KERO Barabara eneo la Kongowe Mwisho - Vikindu haipitiki kwa siku 3 baada ya lori kuziba njia kutokana na ubovu wa barabara

KERO Barabara eneo la Kongowe Mwisho - Vikindu haipitiki kwa siku 3 baada ya lori kuziba njia kutokana na ubovu wa barabara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa Mlamleni kata Tambani Wilaya Mkuranga.

Tuna shida ya barabara hadi sasa ni siku ya tatu barabara haipitiki kutokana na ubovu wa barabara, gari kubwa la mzigo semitrela limeziba njia, hakuna gari wala bajaj inayoweza kupita, hata pikipiki zinapita kwa tabu sana kutokana na eneo lenyewe kuwa na udongo wa mfinyanzi na hakuna barabara mbadala kuelelekea Mlamleni.

Eneo ambalo lina changamoto hiyo ni kutoka Kongowe mwisho kuelekea vikindu umbali kama wa mita 800, kabla hujafika njia ya kukunja kuelekea Toangoma kuna njia inayoingia kulia ambayo haina lami.

Tunaomba msaada katika kupaza sauti kero hii imekuwa ni ya muda mrefu sana.
 
Tuna shida ya barabara hadi sasa ni siku ya tatu barabara haipitiki kutokana na ubovu wa barabara, gari kubwa la mzigo semitrela limeziba

Wapi huko ? Tupia Picha.

Upo umuhimu wa kuwepo sheria gari likiharibika njiani mmiliki abanwe kisheria kuliondoa ndani ya masaa 3 vilevile askari wa ku patrol njia kuu kuwapiga faini wenye magari mabovu yaliyoacha njiani na kuhakiksha alama zinawekwa kuepusha ajali.
 
Tuma rwmani ya google map hilo eneo
 
Back
Top Bottom