Barabara ya Kimara mpaka Kibaha itazamwe upya, vifo vya watu kutokana na kugongwa na magari vimekuwa vingi sana

Barabara ya Kimara mpaka Kibaha itazamwe upya, vifo vya watu kutokana na kugongwa na magari vimekuwa vingi sana

Hii mada inakuja kwa mara nyingine humu, tuache siasa tuongee ukweli ili marekebisho yawe ya kisayansi sio kisiasa, Ile ni freeway, pedestrians, bodaboda hawatakiwi kuwepo pale, pia tulete wataalamu watufanyie uchunguzi kama ile barabara imejengwa kwa kuangalia usalama wa watumiaji, kuwekwe pedestrians traffic lights 🚥 ambazo zitatumiwa na binadamu wanaotaka kukatiza ile freeway, kujengwe fixed speed cameras to control speed ya magari, na pia tuweke camera's za kurekodi muda ambao gari ina safiri kutoka point A to B,overspending iwe ni fine kubwa(sio spot fine)ila irekodiwe na kumbukumbu za driver, taa za barabarani pale hazifanyi kazi, tuziweke hizi ili visibility iwe nzuri, tuta zote zile futilia mbali ni usumbufu tu
hivi nani alijenga barabara toka pale taa za mnazi mmoja hadi airport mika ya 80? ile barabara ilizingatia vigezo vyote
 
Unajua maana ya high way? Hakuna high way yenye matuta Duniani kote. Jitahidi uwe unaenda nchi za wenzetu uone mambo yakoje barabarani.
Ni sawa usemayo.. Lakini kumbuka kuwa nchi za wenzetu zilizoendelea mara nyingi Hi ways hazIpiti katikati ya miji au kwenye makazi ya watu.. Na inapolazimu Hi way kupita katikati ya mji(Mfano Hi way inayokatisha mji wa Amsterdam kutoka Den Haag kwenda Utrecht) utakuta imejengewa vizuizi ambavyo haviruhusu wakazi wa mji husika kuingia kwenye Hi way hizo..

Sasa kwa hali yetu sisi ambapo barabara inapita kwenye makazi ya watu bila vizuizi vyovyote na kusababisha vifo hatutakuwa na jinsi endapo pesa za kuweka vivuko hazitakuwepo.. Tutalazimika kuwawekea matuta tu.. Madereva wetu wenyewe wavuta bangi na wala mirungi wataweza kufuata sheria za barabarani..?? Sisi kwa suala la usalama barabarani bado tupo nyuma sana.. Leseni zenyewe bado mpaka leo watu wanapata bila hata kupitia driving schools.. Sisi bado sana kujifananisha na nchi zIlizostaarabika..
 
Naanza kwa kuwasalimia wakuu.. Hapa ntaongelea matukio mawili niliyoyashuhudia kwa macho yangu.. Pia ntaongelea matukio machache niliyoyasikia..

Mwezi mmoja uliopita mida ya saa 11 alfajiri nikiwa napita maeneo ya Mbezi mwisho jirani na stendi ya mabasi ya Magufuli nilishuhudia mwili wa mwanamke ukiwa katikati ya matairi ya nyuma ya Lori( Semi Trailer lenye mzigo) dereva wa Lori hilo akiwa amekimbia na kuacha gari ikiwa imenasa mwili wa mwanamke huyo marehemu.

Siku nne zilizopita tukiwa maeneo ya Kibamba Hospitali muda wa saa nne usiku, Kijana mmoja aliwaaga wenzake kuwa anaenda upande wa pili wa barabara atarudi baada ya muda mfupi.. Alipokuwa akivuka barabara aligongwa na gari ndogo tukishuhudia.. Akapoteza maisha palepale..

Miezi miwili iliyopita kijana mmoja ambaye alikuwa katibu wa vijana wa CCM aligongwa akiwa kwenye pikipiki maeneo ya Luguruni na kupoteza maisha palepale..

Miezi kama mitatu iliyopita mama mmoja akiwa anavuka barabara maeneo ya Kibamba CCM aligongwa na Lori(Semi Trailer) na kupoteza maisha palepale..

Sasa nachojiuliza.. TUTASUBIRI MPAKA AFE NANI NDIO TUCHUKUE HATUA..?? Matukio ni mengi sana. Watu wanakufa kwa sababu ya ajali za barabarani.. Wahusika wapo wapi.? Tukumbuke kuwa barabara hii ni Hi way inayopita kwenye makazi ya watu. Huyu mwananchi anayetumia barabara hii tunamlinda vipi kama watu wanakufa kwa kugongwa kwenye Zebra Crossings..??

USHAURI WANGU KWA TANROADS..
Wakandarasi wa TANROADS wabuni vivuko vya kupita chini ya barabara ambavyo ni nafuu kuvijenga ikilinganishwa na madaraja ya kupita juu ambayo yana gharama kubwa zaidi.

Vivuko hivi vitawasaidia waenda kwa miguu, waendesha baiskeli, na hata waendesha bodaboda kuvuka barabara hii bila kuathiri madereva wa magari.. Na nina imani kuwa tutapunguza vifo vitokanavyo na ajali ka kiasi kikubwa sana.

NAOMBA KUWAKILISHA KWA HESHIMA NA TAADHIMA..
Mm bunfsi nilinusurika kugongwa na alphad stop over
 
vivuko vya kupita chini ya barabara ambavyo ni nafuu kuvijenga ikilinganishwa na madaraja ya kupita juu ambayo yana gharama kubwa zaidi.
Ungesema tu waweke vivuko Ila sio kusema kuwa vya chini ama tunnel Ni cheap compared to kivuko Cha juu.
Unaweza ukafanya comparison yake tuone. Yaani Bora ungeita wadau wanaohusika. Ila pengine umeongea vizuri na ikiwekezakana sambaza bandiko lako nbila ya kuwaambia watoe soln gani wao watajua Mana ndio uwanja wao.hizo accident huwa zinarekodiwa. Smt ajali zinatokea due to poor design ambayo Geometric designed condition ya road inashindwana kuendana na driver maneuvering so inatokea. Inafanyika road safety audit Ila before hawajaruhusu itumike. Pia kumbuka na wao Ni binadamu wanakosea.
Pia hakuna dini iliyowahi muua shetani hata huko Kuna Mambo ya ovyo pia.

All in all nakushukuru mno keep it up ,inabidi Kama Taifa tuongee Mambo Kama haya yenye kuokoa maisha ya taifa letu ama mpaka Nani eti afariki.
 
Hapo juu Safi sana umechangia kitaalamu, Ile barabara imejengwa bila kuzingatia usalama wa watumiaji, Ile kampuni na wataalamu wao ni zero, mimi sio engineer wa barabara ila kwa kutumia common sense yangu naona kabisa Ile barabara sio,corners zake, vipimo vyake ni below standard kabisa, kuna kampuni ya China inajenga Ile barabara ya nakonde to chinsali, wapo very slowly ila final product yao ni top class, hawa wa kwetu wametupiga na kitu kizito kichwani
 
alafu tatizo likitokea wanalaumiwa madereva, ila sasa wahandisi nao waweke madaraja rafiki kama manzese na buguruni unavuka kwa mda mfupi, hakuna daraja linatia uvivu kama daraja la kimara hadi uvule upande wa pili ni kama umetembea km moja.
Lile daraja ni amsha Sana , linakera kinyama
 
Harafu kinachonishangaza sio umbali mrefu ila idadi ya ajali ni nyingi sana ukiwa na gari ndogo bora upite kule msata upite Bagamoyo road hiyo ya Chalinze ni kama Chinja chinja fulani hivi maroli pamoja na Bus zinaendeshwa hovyo sana na pana sehemu bara bara imetitia kidogo pale..
 
Lile daraja ni amsha Sana , linakera kinyama
Ila you're safe 100% guarantee otherwise vizia Kama hakuna magari a vuka kwa kukimbia ambapo your life is 50% guarantee i.e anything can happen.limetengenezwa ili ku clear Ile top height ya traffic pia na ku cover needs ya watu wote ikiwemo na disabled people. Shida iko wapi jamani. Unataka liwe fupi baadaye na gari ya urefu fulani isiweze kuvuka kweli
 
alafu tatizo likitokea wanalaumiwa madereva, ila sasa wahandisi nao waweke madaraja rafiki kama manzese na buguruni unavuka kwa mda mfupi, hakuna daraja linatia uvivu kama daraja la kimara hadi uvule upande wa pili ni kama umetembea km moja.
Kwa kweli huyu mkandarasi aliyechora hi michoro ya madaraja ya waenda kwa migu hayupo sawa mtu anatembea KM 1 kuvuka barabara yenye urefu wa mita 10 Kuna na lile la moroco pale na lingine naona linajengwa Mbagala

Wakati wangichimba kwa chini ingekuwa ni rafiki kwa watumiaji pia hata gharama ya ujenzi ingekuwa ndogo
 
Ila you're safe 100% guarantee otherwise vizia Kama hakuna magari a vuka kwa kukimbia ambapo your life is 50% guarantee i.e anything can happen.limetengenezwa ili ku clear Ile top height ya traffic pia na ku cover needs ya watu wote ikiwemo na disabled people. Shida iko wapi jamani. Unataka liwe fupi baadaye na gari ya urefu fulani isiweze kuvuka kweli
Mkuu sio urefu wa kwenda juu tunamanisha design yake ina kona kona unatembea umbali mrefu kuvuka
 
Aliyechora hiyo barabara au aliyepitisha mchoro au aliyekataa mchoro mzuri ndio wa kukamatwa hao...

Kelele za watu zimesaidia ongezeko la daraja la juu Mbezi Mwisho, bila shaka madaraja ya waenda kwa miguu nayo yataongezwa...

Pia bado madaraja ya juu yanahitajika Kimara Stop Over na angalau kwa Msuguri...yawe kama viunganishi vya ile barabara ya pembeni...kwa wakazi wa kuanzia Cha Mkaa hadi Kimara Mwisho...
 
Kwa kweli huyu mkandarasi aliyechora hi michoro ya madaraja ya waenda kwa migu hayupo sawa mtu anatembea KM 1 kuvuka barabara yenye urefu wa mita 10 Kuna na lile la moroco pale na lingine naona linajengwa Mbagala

Wakati wangichimba kwa chini ingekuwa ni rafiki kwa watumiaji pia hata gharama ya ujenzi ingekuwa ndogo
Lile la morocco aisee nlisingizia nna shida ya Achilles tendon kwa guard ili nikatize barabarani
 
sisi waswahili tunashida sana katika matumizi ya barabara, iwe waendesha vyombo vya moto au watembea kwa miguu. waendesha vyombo vya moto hawajali alama za barabarani, watembea kwa miguu nao yapo maeneo wamewekewa miundombinu ya kuvuka lakini hawaitumii, acha tufe labda akili zitatukaa sawa na kujifunza matumizi sahihi ya hizi barabara
 
Aliyechora hiyo barabara au aliyepitisha mchoro au aliyekataa mchoro mzuri ndio wa kukamatwa hao...

Kelele za watu zimesaidia ongezeko la daraja la juu Mbezi Mwisho, bila shaka madaraja ya waenda kwa miguu nayo yataongezwa...

Pia bado madaraja ya juu yanahitajika Kimara Stop Over na angalau kwa Msuguri...yawe kama viunganishi vya ile barabara ya pembeni...kwa wakazi wa kuanzia Cha Mkaa hadi Kimara Mwisho...
Kimara na pale manzese haya madaraja yapo, lakini watu huwa wanavuka chini kwenye barabara za magari, kimara pale hadi ilijengwa fence ya chuma ili watu wasivuke kwa kutumia barabara lakini wako radhi waitafute ile round about ili wavuke kwenye barabara kuliko kuvukia juu. wengi wanaona uvivu mzunguko wa daraja ni mrefu, tanroad wajaribu kujenga underpass waone kama itakuwa rahisi kuvuka chini ya barabara kuliko juu
 
Wasiwasi wangu ni kuwa underpass zitatelekezwa na kuishia kujaa maji ya mafuriko/uchafu chungu nzima kama ilivyo kwa mitaro...

Watanzania, serikali na mamlaka zake za miji hatuna historia nzuri ya utunzaji vitu vinavyohitaji usimamizi/uangalizi wa mara zote...
 
Naanza kwa kuwasalimia wakuu. Hapa ntaongelea matukio mawili niliyoyashuhudia kwa macho yangu.. Pia ntaongelea matukio machache niliyoyasikia.

Mwezi mmoja uliopita mida ya saa 11 alfajiri nikiwa napita maeneo ya Mbezi mwisho jirani na stendi ya mabasi ya Magufuli nilishuhudia mwili wa mwanamke ukiwa katikati ya matairi ya nyuma ya Lori( Semi Trailer lenye mzigo) dereva wa Lori hilo akiwa amekimbia na kuacha gari ikiwa imenasa mwili wa mwanamke huyo marehemu.

Siku nne zilizopita tukiwa maeneo ya Kibamba Hospitali muda wa saa nne usiku, Kijana mmoja aliwaaga wenzake kuwa anaenda upande wa pili wa barabara atarudi baada ya muda mfupi.. Alipokuwa akivuka barabara aligongwa na gari ndogo tukishuhudia. Akapoteza maisha palepale.

Miezi miwili iliyopita kijana mmoja ambaye alikuwa katibu wa vijana wa CCM aligongwa akiwa kwenye pikipiki maeneo ya Luguruni na kupoteza maisha palepale.

Miezi kama mitatu iliyopita mama mmoja akiwa anavuka barabara maeneo ya Kibamba CCM aligongwa na Lori(Semi Trailer) na kupoteza maisha palepale.

Sasa nachojiuliza.. TUTASUBIRI MPAKA AFE NANI NDIO TUCHUKUE HATUA..?? Matukio ni mengi sana. Watu wanakufa kwa sababu ya ajali za barabarani. Wahusika wapo wapi? Tukumbuke kuwa barabara hii ni Hi way inayopita kwenye makazi ya watu. Huyu mwananchi anayetumia barabara hii tunamlinda vipi kama watu wanakufa kwa kugongwa kwenye Zebra Crossings?

USHAURI WANGU KWA TANROADS
Wakandarasi wa TANROADS wabuni vivuko vya kupita chini ya barabara ambavyo ni nafuu kuvijenga ikilinganishwa na madaraja ya kupita juu ambayo yana gharama kubwa zaidi.

Vivuko hivi vitawasaidia waenda kwa miguu, waendesha baiskeli, na hata waendesha bodaboda kuvuka barabara hii bila kuathiri madereva wa magari. Na nina imani kuwa tutapunguza vifo vitokanavyo na ajali ka kiasi kikubwa sana.

NAOMBA KUWAKILISHA KWA HESHIMA NA TAADHIMA.
Wananchi nao wabadili tabia.
Umesema hiyo ni highway, highway hazina zebra rossings hasa za 6 lane!
TANROADS wabuni vivuko vya juu tu hakuna namna, vivuko vya chini vitakuwa makazi ya vibaka.
 
Back
Top Bottom