KATIBA,SHERIA,KANUNI ZINASEMAJE KUHUSU BARAZA LA MAWAZIRI:?
Katiba yetu ibara ya 54 inasema Mawaziri watatokana na wabunge ila hakuna sifa za Udini,Ukanda, Jinsia, Hali ya Ulemavu, elimu nk
Kwa Mujibu wa Katiba ya Tanzania ya 1977 ibara ya 4(1) inasema kwamba " Shughuli zote za Mamlaka ya NCHI katika Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na Vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji,vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji HAKI na pia Vyombo viwili vyenye Mamlaka ya KUTUNGA sheria na kusimamia utekelezaji wa Umma.
ibara ya 4(2) imefafanua vyombuo viwili kuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na serikali ya Zanzibar, Vyombo viwili vya Itaoji haki ni Mahakama ya Jmahuri ya Muungano na Mahakama ya Zanziar na Vyombo viwili vya kutunga sheria ni Bunge la Muungano na Barazala la Wawakilishi.
ibara ya 4(3) inatajja mambo ya Muungano........
ibara ya 4(4) inasema kwamba "Kila chombo kitaundwa na kutekeleza majukumu yake kwa kufuata masharti mengine yaliyomo katika katiba hii.
Sasa kwa kuchangia huu mjadala wenye Hoja dhaifu 3 kuhusu baraza la Mawaziri kwamba
(i) Limejaa Wakristo wengi,
(ii) Kwamba hakuna Wazanzibar
(iii) Kwamba limejaa Wanaume na watu Ukanda wa Ziwa (Demographical variables)
Nilitegemea watu wanukuuu angalau Kifungu chochote cha Katiba/ sheria ambacho Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri atakuwa amekiuka au basi tuseme tunamhukumu kwa kutumia mazoea- mila/norms au maelekezo ya Chama kinachotawala.
HOJA kubwa inayotaka kujengwa ni ya UBAGUZI-DISCRIMINATION.
Katiba inasemaje?
Katiba yetu ibara ya 13(4-5) inapinga aina zote za ubaguzi bila kujali ni aina gani,iwe Dini,kabila,ukanda au Jinsia.
13(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa Kazi au shughuli yoyote ya madaraka ya Nchi
Ni nani anayesema kwamba amebaguliwa? UBAGUZI ndio HOJA kuu hapa; Kuna Mzanzibar anasema kwamba yeye ana haki ya kuwa Waziri ila amebaguliwa?
Kuna Mwanamke anayelalamika kuwa ameachwa kwa sababu ya Jinsia yake?
Kuna Mtu wa Mkoa wowote anayelalamika kwamba ameachwa kwa sababu ya Mahali alipozaliwa?
Ili kupata Majibu ya Maswali hayo, Katiba yetu ibara ya 35 (2) inasema kwamba Ofisi yeyote ya utumishi wa Umma itatatekelezwa kwa NIABA ya RAIS, yaani mwenye Ofisi nni Rais ila Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa MIKOA au Wilaya wanamsaidia tu, Rais huweka mtu ambaye akimwamgalia anajiona yeye,anaona mategemei yake.
Funga Kazi ni ibara ya 37 ambayo walioitunga waliona mbali,inasema kwamba " Rais halazimishwi kufuata ushauri wowote katika kufanya maamuzi yake---hata Bunge linaweza kushauri ila Rais habanwi wala halazimishwi kufuata huo ushauri, You knwo why? Ili kumpatia Rais uwanja mpana wa kutekeleza Katiba kwa minajili ya Haki,
Sasa basi, Sheria inasema kwamba " Yeyote anayeteuliwa na Rais is working for the PLEASURE of the President; yaani if the President is not pleased with you, He will dismiss you on that good moment/minute/second.
Kwa ufupi kabisa, hadi Juni 2021, kutakuwa na Wazanzibar zaidi ya 2 kwenye Baraza la Mawaziri, kutakuwa na Wanawake zaidi ya 5 kwenye Cabinet, na watu wa Mikoa/Kanda zingine zinazoona haijaingizwa kwa Cabinet; utauliza nimejuaje? Kila timu inakuwa na Wachezaji 11 uwanjani ila kunakuwa na reserve List in case of majeruhi, RED CARD, or whatever Mchezo lazima uendelee; hata Simba SC Juzi mliona akina KAGERE waliingia dakika ya 85
Pili, Ukiangalia Size ya Manaibu Mawaziri 23 ni idicator kwamba ni waiting list ya kuingia kwa cabinet ndani ya muda mfupi, Wazanzibar wapo 3, wanawake manaibu are 4,Mikoa na Kanda mbali mbali wapo wengi.
Tunachoweza kufanya kwa mujibu wa Katiba hii,ni kumwombea Rais na Washauri wake HEKIMA, BUSARA NA AFYA NJEMA ili Mungu mwenyewe awafunulie SIRI zake ambazo hata sisi hatuzijui. Ingekuwa Katiba yetu inasema Mawaziri LAZIMA wathibitishwe na BUNGE-WANANCHI, hapo wanaolalamika wangekuwa na HOJA za kutaka kuwe na mabadiliko, kwamba Bunge liwakatae baadhi ya Mawaiziri ili kuziba malalamiko yao, huo mlango haupo kabisa.
Labada Katiba yetu iseme kwamba kwenye Wizara 5 za Muungano, Kila Pande ya Muungano iwe na Uwakilishi ndani ya Baraza la Mawaziri na iseme kati ya Wizara atazounda Rais, 3 lazima 1/3 iwe ni Wanawake; hapo kutakuwa na Nguvu ya Kikatiba na itakuwa ni kufuata tu.
ILANI ya chama inasemaje?