezaji wao Afrika ulikuwa mkubwa kama kwao sasa wakaona kazi kuachia koloni lakini kwakuwa kiranja alishaamua ndio maana walishindwa.
 
Tanzania yenyewe imeshindwa kuendesha bandari zake, kusimamia huduma ya mawasiliano (TTCL) na kutoa huduma ya ndege. Itaweza kuwekeza Kenya?
Ni jibu hili swali kwanza.
Una huduma yoyote unayotoa mtandaoni kwa mataifa mbalimbali?
Sasa hayo maswala ya bandari sijui TTCL sijui ndege hayo ni matatizo ya nchi husika... Na mengi hapo yanashindwa kujiendesha kutokana na ukata wa Dollar... Sasa si nimekwambia ili uwekeze kwenye nchi nyingine ya Afrika si unatakiwa uwe na Dollar, sasa kama hauna Dollar za kutosha utawekezaje... Lakini ukiwa na sarafu ya Afrika unawekeza vizuri tu kwa sababu hiyo nchi nao watakuwa wanatumia sarafu sawa na yako
 
Labda watawala wawe wameshushwa toka mbinguni lakini kwa watawala tulionao it’s impossible ni sawa na kuota mchana huku unatembea.
 
Haya vipi kwenye kuwa na sarafu yetu, Tunaweza au hatuwezi?
 
Unafanya biashara au unatoa huduma gani mtandaoni?
 
Labda watawala wawe wameshushwa toka mbinguni lakini kwa watawala tulionao it’s impossible ni sawa na kuota mchana huku unatembea.
Hayo ni mawazo yako na yataheshimiwa... Lakini swala la kuwa na Sarafu moja ni la kila Muafrika na si watawala, tukiwa na sauti moja litawezekana ila kila mtu akiwa anala kwake mara huyu anasema haiwezekani hapo lazima tushindwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…