Barabara za Mji wa Serikali Dodoma zimeshafungwa taa za barabarani

Barabara za Mji wa Serikali Dodoma zimeshafungwa taa za barabarani

Na barabara ya kimara -mbezi -kibaha wamalizie japo waweke hata taa.. Ni miaka miwili tangu mwendazake atangulie na wameipotezea...giza kama porini
 
Wanajitoaga ufahamu tuu hao..Hata Ruto keshawageuka Ma Hustler huko baada ya kuona reality.
Duh,
Sasa tusemeje kama siyo kupungukiwa na akili huku!
Unataka tafsiri unayoitaka wewe ndiyo iwe mawazo ya Ruto?
Amewageuka vipi, wakati ndio anaendelea kuboresha aliyoahidi kwa ufanisi zaidi kutokana na hali inavyoruhusu?

Kuwageuka vipi, kuifanya 'Hustler Fund' kuwa mkopo badala ya grant?

Anayokazia sasa hivi Ruto ndiyo hasa yatakayowaponya waKenya kama hataishia kuyasemea mdomoni tu bila ya kuyatekeleza ipasavyo.

Anakazia waache kukopakopa, na badala yake wajikite katika kukusanya kodi ili zitumike kulipa madeni na kuendeleza nchi yao. Huko ndiko kuwageuka unakokuona wewe?
 
Kila mtanzania mzalendo wa kweli haachi kutaja jina la Magufuli kwa mazuri. Bado nafarijika bado SGR ,Bomba la mafuta na Stigers gorge havijakamilika lakini wapinzani wanakiri kazi zake.
Na UDOM alijengaMagufuli? Wafuasi wa Magufuli ni washamba km yeye mwenyewe. Huo mji anaujenga mama, ndg yenu hakufanya la maana aliuacha ukiwa ndio unaanza kujengwa.
 
Wamapotumia Kodi zetu vizuri kwanini tusiwapongeze?

Kwetu sisi Madereva wa safari ndefu imekosekana Dom Bypass itakayokuwa inatufanya tusiingie Mjini kati ni kero sana
Mbona hiyo ipo, labda useme tu kuwa haijatekelezwa. Ujenzi wa mji ni hatua kwa hatua.
 
Ila wewe na familia yako ndio viongozi wazuri? Kwa taarifa yako unapoteza muda wako tu bure kwani Watz waliowengi wanamheshimu sana Hayati Magufuli na wanakumbuka sana mazuri aliyowatendea, lakini wewe na mafisadi wenzio hamuwezi kumpenda Hayati kwa kuwa aliwathibiti ipasavyo.
Familia zipi? Kama aliyekua makamu wake anamng'onga Kila siku unadhani nani alikua anamkubali zaidi ya wanafiki wachache?

Mfano JPM alipinga chanjo mbona ikaletwa na watu zaidi ya 2M walichanjwa? Same to Alipinga watoto wajawazito wasirudi shule ila Mama karuhusu na sijaona mtu kapinga.... WaTanzania ni wanafiki sana.

Wanaomshabikia JPM ni wasio na elimu ambao walikua wanadanganywa amekamata makontena ya Trillion 450 na wakaamini!!
 
Kasi ya ujenzi wa huo mji imepungua sana.Kuna magorofa zaidi ya 50 ambayo ni ofisi za mawizara,ajabu ni kwamba mengi yametelekezwa bila kuisha,yale yanayoendele kujengwa unakuta mafundi ni wachache sana,gorofa linajengwa na mafundi watano peke yake,.
Acha kueleza uongo hapa. Majengo yote ya ghorofa kwa ajili ya wizara mbalimbali ndio yameanza ujenzi awamu hii ya sita na fedha zipo. Majengo hayo yapo hatua mbalimbali hakuna lililosimama
 
Ni sahihi huo mji wa Mwendazake utapendeza ukikamilika, nimewahi kuutembelea mwaka huu ukiwa kwenye hiyo hatua ya Ujenzi.

Hivi Ikulu imefichwa wapi kwenye huo mji? nahisi imetengwa mbali na eneo la Wizara
Aliyeihamishia serikali Dodoma ni Mwl Nyerere tusijisahaulishe
 
Hii ni dalili kwamba mleta mada ameona chuki za kipumbavu hazisaidii zaidi ya kumuingezea presha
 
Upinzani unakuwa na thamani kama panakuwepo na mindset ya sampuli hii, kuwa unpredictable, sio kupinga tu, kwani ukishazoeleka hivyo watu wataanza kuyapuuza mawazo yako, lakini ukiwa na misimamo tofauti [zuri sifia, baya kemea] kwangu hapa ndipo unachokisema kitasikilizwa.

Kuogopa kusifia kwa kudhani kwamba watatumia hiyo sifa uliyowapa kukukaanga mbele ya safari, kwangu ni hofu tu isiyokuwa na maana.
 
Upinzani unakuwa na thamani kama panakuwepo na mindset ya sampuli hii, kuwa unpredictable, sio kupinga tu, kwani ukishazoeleka hivyo watu wataanza kuyapuuza mawazo yako, lakini ukiwa na misimamo tofauti [zuri sifia, baya kemea] kwangu hapa ndipo unachokisema kitasikilizwa.

Lakini kuogopa kusifia kwa kudhani kwamba watatumia hiyo sifa uliyowapa kukukaanga mbele ya safari, kwangu ni hofu tu isiyokuwa na maana.
Kwa Sasa sifa anapaswa kupewa mama Samia kwa kuendeleza miradi iliyoanza awamu ya tano, maana ana Madaraka kamili ya kuachana na miradi hiyo na kuanzisha ya kwake, wote tunajuwa Rais wa Tanzania kikatiba ni Mungu mtu.
 
Familia zipi? Kama aliyekua makamu wake anamng'onga Kila siku unadhani nani alikua anamkubali zaidi ya wanafiki wachache?

Mfano JPM alipinga chanjo mbona ikaletwa na watu zaidi ya 2M walichanjwa? Same to Alipinga watoto wajawazito wasirudi shule ila Mama karuhusu na sijaona mtu kapinga.... WaTanzania ni wanafiki sana.

Wanaomshabikia JPM ni wasio na elimu ambao walikua wanadanganywa amekamata makontena ya Trillion 450 na wakaamini!!
Nionyeshe mwanafunzi hata mmoja ambaye anamimba anaendelea na masomo!! Siasa hizo.
 
Sasa uwe unashuka na ndege Dar utatamani wafunge madirisha wageni wasione chini kutu juu ya kutu ikitokea bahati tu inashukia upande wa Posta utaona afadhani kidogo lakini ditection ile ya Ilala utasema kambi ya wakimbizi.
Hamia kwa mabwana zako huko. Kwani unalazimishwa kuja TZ?
 
Back
Top Bottom