Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Sijawahi kupiga kura kuchagua mwakilishi, wala shehia wala raisi wazanzibar. Hilo swali linawafaa wazanzibari zaidi

Sio lazima uwe Mzanzibari ili kujua wajumbe wa baraza la Mawaziri wa serikali ya Mapinduzi ili hali wewe ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania!!!
 
Kutokupiga kura Zanzibar hakukufanyi ushindwe kukemea ubaguzi wa kidini unaotokea kule, kwani ulimwengu unavyolalamikia mauaji ya Tigray kule Ethiopia wote wanapiga kura kule? wacha majibu yako ya kitapeli, hoja zako nyingi ni nyepesi sana.
 
Kutokupiga kura Zanzibar hakukufanyi ushindwe kukemea ubaguzi wa kidini unaotokea kule, kwani ulimwengu unavyolalamikia mauaji ya Tigray wote wanapiga kura kule? wacha majibu yako ya kitapeli, hoja zako nyingi ni nyepesi sana.
Anzisha mada ya udini Zanzibar tuchangie
 
Anzisha mada ya udini Zanzibar tuchangie
Kwa hili kubali tu huna hoja, issue ya Zanzibar ndio nimeileta ikufunge mdomo kabisa, siku nyingine mjifunze kuacha tabia ya kufikiria vitu vidogo mnajidumaza akili bila kujua.
 
.
Kwa hili kubali tu huna hoja, issue ya Zanzibar ndio nimeileta ikufunge mdomo kabisa, siku nyingine mjifunze kuacha tabia ya kufikiria vitu vidogo mnajidumaza akili bila kujua.
Pengine wewe unanufaika directly au indirectly na hii system ya ubaguzi unaowapa fursa wakiristo zaidi kuliko waislamu serikalini. Ukileta mambo ya SMZ kwenye ishu za SMT unaonekana unachanganya madafu na maembe na unaonekana hujui SMZ mipaka yake wapi na SMT mipaka yake ni ipi maana SMZ ni ya Wazanzibari, sisi Watanganyika haituhusu, wakati SMT ni ya wote Wazanzibar na Watanganyika kwa pamoja katika mambo yale ya muungano. Sasa kama una interest sana na Serikali ya Wazanzibar, ianzishie mada tu watu wajadili mimi sina Interest nayo kihivyo kwa maana sinufaiki nayo kwa chochote na silipi kodi huko na sina uwakilishi kwenye hiyo serikali.

Ninachojua ni kuwa Zanzibar ni semi-autonomous, wana mambo yao ya ndani ya nchi yao na mengine ya Muungano, Sasa kwa kuwa SMZ siyo jambo la muungano basi mambo yao hayanihusu kivile. Narudia tena, kama unakereka na SMZ anzisha mada hapa JF siyo lazima nianzishe mada unayoitaka wewe!
 
"Pengine" wacha kuongozwa na hisia kujibu hoja, hoja hujibiwa kwa hoja ukiweka na mifano kuthibitisha hoja yako.

Zanzibar kuwa semi autonomous or whatever hakukuzuii wewe kukemea maovu yanayotokea kule, braza kubali kutuliza kichwa ufundishwe usivyovijua, unaonekana mind yako ime-stuck, learn to think outside the box.

Thread sina muda wa kuanzisha kuzungumzia upuuzi wa udini kwangu hauna maana, simply sina muda wa kuangalia majina ya watu nianze kujiuliza huyu wa dini gani kama wewe ulivyo.
 
Naona unarudia yaleyale, unazunguuka unarudi palepale, unajibiwa unarudi palepale.

Ni hivi, Kukemea uovu hakuna monopoly, hata wewe unaweza kuanzisha mada ukakemea unayoyataka. Ila kwangu miye serikali ya SMZ ni ya Wazanzibari kwa ajili ya mambo yasiyo ya muungano. Sina interest sana kuizungumzia kama vile ambavyo sina interest kuzungumzia serikali ya Burundi, Nitaizungumzia tu iwapo kuna mambo mtambuka yanayoathiri maslahi endelevu ya Watanganyika nikiwemo miye.
Ila Serikali ya Muungano hicho ni cha wote lazima wote tuikabe mashati
 
Naunga mkono hoja, this is very objective
P
 
Nisingekuwa msomi nisingekufungua macho kwa hiyo kauli yangu, na si mtizamo wangu tu bali ni ukweli ulio sahihi. Fika ofisi za serikali siku ya Ijumaa kutafuta huduma, utasikia muhusika kaenda kuswali, yaani wakati wa kazi. Umeshawahi kujiuliza kwanini Uturuki na Misri wameendelea, umesoma hii?
 

 
Acha kudanganya, utakuwa wajua Misri na Uturuki kuliko mimi wewe? Misri Ijumaa hakuna kazi kabisa, na Uturuki wanasimamisha kazi wakati wa swala. Hilo halikuwafanya wasiendelee. Na hivi sasa ndiyo nchi yenye uchumi promising kuliko yeyote Ulaya. Wakati uchumi wa nchi za Ulaya ukiduwaa, wa Uturuki umekuwa kwa 4.5% ….pamoja na Kuswali kwao!
Wewe huna elimu ya kujua kitu gani kinakuza uchumi na gani kinazorotesha. Kwa chuki zako za asili, unaona ni kuswali!
 
Kuwa Waziri kunahitaji zaidi ya elimu ya stashahada; kunahitaji pia busara na hekima!!! Sidhani kama hawa wanyiramba wote wana attributes hizo!!!! JIWE anataka walio kondooo!!!
Hakuna ambaye si kondoo! Watumishi wa umma wote ni kondoo!

Nitajie kiongozi aliyepo CCM ambaye ana elimu na hizo busara ulizozitaja ambazo kimsingi mimi haziniingii akilini anayeweza kuwazidi hao Wanyiramba
 
Wewe utakuwa umekunywa kinywaji kikali. Mimi ninampinga mdini halafu unanipayukia?
why?
 
Hakuna ambaye si kondoo! Watumishi wa umma wote ni kondoo!

Nitajie kiongozi aliyepo CCM ambaye ana elimu na hizo busara ulizozitaja ambazo kimsingi mimi haziniingii akilini anayeweza kuwazidi hao Wanyiramba
Ntakutajia mawili ambao hata Jiwe anawagwaya na ndio maana amewatoa kwenye baraza lake bila sababu za msingi: Prof. Mbarawa na Japhet Hasunga!!!
 
Ntakutajia mawili ambao hata Jiwe anawagwaya na ndio maana amewatoa kwenye baraza lake bila sababu za msingi: Prof. Mbarawa na Japhet Hasunga!!!
Wana kipi cha kumtisha?
 
Tanzania kuna uhuru wa kuabudu kwann asiswali? Alafu ulilizungumzia ishu ya swala tano kwa waislamu...tambua ya kwamba swala ya alfajir kwa huyo mwislam swala hiyo huiswali kwake isitoshe swala ya saa 7 na saa 10 ienda akaiswalia akiwq kazini na tena haizidi hata dk 10,je hizo dk 10 zikushinde ww kumsubiri aliyekwenda kuswali kwa ajili ya mola wake?

Mara ngapi umechomeshwa mahindi na mtoto wa kike ikiwa umetumia muda mwingi kumsubili seuze hizo dk 10?,je ingelikuwa jumatano ndo siku kuabudu kwa wakristu wangeacha kwenda kusali? Serikali haina dini lkn watu wake wana dini.....nimeamini mtoa ana point katika hili...ninyi ndg zetu mmejaa hila na chuki dhidi ya waislam..

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Lowassa alimteuliwa waziri wa maji alihakikisha mikoa ya Shinyanga na Tabora inapata maji kutoka Ziwa Victoria wakati Wilaya zake za Monduli na Longido zilikuwa na uhaba wa kiwango cha juu cha maji. Hapo demografia kwenye uwaziri imefanyeje?
 
Nimesoma bandiko na kuelewa hoja. Lakini sikubaliani na hoja hiyo. Nitaifupisha na kuihakiki hapa chini, tena kwa ufupi kabisa. Mleta bandika amejenga hoja ifuatayo
Sisi waislamu watulivu wanyekekevu pia tupo kimya si kwamba hili hatulioni la hasha ' ila tunasubiri zamu yetu awamu ijayo tuone je nanyi wenzetu mtakuwa na subira kama yetu ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…