Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Hv mpaka Leo bado mnawaza Mambo ya dini Tena dini zenyewe za mwarabu na mzungu.. Huu ndio wazimu wenyewe
 
Heri yetu tusie na Dini,lakin nimejiuliza sana mkuu umeanzaje kukaa na kuanza kuwaza suala la udini kwenye teuzi me nadhan wewe ndo mbaguz nambari moja.

Me nadhan teuzi zinafanyika kutokana na uwezo na weledi wa mtu na si dini,mkoa au kabila.

Hata lingejaa waislamu wote as long wana deserve me sion shida na wote n watanzania wanafanya kaz kwa maslahi ya taifa hili.
Afu izi din sio zetu mkuu achana na ayo mambo ni ujinga mtupu
Jee unamaanisha hawanauwezo na hawa deserve to be part of the central Government?
 
Tumwache Rais wetu afanye kazi, Tuache uchonganishi alichofanya ni sahihi,,kwani tunataka watu wa kanisani au msikitini???Tunataka watendaji...Toeni udini wenu huko.
Waislamu sio watendaji
 
b) Hili ni baraza la Tanganyika, Yawezekana vipi usiwe na baraza lenye waziri kamili hata mmoja Mzanzibar?

Naomba nifahamishwe pia kwenye Baraza la Mawaziri Zanzibar kuna mtanganyika alishawahi kuteuliwa nafasi ya uwaziri[emoji23]
Adam Mwakanjuki
 
Mkuu naona point yako kubwa ipo kwenye namba 1, uongo? haya mengine umechomekea tu ili usionekane mdini.
 
Mwenye kujua kule Zanzibar Kuna mawaziri wangapi wasio waislamu anijuze please.
 
Kwani ni lazima kuteua waziri toka huko wapi katiba imesema hivyo mbona wao hawateui toka bara!
Akili ndogo utaijua tu. Unaelewa baraza la huko ni rais wao ndo anateu ambaye siye rais wa JMT.

Lakini huyu wetu Tanganyika ni rais hadi huko zenji.

Ama nikuchoree hapa hesabu za set uelewe vzr.

Kipara weee.
 
Kwani wameteuliwa kwenda kusoma Quran au biblia au kwenda kufanya kazi? Tufike mahali mtu ateuliwe kwa kufuata uwezo wake wa kutenda kazi na sio dini wala rangi yake wala jinsia yake. Ni wazi mtoa maada ilitakiwa ushitakiwe kwa kuonyesha ubaguzi hadharani kabisa. Unaonyesha ubaguzi wa kidini hadharani hao watu wameteuliwa wakafanye kazi na sio kwenda kuhubiri.
Jinsi ulivyoandika tu unaonekana umejawa na udini, kwa nini haitokei hata kwa bahati mbaya siku moja waislam wakateuliwa wengi kuliko wakristo hata kwa 60% tu? Miaka ya nyuma mlikuwa mnajificha kwenye kichaka kua waislam wengi hawkuwa na elimu ya juu.. Lakini Leo waislam wengi wasomi.. Sura ya udini wakati huu haijifichi sema tu mhusika mkuu hujifanya hajali lolote anashupaza shingo kama farao wa misri.
 
Ndugu zangu Waislam bara na visiwani msiwe mashaka. Mwenyezi Mungu yupo na atayajibu. Ila niwakumbushe mnawatu imara Sana pale juu kuanzia Jaji Mkuu, Waziri Mkuu na Mam Samia. Msimsahau waziri Jafo Ila Jaji Mkuu embu ndugu wa Islam msimsahau huyu Mh ktk Salah zenu mwekeni mbele za Mungu Jaji Mkuu wa Taifa. Hili. Amin
Hapo kwa jaji mkuu sio kweli, ni mkatoliki pure.. Hilo ni jina tu.
 
Kiongozi anayetaka maendeleo ya nchi yake hana woga na wale ambao anahisi wana uwezo kuliko yeye. Magufuli mara nyingi ana complex ya kuwaogopa wale anaodhani wana akili kuliko yeye na hilo liko wazi kwenye uteuzi wa baraza lake la mawaziri!!! Kuna qualities tatu zinazoangaliwa na kiongozi mahili katika kuwateua wasaidizi wake nazo ni :- MERITOCRACY [Umahili] ; PATRIOTISM[ uzalendo] na INTERGRITY[ Hadhi/Heshima].

Kama Magufuli angetumia vigezo hivyo na kuweka complexes zake kando angekuja na Baraza la mawaziri bora kuliko hili alilotangaza na lingewajumuisha mawaziri wa zamani Prof. Mbarawa na Japhet Hasunga!!!!
 
kila mahala uwiano ni muhimu sana ktk kujenga umoja na maelewano, ni vyema kila kiongozi aliye pewa dhamana akalitazama hilo kwa nia njema ya kujenga umoja wenye nguvu ya pamoja kwa taifa letu kwa kuzingatia taaluma weledi na uadilifu, tusipo litazama jambo hili kuna hatari ya kutugawa siku za mbeleni, sio tu kwenye nafasi za uwaziri bali ktk kila idara za serikali ni muhimu viongozi wake wakalitazama hilo bila kuona aibu kwa maslahi ya nchi yetu, Mungu ibariki Tanzania
 
AHADI YA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE KWA WAISLAM 1962

Haiwezekani kuielewa ahadi ya Nyerere katika haki na usawa kwa raia wote kama alivyoahidi wakati wa kudai uhuru, hadi usome hotuba yake aliyoitoa tarehe 10 Desemba, 1962 katika Bunge wakati Tanganyika inakua jamhuri.

Hotuba ya Nyerere ilijikita kwenye matatizo ya upogo kati ya Waislam na Wakristo.

Nyerere alikuwa na haya ya kusema:

‘’Hakuna njia nyepesi ya kuondoa tafauti baina ya raia wetu Waafrika na wasio Waafrika; hakuna njia nyepesi ya kuondoa tofauti za elimu kati ya Wakristo na Waislam, au baina ya wachache wenye elimu na wengi wa watu wetu wasio kuwa na elimu; hakuna njia nyepesi ambayo Wamasai na Wagogo wanaweza wakalingana na Wahaya na Wachagga na Wanyakyusa.’’

Hii ilikuwa kauli ya serikali ya kudhihirisha nia yake njema kwa Waislam.

Kauli hii ilikuwa ya kuwapa matumaini na kuwahakikishia Waislam na wale wote walioathirika na dhulma ya wakoloni, kuwa serikali ilikuwa inatambua shida zao na itachukua hatua zifaazo kurekebisha hali hiyo.

Bila shaka Nyerere alisema maneno haya akitambua mchango mkubwa wa Waislam wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nyerere alisema maneno haya akijua kuwa ingawa yeye alikuwa Rais Mkatoliki lakini Waislam kwa nia ya kuleta umoja wa Watanganyika chini ya TANU na kupigania uhuru hawakusita kumuunga mkono kwa dhati.

Na siku alipoacha uongozi baada ya kutawala kwa robo karne Mwalimu Nyerere katika hotuba yake maarufu ya kuaga aliyotoa Diamond Jubilee Hall alikuwa na haya ya kusema:

''Waislam wametupa nafasi kupitia sera yetu ya elimu, kurekebisha upogo.

Sasa nipo katika hali ya kufurahisha kwa kuwa wakati mwingine sielewi kama Mbunge mpya, Waziri, au Katibu Mkuu katika wizara zetu za serikali, ni Muislam au Mkristo au hana dini labda pale jina lake la kwanza linapotoa utambulisho.

Na hata hivyo hiyo siyo njia ya kuaminika kutoa utambulisho wa dini kwa kuwa tuna Wakristo wenye majina ya Kiislam, na Waislam wenye majina ya Kikristo.

Kuvumiliana huku nyie ndiyo sababu; nilichofanya mimi ni kuzungumzia maadili haya kwa niaba yenu.''

Huyu ndiye Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyoeleza tatizo la Waislam na jinsi alivyolitatua.

Yapo mengi ambayo yangewezwa kuelezwa kuhusu ukweli wa kauli hii lakini tutosheke na haya.

Leo Waislam wanatatazika na idadi yao katika Baraza la Mawaziri lililo na Waislam 3 dhidi ya Wakristo 20.

Picha ya kwanza kulia ni Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Max Mbwana na Mwinjuma Mwinyikambi mwaka wa 1962.

Picha ya pili ni Mshume Kiyate na Julius Nyerere 1964 na picha ya tatu ni kulia Haruna Taratibu, Saadan Abdu Kandoro, Julius Nyerere, Sheikh Mohamed Ramia na Iddi Faiz Mafungo wakiwa Dodoma 1956.

Screenshot_20201207-063029.jpg
 
Jinsi ulivyoandika tu unaonekana umejawa na udini, kwa nini haitokei hata kwa bahati mbaya siku moja waislam wakateuliwa wengi kuliko wakristo hata kwa 60% tu? Miaka ya nyuma mlikuwa mnajificha kwenye kichaka kua waislam wengi hawkuwa na elimu ya juu.. Lakini Leo waislam wengi wasomi.. Sura ya udini wakati huu haijifichi sema tu mhusika mkuu hujifanya hajali lolote anashupaza shingo kama farao wa misri.
Well said
 
kila mahala uwiano ni muhimu sana ktk kujenga umoja na maelewano, ni vyema kila kiongozi aliye pewa dhamana akalitazama hilo kwa nia njema ya kujenga umoja wenye nguvu ya pamoja kwa taifa letu kwa kuzingatia taaluma weledi na uadilifu, tusipo litazama jambo hili kuna hatari ya kutugawa siku za mbeleni, sio tu kwenye nafasi za uwaziri bali ktk kila idara za serikali ni muhimu viongozi wake wakalitazama hilo bila kuona aibu kwa maslahi ya nchi yetu, Mungu ibariki Tanzania
Huyu mtawala wetu ni mbaguzi haswa wa nyaja zote
 
Back
Top Bottom