Barabara ya Mabwepande jinsi ilivyotengwa na CCM

Mkuu umeandika kwa uchungu Sana...sema ndio serikali yetu wameamua kuwadhulumu wananchi waziwazi daah
 
Bila aibu sitoshangaa wakija tena kwa mbinu hii CCM sijui nan kawaroga wizi wazi na kudhulumu haki za wananchi
 
Mkuu Abby uladu mbunge wa huko ni nani ili adhibiwe kwa kutowasemea kero zenu!
Kuna wabunge wawili katika eneo hilo ambao ni Kitila Mkumbo-Ubungo (Robo ya Mabwepande, Mpiji, Makabe, Msumi, Makabe, Kibamba, Kiluvya na Mbezi Msakuzi na Gwajima-Kawe (Madale, Tegeta, Mbezi, Mbweni, Salasala, Goba, Bunju A & B, Mabepande robo tatu, Mbopo, Kinondo, Nyakasangwa
Barabara-Makabe-Msakuzi-Mpiji (Kitila)
Barabara-Njiapanda Mlonganzila-Kibwetere-Mpiji-Mabwepande robo (Kitila)
Barabara-Makabe-Msumi (Kitila)
Barabara-Mabwepande-Bunju (Gwajima)
Barabara-Mbopo-Bunju (Gwajima)
Hizo barabara tajwa hapo juu ikianza mvua ni sawa unasafiri kwendamkioani kupitia barabara ya Ngerengere hadi Kisaki
Mbweni kwenye nyumba za kifahari barabara zake zina lami lakini imeanza baada ya uwepo wa Mabwepande, Bunju na Mbopo na Msumi ni ubaguzi wa hali ya juu sana
 
Iko poa, very natural kama Ngororo vile ambazo watalii wanatoka ulaya kuja kuziangalia.
 
Kada Mkongwe wa CCM na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere ( MNF ) Mzee Butiku si anaishi huko huko ( Nyumba za TBA ) kwanini hawaitengenezi au hata Yeye Mwenyewe kuomba itengenezwe?

Inashangaza sana na Kufikirisha mno.

Mbunge wa eneo husika yuko wapi?
 
Mbunge wa eneo husika yuko wapi?
Ni AsKofu WA Kanisa muda mwingi yupo na Masala ya Kondoo zake. Akizuka Kawe anazukia Waendesha Bajaj na Bodaboda akitumaini hili ninkundi Kubwa la kujipatia Kura ukiwawezesha Maokoto kidogo.
 
Swadakta hakuna ulichobakisha wananchi wa huko wamebaki na maumivu mazito juu ya serikali hii ajabu bado wapo kimya tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…