Barabarani kuna watu wana Immunity, usijaribu kuiga. Sheria haziwahusu

Kabisa ndugu kuna kaukakasi kidogo kwenye hayo mambo ya diplomasia.
Wana kinga nyingi,gari,afisa au nyumba ya ubarozi flani ni nchi husika.

Embu fikiria sasa polisi kuikamata nchi ya uholanzi au uturuki😅😅
 
Kuna jamaa walimtaitisha hivi maeneo flani mbele ya kibaha.itakua wewe.ulikua na ndiga nyeusi
 
Hawajanichoma, mbinu iliyotumika ilikuwa well planned.
Yule askari alisimama barabarani kabisa akawa anafanya ishara ya mdogo mdogo kwa mkono.
Basi itakuwa kuna sehemu trafic wenzie walikuona wakawaambia..!!

Wasingewaomba hao wa ubalozi wapunguze mwendo, walishapewa mchezo mzima na wenzao..!!
 
Watagundua wapi? Nitaongea nao kabisa niwaambie tuko safari moja.
Wanimegee Immunity
😀
Investigative processes.

Wanaweza kukuuliza tu idadi yenu mko wangapi. Jina la madereva ni akina nani?

Ukitaja.. huko mbele wanaweza tu wakauliza jina la dereva mmoja. Nawe ukichemka imekula kwako. Punguza janja janja. Polisi wa barabarani ni waelewa ukiongea nao bila ujanja ujanja.
 
Pole sana kwa yaliyokukuta.

Siku nyingine unga na yale magari ya BOT (zIle za grey zinazopeleka hela). Halafu njoo usimulie hapa.

Iliwahi kunikuta, polisi akaniambia nakimbiza gari ya BOT 😀 hapo Mkuranga tu nikiwa naelekea Mtwara.

Baada ya ile kauli nikamtazama yule askari nikajikuta ninacheka na yeye akacheka, kisha akaniambia ''bwana mdogo, usilete uhuni barabarani'' akanipa leseni yangu, nikaendesha kwa nidhamu ya hali juu kutoka Mkuranga mpaka Mikindani.
 
Hao wa Bot walinikwangua ,alafu ndio vile hawasimamagi,niliwaungia mpaka walisimama .walinilipa aisee.
 
Nimeshakutambua na wakati mwingine usirudie tena. Utakutana na kitu kizito.
A
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…