Asalamaleko!
Mimi ninaishi Dar es salaam maeneo yenye kusongamana sana.
Watu ni wengi mno na wanapumuliana uso kwa uso kwa namna ambayo endapo kungekuwa na gonjwa la mlipuko basi wangekufa wote kama kuku wenye mdondo.
Huku sijasikia mtu yeyote aliyekufa kwa corona. Hakuna hata sisimizi aliyekufa.
Lakini tunaona Bibi Samia amejivika mibarakoa mikubwa usoni kama afisa-mazingira.
Ndio kusema kwamba, anajikinga na corona?
Halafu inaonekana corona inachagua mahali rasmi pa kupiga kambi. Kwa sasa corona imehamia ikulu!
Kama ambavyo dunia nzima imepata nafuu na maisha yameanza kurejea katika hali ya kawaida, kirusi huyu wa corona tunaambiwa amehamia India.
Kote kwingine duniani, corona amefifia na kufa makali, kakimbilia kwenda India kuweka makazi.
Huyu Kirusi ana akili sana. Sasa hivi hayupo Kariakoo wala Manzese wala Buza. Kakimbilia kwenda kujificha Ikulu.
Wow! What an intelligent virus! Anajua mahali pa kukaa. Anahama kule anahamia huku tena kwa ratiba rasmi kabisa.
Leo yupo Marekani, kesho anahamia South Africa, Kesho kutwa anahamia India. A very systematic virus!
Chanjo zinakuja lini?
Halafu pia lockdown itaanza lini?
Huyu kirusi akitoka magogoni akihamia hapa Kariakoo itakuwaje!?
Tunahitaji hatua madhubuti zichukuliwe mapema!
Kila mtu avae mabarakoa na kujitakasa mikono!
View attachment 1780570