Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Hahahahaha

Wachaga wakilalalmila kutokuwepo kwenye Cabinet sawa

Wanawake wakilalamika uchache wao kwny Cabinet sawa

Waislam hairuhusiwi kulalamika… ngoja atokee Rais Mwislam halafu waislam wafike 40% usikie kelele za vigango na parokiani kama wakati wa Jakaya walipofika 36 % hadi Mtikila akaandika Waraka eti Jakaya ni Gaidi anaetaka kusilimisha Nchi akaugawa kwny Mkutano wa Jukwaa la Kikristo akasifiwa sana na Ma Baba Askof kwa 'Uzalendo' akiitwa Mfia Kristo…

Kwenye hoja ya udini hapo umekosea sana.
 
Heri yetu tusie na Dini,lakin nimejiuliza sana mkuu umeanzaje kukaa na kuanza kuwaza suala la udini kwenye teuzi me nadhan wewe ndo mbaguz nambari moja.
Me nadhan teuzi zinafanyika kutokana na uwezo na weledi wa mtu na si dini,mkoa au kabila.
Hata lingejaa waislamu wote as long wana deserve me sion shida na wote n watanzania wanafanya kaz kwa maslahi ya taifa hili.
Afu izi din sio zetu mkuu achana na ayo mambo ni ujinga mtupu
Hapo hakuna kuwaza ni uelewa
 
Uko sahihi, Ukitaka kuona wakiristo wakiungana kuteteana ni katika vitu kama hivi-Hapa watamtea Magufuli kwa nguvu zote kwa sababu analinda maslahi yao kwa vitendo na bila haya!

Hoja nzima maadamu nimetaja waislamu tu basi hawana haja ya kuona kuwa nimetetea wanawake na Wazanzibar

Nchi hii kuna udini wa kimyakimya wa ajabu sana, haya anayofanya Magufuli ni pembe tu imeanza kuchomoza ya kilichojificha chini
Unaona idea zako ni udini udini,

So mdini ni wewe.
 
% ya Wakristo Zanzibar ni ndogo kuliko ya Baniani huku bara, ushawahi kusikia mtu anajadili kwanini Baniani hawapati fursa za kiutumishi serikalini bara?
Baraza la mawaziri Zanzibar limekaa kimsikitimsikiti mbona hulalamiki?
 
Mleta mada umeisha 'fail'. Jiandae, kupokea barua ya 'discontinuation'!
 
Unazingua kweli Yani ,serikali yetu haina dini na tunaweza ongozwa na mtu yoyote Yule ilimradi havunji katiba, katika katiba hakuna sheria inayosema wanawake 50% na wanaume 50%, au dini flani 50% na nyingine 50%, dini ni nyingi hapa Tz katika baraza la mawaziri,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mada mfu kabisa! Unataka kuchonganisha kwa kutumia dini, uzanzibara. Uzuri ni kwamba wananchi wameshachoka na propaganda zenu, wao wanafanyiwa wanachotaka.. angalia vituo vya afya, Hosp, barabara, shule, n.k nk
Mada ni hai kabisa. Hata wafu tunawaheshimu na kuwakumbuka. Vituo vya afya havina watumishi wala dawa za kutosha; barabara nyingi zimejengwa kwa misaada ya mabeberu; Shule zimefurika watoto wanakaa chini na walimu hawatoshi; biashara zimekabwa koo na machinga pamoja na TRA; raia wamenyang'anywa uhuru wa kuchagua viongozi wanaowataka; raia wanawaogopa watawala kuliko Mungu; uvunjifu wa katiba umetamalaki; imani ya raia kupata haki yao kwa njia ya mahakama imeshuka; n.k, n.k.
 
Kwa Islam mtanielewa, siku moja kabla ya uchaguzi Muft alikuwa Chamwino akifungua "msikiti" halafu huyo huyo aje akemee huu utezi kweli? Kwa hili Islam hatuna.mtetezi. kama kuna ambaye hajanielewa asinikurupukie
 
Baraza la mawaziri Zanzibar limekaa kimsikitimsikiti mbona hulalamiki?
Sipigi kura kwenye serikali ya mapinduzi ya Zanzibar sina interest napo
Ila Wazanzibar wanapiga kura kwenye serikali ya JMT na nchi yao ni sehemu ya muungano wa nchi mbili zinazounda JMT
 
Huwa mnaungana pamoja na kuteteana kwenye maslahi ya watu wa dini yenu.

Nahisi ningeishia kutaja wanawake na wazanzibar peke yake mgeunga mkono hoja, ila kitendo cha kutaja kuhusu umuhimu wa kuwepo kwa notable inclusiveness ya waislamu kwenye baraza mmeona hii mada haijakaa sawa hahaha

Kemeeni teuzi za udini, nchi hii ni yetu sote

Lakini tutaendelea kulisema hili maana halijakaa sawa
Unamatatizo kichwani si hivi hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Islam mtanielewa, siku moja kabla ya uchaguzi Muft alikuwa Chamwino akifungua "msikiti" halafu huyo huyo aje akemee huu utezi kweli? Kwa hili Islam hatuna.mtetezi. kama kuna ambaye hajanielewa asinikurupukie
Mufti na Masheikh wasiojitambua wanatumiwa kwa kupewa maslahi machache ili wawe Manyapara dhidi ya waislamu wenzao. Ni sheikh Ponda aliyeona picha pana na kuamua kumkataa Jiwe, kwa sababu Jiwe ni mdini wa kutisha
 
Zanzibar ina wabunge wa Muungano ambao huingia ktk bunge la Muungano Dodoma.

Ajabu kutoka Bunge hilo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni wabunge wa Tanganyika tu ndiyo waliopewa nafasi kamili ya uWaziri ktk baraza / cabineti ya mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Huku ni kuudhoofisha Mungano kwa kuwa nafasi zote 23 za uwaziri kamili zimekwenda kwa wabunge wa Tanganyika wakati kuna wizara mahususi ktk serikali ya Muungano zinazofanya kazi kwa niaba ya Muungano kama wizara ya mambo ya nje, wizara ya mambo ya ndani , wizara ya ulinzi na wizara ya fedha ambapo angalau hata waziri kamili mmoja angetoka Zanzibar kuonesha Muungano wetu au hata mawaziri 3 wangetoka Zanzibar na mmoja Tanganyika kushika wizara hizo 4 za Muungano .
 
Kwani wameteuliwa kwenda kusoma Quran au biblia au kwenda kufanya kazi? Tufike mahali mtu ateuliwe kwa kufuata uwezo wake wa kutenda kazi na sio dini wala rangi yake wala jinsia yake. Ni wazi mtoa maada ilitakiwa ushitakiwe kwa kuonyesha ubaguzi hadharani kabisa. Unaonyesha ubaguzi wa kidini hadharani hao watu wameteuliwa wakafanye kazi na sio kwenda kuhubiri.
 
Back
Top Bottom