Barabarani kuna watu wana Immunity, usijaribu kuiga. Sheria haziwahusu

😹😹😹 Alitaka kukukomesha sasa hayo yote ya nini jamani..!!

Kweli kuna wengine wako vizuri mimi nishakutana na watu wa hivyo sana.
Tatizo gender yangu wanaanza approach za kifala but sometimes mpk wese wananipea 🤣
Mpaka wese?
Halafu nilikuahidi road trip.
Unanafasi next week tuende Simiyu?
 
Niliona siku moja nipo kwa basi naenda dodoma,kenge mbili bmw salon na crown vimeng’ata tako la V8,nikasema huu sio uendeshaji
Ujue kuna sababu!
Ishu ni kuwa makini tu.
Na unasogea karibu sehemu ambayo ina kizuizi.
Na ni halali kwanini wao wasisimamishwe sisi tusimamishwe?
Advantage can be taken.
 
Ukiiga tembo kunya, kundu pasuka. Kwako wewe imekuwa fuko pasuka kwa kulipa fine.
 
Wewe ni mjinga sana, tii sheria za barabarani kwa usalama wako na chombo chako cha usafiri na watumiaji wengine wa barabara.

Sheria za barabarani ni kwa faida yako mjinga mkubwa wewe
Umaskini ni mbaya sana!
Punguza hasira
 
Kuna mawili, either walikureport “kuna unknown car nyuma yetu inatufatilia” ama traffic mliowapita wamekuchoma kwa wenzao kuna kigari kimeunga em kikamateni. Walikufanyia roho mbaya tu
 
Wawekwe wazi kuwa wako exempted kwenye sheria za Barabarani

Wanadiplomasia Wana immunity ya kisheria ya kutokushitakiwa kwenye suala zima la Uvunjaji wa Sheria za nchi mwenyeji wanakofanyia kazi zao za kidiplomasia. Soma vizuri ule Mkataba wa Kimataifa wa Vienna. Wana kinga pia hata kwenye makosa ya jinai, mathalani, ikitokea Balozi wa Nchi ya nje akafanya kosa la Mauaji hapa Tanzania, kamwe hawezi kushitakiwa katika Mahakama za hapa Tanzania kwa kosa hilo la Mauaji. Labda Serikali itakachofanya ni kumfukuza hapa nchini na aondoke mara moja ndani ya Mipaka ya Nchi hii, lakini siyo kumfikisha Mahakamani.
Wanadiplomasia wanaweza kushitakiwa Mahakamani wao wenyewe binafsi kutokana na makosa fulani fulani tu maalumu ambayo yameainishwa kwenye Mkataba huo wa Vienna, na wala siyo vinginevyo.
 
bas ni seme gar zenye p no za kigeni nyingi hawazingatii sheria na hawachukuliwi hatu tofauti na zile za ndani..napo hujaelewa?
Gari zenye usajili wa Namba za kutoka nje ya nchi hazina immunity ya kuvunja Sheria za Usalama Barabarani, wanaweza kutozwa faini endapo kama watavunja Sheria hizo. Unless gari hizo ziwe za Wanadiplomasia ambao wapo kikazi katika Nchi ya ugenini, na gari husika ziwe na usajili maalumu Kama gari za taasisi za kimataifa.
 
Sawa, watumishi wa umma mfano, Mwalimu,Daktari,Polis n.k nani anaruhusiwa kumiliki gari yenye plate no za nje ya nchi mfano Congo,Kenya,Uganda,Zambia na Malawi?
 
Sawa, watumishi wa umma mfano, Mwalimu,Daktari,Polis n.k nani anaruhusiwa kumiliki gari yenye plate no za nje ya nchi mfano Congo,Kenya,Uganda,Zambia na Malawi?
Wanaruhusiwa ndiyo, lakini katika Mazingira fulani fulani maalumu tu na kwa sababu au kwa wakati maalumu tu.
Hata wewe binafsi pia unaruhusiwa kisheria, lakini kutokana na sababu hizo hizo. Soma vizuri Sheria za Usalama Barabarani pamoja na Sheria nyinginezo za nchi hii kuhusiana na suala hili. Pitia Sheria za TRA kuhusiana na taratibu za suala hili la usajili wa Vyombo vya Moto
 
Ndugu mleta mada si kila kitu utaambiwa ili ujifunze mengine lazima ukutane nayo ili ujifunze na uwe mwalimu kwa wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…