denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
Wachana na hisia hit the target. Hujajibu hata point yangu moja unakimbia kimbia tu. Sikushangai ndio maana hata hoja za Mama Amon kule mwanzo hujajibu hata moja.Nahisi umerukia mada, ingekuwa ni vyema ukarudia kusoma mada husika, kisha ukasoma post uliyoiquote ambayo nilikuwa namjibu yule bibie uone muktadha mzima wa hiyo post.
Kama huoni tatizo kuwa na waislamu 3 ndani ya baraza la mawaziri la watu 23 huewezi kuelewa mada hii.
Na kama huoni tatizo watu kulaani teuzi zilizokaa kikanda au kikabila lakini watu haohao ambao hulaani mambo hayo hawaoni tatizo teuzi zilizokaa kidini na huwa wanafumba macho kama ni nothing pindi teuzi hizo zikifanywa, basi huwezi elewa jibu nililomjibu huyo uliyeniquote nikimjibu.
Ukitaka kuelewa vizuri geuza role, uwe na raisi Muislamu aunde baraza la mawaziri 23 lenye wakiristo 3 tu kisha lete mrejesho hapa hizo shutuma, lawama, miguno kutoka kila kona ya nchi!
Inawezekana vipi kwenye baraza la mawaziri lenye watu 23 liwe na waislamu 3 tu ina maana katika nchi hii hakuna waislamu wa kutosha wenye vigezo hadi hiyo tochi ya uteuzi iwe inamulikia watu wa imani moja tu?
Mimi nilitegemea muupige vita udini kwa vitendo, sasa mnashambulia watu wanaoukemea udini huo kwa kuonyesha kuwa kuna kila dalili za udini katika teuzi!
Bado niko pale pale siondoki, kuongelea haya mambo ya dini ni kupoteza muda bila sababu, binafsi sioni maana ya kuangalia watu kwa majina yao ili nianze kujiuliza kama huyu ni mwenzangu au sio.
Nimeshakwambia kule juu serikali ikifanya uhuni wake haiulizi dini ya mtu, unatakiwa umjue adui yako vizuri ili ujue namna ya kumshambulia, nyie naona miaka yote mnaruka ruka tu.
Kule Zanzibar Mwinyi katangaza Baraza lake la Mawaziri, asilimia kubwa ni waislamu, lakini sijamsikia mkristo yeyote au pagani akilalamikia hilo, HAKUNA.
Nyie wenyewe mko kimya kwenu mnaona ni sawa kwasababu kwa mtazamo wenu mnaona mmebebwa, miaka yote mnajiona dhaifu, mnaonewa, na hali hii ndio inawajengea tabia ya ubinafsi mnayotaka ienee kila mahali, na huu pia ni uthibitisho kwako wengine hayo mambo ya dini hatuna sababu ya kuyajadili, yanafupisha upeo wa fikra; if you think small you will remain small for life.
Halafu usinijibu issue yangu ya udini kwa kuchanganya na ukanda sijui ukabila, stick to the point, mimi najibu suala la udini pekee kwasababu huu ndio kama wimbo wenu wa taifa; wacha huo ukabila na ukanda wachangie wengine.
Mna tatizo la kisaikolojia. Siku nyingine mkija na hii hoja ya ajabu ajabu muwakumbuke na wapagani sababu nao hawana wakuwasemea.