Barabara zote ni za serikali, polisi wanaweza kukuzuia kuweka gari lako barabarani!

Ila yeye na wenzao wakipita service road au njia sio rasmi ni sawa sawa tu.

Tunawaona mara nyingi, hii nchi kuna watu wanatakiwa kufuata sheria na wengine wapo juu ya sheria, tutafika kweli?
 
Na inaweza kuichukua pia muda wowote ule
Hapa kwenye kuichukua muda wowote ule, unapaswa uelewe kuwa kuna sheria pia
Maana unaandika as if kiongozi/serikali inaweza kuamua tu kuchukua leseni yako bila sababu za msingi. Lazima kuwe na sababu ya msingi inayojitosheleza kumnyang'anya mtu leseni, sio kiholela holela tu
 

na ndicho nilichomaanisha kulingana na kosa, na trafiki karibia wote wanalijua hilo, again ni mara chache sana trafiki anakuwa amekuonea, wengi wa maderva wanaosimamishwa wana makosa lkn hata labda hawajui kama wana makosa au wanajua lkn kiburi, ubabe na dharau vimewajaa ...
 
Serikali ni mwajiriwa wa wananchi, na sisi wananchi ndio walipa Kodi ambazo ndio ujenga barabara.

Kimsingi mwanachi ndie mmiliki wa barabara, hapaswi kubugudhiwa. Kinachohitajika ni kuweka taratibu mzuri na sheria zisizo kandamizi.
 
Hivi kuna serikali bila wananchi? serikali inapata wapi pesa kwaajili ya kujenga miundombinu?

Serikali kama chombo ina mandate ya kusimamia na ku-regulate miundombinu, ila si sahihi kufikiri mwananchi kutumia barabara ni upendeleo
 
Serikali ni Nani?
 
Sawa. Kwani Serikali ni nani? na huyo mtu binafsi ni nani? Askari trafiki ni mtu au Serikali? Tuludi kwenye makosa....Serikali inaweza kukosea au haiwezi kukosea? Je, ikikosea nani wakuiwajibisha? Askari Trafiki hawezi kosea au anaweza ? Je, akikosea nani wa kumuwajibisha?..Je, Huyo mtu binafsi hawezi kufanya kazi mbili.? Serikali na Yake. Tuanzie hapo kwanza. Tusikariri....
 
Kwani serikali ni nini?, ni akina nani? na kwanini wawe na mamlaka makubwa kiasi hicho kiasi cha kuamua lolote? Hii nchi ina wapumbavu wengi sana.
 
Mkuu mtoa posti ni mpumbavu
 
Pumbavu!
 
Unasoma comments za wenzako ili na wewe ujue utachangia nini na kwa namna gani ili kuepuka kurudia-rudia (Tautology)kile kilichokwisha semwa na wenzako. Ndo maana ya mjadala. Ruhusu wadau waisome koment yako lakini nakubaliana na wewe na nakazia hoja kwamba Matusi, Kejeli n.k. sio sahihi
 
Maswali mawili kuntu.
1. Hizo barabara zimejengwa kwa kodi za nani?
2. Hizo barabara zimejengwa kwa ajili ya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…