Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Bakwata ni Tawi la CCM na ndiyo walalamikaji wakuu
Hakuna Bakwata anayelalamika. Awamu hii imejenga msikiti wa mabilioni pale kinondoni, hawawezi kulalamika.

Mleta mada analeta mindset za udini, watu wanataka waone kazi inafanywa na ilani ikitekelezwa kwa vitendo, masuala ya dini ni huko huko makanisani na misikitini.
 
Jinsi ulivyoandika tu unaonekana umejawa na udini, kwa nini haitokei hata kwa bahati mbaya siku moja waislam wakateuliwa wengi kuliko wakristo hata kwa 60% tu? Miaka ya nyuma mlikuwa mnajificha kwenye kichaka kua waislam wengi hawkuwa na elimu ya juu.. Lakini Leo waislam wengi wasomi.. Sura ya udini wakati huu haijifichi sema tu mhusika mkuu hujifanya hajali lolote anashupaza shingo kama farao wa misri.
Tatizo analopata anayeunda Baraza ni kuwa ingawa wingi wa wananchi wa Tanzania Wakristo na Waislam ni karibu 50/50 lakini Wasukuma Wakristo ni wengi kuliko Waislam ndo maana wateuliwa Waislam hawapo. Hata Pascal Mayalla ni Mkristo akiteuliwa ataongeza namba ya Wakristo!
 
Nikiangalia hili baraza la mawaziri, by all standards haliakisi sura ya Taifa na kwa hiyo halisaidii kwa namna yoyote kuimarisha umoja wa Kitaifa.

1. Hivi inawezekana vipi uje na baraza la Mawaziri la watu 23 lakini lenye Waislamu 3 tu?

Takwimu hizi ni 87% Wakiristo, na 13% Waislamu. Je, hii maana yake ni kwamba asilimia kubwa ya watu wanaoweza kufanya kazi ya kuendesha serikali yetu katika nchi yetu more than 80% ni watu wa dini moja? Hili linaacha maswali mengi. Lakini haya sishangai, inaonyesha tu kuhusu ujeuri wa mamlaka za uteuzi, Waislamu hili suala wamelilamikia sana, Mwaka 2016 Sheikh Khalifa alilisemea, Kisha mwaka huu kwenye Waraka wa shura ya maimamu Sheikh Ponda alilisema.

Binafsi sioni kama ni weledi wa kiungozi kutoheshimu demography za nchi yako katika kuunda timu ya kufanya nayo kazi. Naiona kama ni udini wa dhahiri tu ambao unashuhudiwa na aina ya teuzi zilizofanyika toka muhula wa kwanza wa serikali hii!. Je, Waislamu wanapenda haya? - La hasha, lakini pamoja na hayo Wa kulaumiwa pia ni viongozi wao, hawajitambui, hawajielewi, wanapigana mishale wao kwa wao badala ya kusimama kwa sauti moja ya kuangalia maslahi ya watu wao. Angalau Sheikh Ponda anajitambua, aliliona hili.

2. Baraza la Mawaziri halina Waziri hata mmoja kutoka Zanzibar
Zipo wizara za muungano, hakuna waziri hata mmoja wa wizara hizo ambaye ni Mzanzibar. Ni yaleyale niliyoyasema kwenye nukta ya juu. Huwezi kuunda timu ya mambo ya nchi isiyozingatia demography za kitaifa. Kwa mfano Huwezi mathalani ukachukua watu kutoka Kanda moja ukaunda baraza la mawaziri halafu ukasema eti hawa vigezo vyao vinatosha, Well hata kama vinatosha je wao peke yao ndo wenye vigezo? . Lakini katika hili Wazanzibar wa CCM nao wajilaumu wenyewe, Wameamua kuitoa nchi yao kwa Tanganyika "iwasimamie" basi wacha nchi yao igeuzwe mkoa, yaani hata mawaziri kutoka kwao ni hiyari tena kama ilivyo mawaziri kutoka Mtwara, Mwanza au Tanga

3. Idadi ya Wanawake ni ndogo katika baraza zima la Mawaziri

Sijajua kama ilikuwa ni vision ya kitaifa au ni maono ya kiuongozi tu wa serikali za awamu ya tatu na nne. Lakini kuna kipindi tumewahi kuwaza 50/50. Japo kwa maoni yangu hiyo siyo hoja, lakini kwangu hoja ya msingi ilikuwa ni kuwa lazima katika vyombo vya mamlaka na maamuzi jinsia zote zionekane vizuri siyo kuwa na mfumo uliolalia upande mmoja kupita kiasi (mfumo dume), Sasa wanawake wa kutosha wapo, kwa nini baraza la mawaziri liwe na wanawake kiduchu sana kwenye hili baraza?

Kwa hiyo ukiniuliza kuhusu hili baraza nitakwambia kuwa:
a)
Hili baraza linanuka udini, ni as if Magufuli katuletea parokia ya Mtakatifu Joseph, haliakisi demography ya kitaifa ya kwamba nchi hii ina watu wengi wa imani zote hizi mbili. Nilitegemea kuona baraza lenye sura ya kitaifa, lakini naona baraza lenye sura ya Tanzania ya Kikristo zaidi

b) Hili ni baraza la Tanganyika, yawezekana vipi usiwe na baraza lenye waziri kamili hata mmoja Mzanzibar?

4) Ni baraza la Mfumo dume - Ratio ya akina mama katika baraza hilo siyo wakilishi, sioni ni kwa namna gani baraza hilo linasaidia kuondoa mfumo dume

Namshauri Magufuli atengue hilo baraza kabla ya kuliapisha. La sivyo litampa tabu kwenye kubalance force za kijamii za kitaifa.

Katika kipindi hiki ambapo jumuia ya kimataifa inamnyooshea kidole juu ya aina ya utawala wake, ingekuwa busara kujaribu kubalance force za ndani, ingemsaidia sana.

Ila akizidi kukataliwa ndani ya nchi na nje ya nchi, basi ajiandae kutumia miguvu zaidi kutawala katika kipindi hiki cha miaka mitano, kwa sababu kutakuwa na silent rejection ya utawala wake ndani ya nchi na hii itamsumbua sana!
Hapo ndipo serikali zinapoanza kufail..haiwezekan umchague mtu kufuatana na dini yake au kabila yake.. never should and will it be like that.
Chagua mtu kwa kufuata uwajibikaji wake na CV yake kwa ujumla..kwenye hiyo nafasi..kama hujui historia kaa kimya..nikudokeze tu.
Wakat wa mwalimu kuna kwenye suala la kuchagua nani ashike wapi..kuna dini ikataka watu wake nao wachaguliwe ambao walikuwa wakiijua tu dini yao bila kuwa na elimu dunia ya kiungozi na uzoefu wa aina yyte pas na uzoefu wa kwenye dini yao..mwalimu akawaambia somesheni watoto wenu elimu dunia mana serikal haina dini wala haichagui mtu kuja kuongoza kidini au kikabila bali inachagua mtu kuangalia umahiri wake katika nafasi husika..
Suala la kusema usawa wa kiiman au kikabila ni upuuzi wa hali ya juu kwa dunia hii ya sasa..watu wanapaswa kuchaguliwa kulingana na umahir wao katika kutenda kaz.
Japo ikiwa itabainika kufanywa kwa kitendo hicho bas mamlaka husika zinaweza kushughulika na suala hilo mana wanadamu pia wanamapungufu yao
 
Nikiangalia hili baraza la mawaziri, by all standards haliakisi sura ya Taifa na kwa hiyo halisaidii kwa namna yoyote kuimarisha umoja wa Kitaifa.

1. Hivi inawezekana vipi uje na baraza la Mawaziri la watu 23 lakini lenye Waislamu 3 tu?

Takwimu hizi ni 87% Wakiristo, na 13% Waislamu. Je, hii maana yake ni kwamba asilimia kubwa ya watu wanaoweza kufanya kazi ya kuendesha serikali yetu katika nchi yetu more than 80% ni watu wa dini moja? Hili linaacha maswali mengi. Lakini haya sishangai, inaonyesha tu kuhusu ujeuri wa mamlaka za uteuzi, Waislamu hili suala wamelilamikia sana, Mwaka 2016 Sheikh Khalifa alilisemea, Kisha mwaka huu kwenye Waraka wa shura ya maimamu Sheikh Ponda alilisema.

Binafsi sioni kama ni weledi wa kiungozi kutoheshimu demography za nchi yako katika kuunda timu ya kufanya nayo kazi. Naiona kama ni udini wa dhahiri tu ambao unashuhudiwa na aina ya teuzi zilizofanyika toka muhula wa kwanza wa serikali hii!. Je, Waislamu wanapenda haya? - La hasha, lakini pamoja na hayo Wa kulaumiwa pia ni viongozi wao, hawajitambui, hawajielewi, wanapigana mishale wao kwa wao badala ya kusimama kwa sauti moja ya kuangalia maslahi ya watu wao. Angalau Sheikh Ponda anajitambua, aliliona hili.

2. Baraza la Mawaziri halina Waziri hata mmoja kutoka Zanzibar
Zipo wizara za muungano, hakuna waziri hata mmoja wa wizara hizo ambaye ni Mzanzibar. Ni yaleyale niliyoyasema kwenye nukta ya juu. Huwezi kuunda timu ya mambo ya nchi isiyozingatia demography za kitaifa. Kwa mfano Huwezi mathalani ukachukua watu kutoka Kanda moja ukaunda baraza la mawaziri halafu ukasema eti hawa vigezo vyao vinatosha, Well hata kama vinatosha je wao peke yao ndo wenye vigezo? . Lakini katika hili Wazanzibar wa CCM nao wajilaumu wenyewe, Wameamua kuitoa nchi yao kwa Tanganyika "iwasimamie" basi wacha nchi yao igeuzwe mkoa, yaani hata mawaziri kutoka kwao ni hiyari tena kama ilivyo mawaziri kutoka Mtwara, Mwanza au Tanga

3. Idadi ya Wanawake ni ndogo katika baraza zima la Mawaziri

Sijajua kama ilikuwa ni vision ya kitaifa au ni maono ya kiuongozi tu wa serikali za awamu ya tatu na nne. Lakini kuna kipindi tumewahi kuwaza 50/50. Japo kwa maoni yangu hiyo siyo hoja, lakini kwangu hoja ya msingi ilikuwa ni kuwa lazima katika vyombo vya mamlaka na maamuzi jinsia zote zionekane vizuri siyo kuwa na mfumo uliolalia upande mmoja kupita kiasi (mfumo dume), Sasa wanawake wa kutosha wapo, kwa nini baraza la mawaziri liwe na wanawake kiduchu sana kwenye hili baraza?

Kwa hiyo ukiniuliza kuhusu hili baraza nitakwambia kuwa:
a)
Hili baraza linanuka udini, ni as if Magufuli katuletea parokia ya Mtakatifu Joseph, haliakisi demography ya kitaifa ya kwamba nchi hii ina watu wengi wa imani zote hizi mbili. Nilitegemea kuona baraza lenye sura ya kitaifa, lakini naona baraza lenye sura ya Tanzania ya Kikristo zaidi

b) Hili ni baraza la Tanganyika, yawezekana vipi usiwe na baraza lenye waziri kamili hata mmoja Mzanzibar?

4) Ni baraza la Mfumo dume - Ratio ya akina mama katika baraza hilo siyo wakilishi, sioni ni kwa namna gani baraza hilo linasaidia kuondoa mfumo dume

Namshauri Magufuli atengue hilo baraza kabla ya kuliapisha. La sivyo litampa tabu kwenye kubalance force za kijamii za kitaifa.

Katika kipindi hiki ambapo jumuia ya kimataifa inamnyooshea kidole juu ya aina ya utawala wake, ingekuwa busara kujaribu kubalance force za ndani, ingemsaidia sana.

Ila akizidi kukataliwa ndani ya nchi na nje ya nchi, basi ajiandae kutumia miguvu zaidi kutawala katika kipindi hiki cha miaka mitano, kwa sababu kutakuwa na silent rejection ya utawala wake ndani ya nchi na hii itamsumbua sana!
Binafsi sikutarajia na wala sitarajii jambo lolote POSITIVE kutoka kwako, Missile of the Nation, au kutoka kwa Lissu au Bob juu ya lolote litakalofanywa na Serikali hii ya CCM ILA unafiki, uzandiki, mapandikizo ya chuki, machonganishi ya aina zote za uzushi, na zaidi ya yote UCHOCHEZI. Hayo ya ukanda, udini, ubaguzi wa jinsia na mengine machafu na ya UONGO kwenye bandiko hili - mliyasema mwaka 2015 na leo mnayarudia tena na zaidi kwa mashinikizo na kutumwa na Lissu kwa nia na malengo ya kututoa kwenye reli na ajenda zetu za maendeleo. Kwa kweli hamuwezi na MTASHINDWA tena kwa AIBU kubwa zaidi ya ile ya kwenye GE 2020!
 
Hivi JK angeunda baraza la mawaziri lenye waislamu 20 na wakiristo 3, usingeona hapo kuna tatizo?
 
Hivi JK angeunda baraza la mawaziri lenye waislamu 20 na wakiristo 3, usingeona hapo kuna tatizo?
Hayo maswali ni muendelezo wa hoja za kibaguzi na kizushi kama siyo za UCHOCHEZI. Serikali hii imeshavuka kwenye huo mtego wa kidini na kikanda na pia hizi ni sehemu ya vile VIHOJA NA VIOJA vya miaka yote. Tilivisika 2015 wakati wa Lowassa juu ya Ukatoloki na Uluteri. Kwa kweli hapa hakuna hoja yoyote bali ni kutaka kubabaishana humu JF baada ya KUSHINDWA KWA KISHINDO - sasa mnadakia issues badala ya kukoswa hoja zenye nguvu.
 
Nashauri tuelekeze nguvu zetu katika haya:

  1. Jinsi Ilani itakavyotafsiriwa katika mpango mkakati wa Taifa wa miaka mitano, 2020/25
  2. JInsi mpango mkakati wa Taifa wa miaka mitano, 2020/25, utakavyotafsiriwa kwenye mipango mikakati ya kisekta (wizara),
  3. Jinsi, mpango mkakati wa Taifa wawa miaka mitano, 2020/25, utakavyounganishwa na mipango mikakati ya LGAs.
  4. Vigezo vya kuwapata watekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa miaka mitano, 2020/25, pamoja na mipango mikakati ya LGAs.
  5. Ukusanyaji wa rasilimali kwa ajili ya kutekeleza mipango hii.

Karibu Sumbawanga!
Haya yote umeandika ila umeacha suala la bajeti kuakisi huo mpango mkakati?

Kma bado utekelezaji wa bajeti za maendeleo ni chini ya 50% kwa wizara crucial basi hayo mamipango hayana faida yeyote ile kwenye kufikia malengo kma taifa.

Ambacho ungeshauri ni kupunguza disparity katika vipaumbele haiwezekani tuweke nguvu kwenye eneo moja na kusahau kabisa sekta zingine.

Mfano suala la nishati unaona kuna mega project kma 3 kwa mkupuo ilihali kilimo cha umwagiliaji tu accessibility yake bado ipo chini ya 10%!! Ssa tutafika kweli kma nguvu zote zinaenda eneo moja kuliko mengine?

So mipango bila utekelezaji (Bajeti za maendeleo kuheshimiwa) inabakia tu hotuba za kufurahisha majukwaa.
 
Hivi waziri akiwa wa dini flani wewe mwananchi wa kawaida ambaye uko dini ya huyo waziri unanufaika nini katika maisha yako ya kila siku? hebu tuanzie hapo kupata hayo manufaa kwa waziri akiwa wa dini yako

Mimi kwa mtazamo wangu nafikiri ni ufinyu wa kufikiri sana kwa mtu anayetoa hoja ya namna hii
 
Hujui kwamba uwaziri ni nafasi ambayo ina marupurupu mengi sana?, faida hii ya kipato ina maana familia ya waziri itakuwa na nafuu sana kiuchumi , watoto wake watasoma shule nzuri zaidi, kupata elimu bora zaidi, kupata bima za afya bora zaidi, kuishi makazi bora zaidi, Na hii faida itawagusa hata ndugu za hao mawaziri. Sasa keki hii ya Taifa inapogawiwa kwa watu wa imani moja maana yake ni kuwa taasisi moja tu ya baraza la mawaziri tayari inaenda kuchangia katika tabaka kwa watu wa imani moja kunufaika zaidi na keki hii ya Taifa kuliko wenzao. Sasa hebu mfano huo uurejee kwenye teuzi nyingine nyingi zilizobaki kama vile wakurugenzi, manaibu waziri, ma DC, ma RC ma DAS, ma DED, Mabalozi wawe majority wa dini moja kama Magufuli alivyowateua utaona kuwa kipato kitokanacho na utumishi katika serikali kinakwenda kwa watu wa dini moja zaidi na hivyo kufanya watu hao waenjoy keki ya Taifa zaidi kuliko watu wa dini ya pili.
Faida za kiuchumi zitokanazo na nafasi hizo za utumishi zinakuwa transmitted kwa familia na matokeo yake watoto wao wakipata elimu bora, kuishi nyumba bora, afya bora kutokana na vipato vile basi cycle inajirudia tena huko mbeleni ndo wataendelea kupata fursa zaidi kuliko wenzao wanaowekwa pembeni katika teuzi hizi

Teuzi za udini zinafanya familia za wateuliwa ambao ni wa dini moja kunufaika na keki ya Taifa zaidi na hivyo kuziempower kuliko familia nyingi tu zilizowekwa pembeni, na hii effect ya itakuwa propagated kwa vizazi vingine vijavyo kwa sababu kuna watu wamejengewa msingi mzuri kiulaini na kwa kupendelewa huku wengine wakihustle tu na kutonufaika na fursa za utumishi wenye marupurupu mazuri, Ni dhahiri waliojengewa msingi mzuri wataendelea kuwa top ya hawa wanaobaguliwa japo na wao vigezo vya kukalia nafasi hizo wanavyo!
 
Mimi ni mwislam, ila alieleta mada hii ni Mjinga, unastahili tu kuelimishwa huenda ukaeleimika, ukaondokana na ujinga. Kwa hiyo ulitaka rais achague baraza la mawaziri lenye wakristo 50% na waislam 50%?. Kwa hiyo achague tu kukuridhisha wewe kwa idadi hiyo hata kama watendaji husika hawawezi kazi.......
Heshima yako mkuu
 
Manaibu waziri siyo sehemu ya Baraza la mawaziri na hawaingii kwenye vikao vya Baraza la mawaziri.
Moja: Balaza la Mawazili ni pamoja na manaibu, je manaibu wale hujawaona?!?

Mbili: Balaza la Mawazili ni pamoja na Makamu wa Raisi, Waziri Mkuu, Raisi wa Zanzibar, hawa nao ni makafiri?!? ewe uliyedini ya 'kweli'

Tatu: Nafasi za uongozi si zawadi, kwa dini, makabila, mikoa; hadi liwe ni swala la kufa na kupona, kwamba ni lazima dini, kabila, mkoa upate
 
Wanaomkea Magufuli mara kwa mara kwa udikteta wake haimaanishi nao ni madikteta kwa sababu wanausema udikteta wake!
Si kila usemacho basi nawe wakiunga mkono, ingekuwa hivyo basi watu wasingeisema dhambi na kuikemea
Udikteta unauchukulia poa wewe hilo nelo kalianzisha Lissu wachache kama wewe mmelindandia ,mtu kuitwa Dikteta usichukulie poa kisa kabana rushwa na katimua watushi hewa na kubana wapinzani ndio sifa pekee na Kagame na M7 waitwaje na hao ni baadhi.
 
Mimi ni mwislam, ila alieleta mada hii ni Mjinga, unastahili tu kuelimishwa huenda ukaeleimika, ukaondokana na ujinga. Kwa hiyo ulitaka rais achague baraza la mawaziri lenye wakristo 50% na waislam 50%?. Kwa hiyo achague tu kukuridhisha wewe kwa idadi hiyo hata kama watendaji husika hawawezi kazi.......
Mimi ni mkristo napingana na wewe ambaye umejiunga leo hii kutetea udini huu ulio wazi
Kwenye hili baraza Magufuli kawa mdini Sana kupendelea dini yetu sisi wakristu
Sio sahihi kusema katika hi nchi hakuna waislamu wenye uwezo wa kufanya kazi ya uwaziri
Mtoa posti yupo sahihi
Rais anatengeneza udini kwa uteuzi wa upendeleo ila wajinga wajinga na waimba mapambio kama wewe wanatetea upendeleo huu wa wazi
Hii nchi ni yetu sote waislamu hata Kama ni wachache wapo wenye uwezo wapewe nafasi hiyo ndiyo maana ya dhama ya social inclusion
 
Back
Top Bottom