Barabarani kuna watu wana Immunity, usijaribu kuiga. Sheria haziwahusu

Barabarani kuna watu wana Immunity, usijaribu kuiga. Sheria haziwahusu

Pole sana kwa yaliyokukuta.

Siku nyingine unga na yale magari ya BOT (zIle za grey zinazopeleka hela). Halafu njoo usimulie hapa.

Iliwahi kunikuta, polisi akaniambia nakimbiza gari ya BOT 😀 hapo Mkuranga tu nikiwa naelekea Mtwara.

Baada ya ile kauli nikamtazama yule askari nikajikuta ninacheka na yeye akacheka, kisha akaniambia ''bwana mdogo, usilete uhuni barabarani'' akanipa leseni yangu, nikaendesha kwa nidhamu ya hali juu kutoka Mkuranga mpaka Mikindani.
Kazini kwako kulikuwa kuna kazi
 
Kabisa ndugu kuna kaukakasi kidogo kwenye hayo mambo ya diplomasia.
Wana kinga nyingi,gari,afisa au nyumba ya ubarozi flani ni nchi husika.

Embu fikiria sasa polisi kuikamata nchi ya uholanzi au uturuki😅😅
Wanaziendesha mbona ni wabongo kabisa! Weusi wenzetu
 
Namaanisha sheria za Barabarani,

Leo walitaka kunilaza ndani.
Nimefuata gari zenye namba za kibalozi! Ilikuwa rahisi hadi niliposimamishwa na Polisi muda mchache baada yakuvuka Mkata.

Barabara ya Dar - Moshi.

Hawa jamaa wako na gari mbili LC 300 wamenikuta Msata kuna kimgahawa pale nimewaacha ila baada ya kama dakika 10, wakanipita kabla yakufika Mandera.

Nikaona ni kampani nzuri nikaunga nyuma yao, hawajali 50 kabisa.
Niliweza mwendo wao kwasababu Speed yao ilikuwa moderate sana 120kph-150kph .

Wao mbele mimi nyuma, hakuna Traffic anayewapiga mkono, vuka Kimange, vuka Mbwewe!

Tumevuka Mkata, mbele kabisa, naona Police amesogea road kabisa akawataka wale jamaa wapunguze mwendo, Kumbe lengo lilikuwa ni mimi, jamaa walivyopunguza mwendo traffic akafanikiwa akanisogeza pembeni! Washkaji wakaondoka zao.

Mitifuano ya kisheria ikaanza baina yangu na Police, kosa langu ilikuwa overspeed, wakati kuna wenzangu wao hilo haliwahusu kabisa.

Mkuu wa kituo waliponirudisha (ilibidi nipelekwe) akaniambia wenzio wana Immunity, sio kila kitu cha kuiga.

Nimelipa fine japo kwa tabu sana.

Nauliza hizi Immunity zinawaweka wengine juu ya sheria? Why
Mkuu pole sana
Mimi niliwahi ingilia msafara wa mama kizi mkaxi akuwa ni DP
Nakumbuka alikuwa anatoka morogoro wakaniacha mita kama 200
Tumetoka chalinze kufika kibaha nikakuta gari moja ipo njiani kilichofuata ni kuwekwa lock up mungu saidia kuna walio unga bodi nyuma
From that date to date sifanyi hiyo kitu
 
Kajishughulishe kusoma Vienna convention on diplomatic relations ya 1961 utajua vizuri. Kila kitu kipo wazi ukiipitia
Kimsingi hawaruhusiwi kuvunja sheria za barabarani na polisi ana mamlaka ya kuwasimamisha. Kitu ambacho hawezi kufanya ni kuwapa adhabu ya hapo kwa papo ila anaweza kuandika ripoti ambayo serikali ya nchi husika inaweza kutumia channels za wizara ya mambo ya nje kulalamika.
 
Sio rahisi, wakiwa napesa huwa wanakispika kabisa wanatangaza usisogelee msafara wao.
Na ubaya huwa hawazidi speed 100kph inawezekana yale magari yao ni Armoured
Situation ilikua tofauti aisee ,nimewapisha pembeni kabisa .wakanikwangulia uko uko pembeni,haikua damage kubwa sana ,lakini niliitaji kulipwa ,na wao walikua ilo wakiendelea kupoteza muda na Mimi na gari inaangariwa muda wote inaposimama ,wao ndio wangepoteza sio mimi.wakanipa lakki tatu chap ,nikatengeneza kwa Elfu hamsini ,mbili na nusu nikala bia.na niliwakuta wastarabu ,vinginevyo nisingelamba ata mia
 
Kimsingi hawaruhusiwi kuvunja sheria za barabarani na polisi ana mamlaka ya kuwasimamisha. Kitu ambacho hawezi kufanya ni kuwapa adhabu ya hapo kwa papo ila anaweza kuandika ripoti ambayo serikali ya nchi husika inaweza kutumia channels za wizara ya mambo ya nje kulalamika.
Mlolongo kumbe
 
Mkuu pole sana
Mimi niliwahi ingilia msafara wa mama kizi mkaxi akuwa ni DP
Nakumbuka alikuwa anatoka morogoro wakaniacha mita kama 200
Tumetoka chalinze kufika kibaha nikakuta gari moja ipo njiani kilichofuata ni kuwekwa lock up mungu saidia kuna walio unga bodi nyuma
From that date to date sifanyi hiyo kitu
Yeah! Najua makosa kuingilia misafara iliyopo kisheria.
Unaenda lockup moja kwa moja.
 
Hao Plate za Kijani, STM SU na DFPA huwa wanatubeba sana.
Unamkalia hapo takoni 🤣 kama una haraka.
Tatizo trafic wakikuona wanawapa taarifa wenzao wa mbele, wadwanzi kweli 😹😹

Sema kwenye kuover take sehemu linaweza kukuuzia kicheche ukajikuta mmepigana busu na scania 😹😹😹
 
Back
Top Bottom