Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Rais anateua baraza la Mawaziri kwa kushauriana na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Hao wote ni Waislamu kwani wao hawakuliona hilo?

Ishu ya wanaweke wacha wakae nyumbani watulee.

Wazanzibar na wenyewe wana nchi yao. Anyway Mbarawa ameniumiza moyo kukosekana kwenye baraza la mawaziri.

Anyway today is Sunday take your Bible and go to your nearest church.
Nani ashauriwe na nani?
We ni mgeni hapa nchini?
 
Rais angekuwa ni muislamu na akateua waislamu wakutosha (kama nusu tu ya baraza zima), leo jumapili makanisani zingesomwa nyaraka za maaskofu kuipinga serikali, mahubiri na maombi yangekuwa ni kuipinga serikali, wakristo wangeambiwa wafunge siku kadhaa dhidi ya uislamu kushamiri hapa Tz nk.

Viongozi wa kikristo nawajua vizuri.
Siyo kweli. mtoa mada ana hoja lakini wewe umeandika utopolo.
 
mwandishi mtazamo wako ni HASI, mimi nadhani ungechamnua vigezo vya elimu na uzoefu wa kazi badala ya DINI.

HAO WAISLAM uliosema ndio akina BABU TALE, KIGWANGALA na Nanii, kweli wewe unaytaka kutupeekajehanamu
 
Hebu tuangazie macho kwa karibu zaidi, tukiwaacha Kitila Mkumbo, Mwigulu Nchemba na Profesa Majalala, Kuna Mawaziri Wengine wasio Wakatoliki katika hilo Baraza?
 
Kwani ni lazima kuteua waziri toka huko wapi katiba imesema hivyo mbona wao hawateui toka bara!

Angekuwa anafuata katiba hapo sawa. Lakini sio kwa anachokifanya. Ni hivi, huyu jamaa hakustahili kuwa rais maana hajengi utaifa, bali anajali serikali.
 
Pamoja na hoja hii kuonekana ina ukakasi wa kuwagawa wananchi kwa Mtazamo wa Imani Zao jambo ambalo sio zuri lakini kama isemwavyo kwenye Vitabu Vitakatifu Mke wa Mfalme hapaswi kuhisiwa kuwa sio muadilifu vivyo hivyo Watawala hawapaswi kuweka mazingira ya kuhisiwa kuwa Wabaguzi/ Wapendelea Upande Fulani kwa Misingi Fulani iwe ya Kikabila, Kikanda, Imani au Undugu/ Urafiki.
 
Unazingua kweli Yani ,serikali yetu haina dini na tunaweza ongozwa na mtu yoyote Yule ilimradi havunji katiba, katika katiba hakuna sheria inayosema wanawake 50% na wanaume 50%, au dini flani 50% na nyingine 50%, dini ni nyingi hapa Tz katika baraza la mawaziri,


Sent using Jamii Forums mobile app

Ila enzi za kikwete ilokua na dini!?[emoji3]
 
Baada ya kukosa uteuzi umekuja na pumba zako,umepoteza muda wako kuandika upuuzi na kuhubiri udini .
Nchi haiendeshwi kwa misingi ya kidini ni uwezo na uchapaji kazi ndio utakao kubeba.😂😂😂😂
 
Kwani tunahitaji Baraza la Mawaziri la kwenda Misikitini au Makanisani?
Hata kama walioteuliwa watafanya vizuri vp haifai kuwabagua wenzako, kutambua hisia ni kitu muhimu sana katka jamii, binafsi sijafurahishwa na hili baraza kwa sababu hiyo.
 
Hili jambo watu tulilitarajia baada ya kuona orodha ya watia nia hasa upande wa ccm, jimbo lina watia nia kama zaidi ya 50 lkn waislam ni 3 tu. Je ni rahisi hao watatu kushinda hao wengine 47? labda tuseme hapa hekima na busara ziliitajika zaidi.
 
Uliwahi kumuona mbunge wa Tanzania bara anaingia kwenye baraza la wawakilishi Zanzibar ?
Swali uliouliza na la kipuuzi sana na linaadhirisha kotoelewa mfumo wa utawala wa nchi yako.
b) Hili ni baraza la Tanganyika, Yawezekana vipi usiwe na baraza lenye waziri kamili hata mmoja Mzanzibar?

Naomba nifahamishwe pia kwenye Baraza la Mawaziri Zanzibar kuna mtanganyika alishawahi kuteuliwa nafasi ya uwaziri[emoji23]
 
Sio kweli
Tukianza kuangalia vigezo hivyo hakika hakutakuwa na teuzi.Maana ukimaliza ya udini na uzanzibari utakuja ya ukabila kusema baraza zima ni wachaga,wasukuma n.k ukimaliza hapo utakuja na baraza zima halina waziri kijana,mzee n.k kwa kifupi vigezo vyote vikizingatiwa ni mwanzo wa kupata watendaji wabovu na kigezo kikuu na cha muhimu kati ya vyote ni utendaji uliotukuka! Tukianza kuangalia vigezo vingine ni mwanzo wa kupata viongozi wasio na tija kwa taifa kisa tu kuzingatia swala la dini,uzanzibari,wanawake,umri n.k jambo ambalo litarudisha juhudi za taifa nyuma.
 
Wakati wa KIKWETE unakumbuka mawaziri waislam walikuwa wangapi???,, achana na hilo, serikali kuu na wakuu wa mashirika ya Umma. Nakumbuka kwa mfano, Rais Kikwete alikuwa Muislam,,makamu wa Rais Muislam..jaji mkuu muislam,ukienda kwenye mashirika ya umma kama Nssf walikuwa waislam..ATC, mkaguzi mkuu hesabu za serikali.......ACHA UDINI
 
Mada mfu kabisa! Unataka kuchonganisha kwa kutumia dini, uzanzibara. Uzuri ni kwamba wananchi wameshachoka na propaganda zenu, wao wanafanyiwa wanachotaka.. angalia vituo vya afya, Hosp, barabara, shule, n.k nk
Sema wewe umechoka usisemee wananchi wote.
 
Wewe una chuki ya muda mrefu dhidi ya Rais Magufuli, suala la baraza la mawaziri umelitumia kama nyenzo ya kumshambulia.
Mbona unazungumzia mawaziri tu lakini manaibu mawaziri huzungumzii? Au hivyo sio vyeo? Mbona huhoji kuhusu dini zingine kama budha, hindu, sikh na wapagani? Kwani nchi hii ina dini mbili tu? Baraza la mawaziri Zanzibar lina mkristo hata mmoja? Mbona huko huchambui?

Unadai wanawake ni wachache umeangalia na manaibu mawaziri? Baraza la mawaziri sio chombo cha uwakilishi bali ni chombo cha utendaji hivyo kinachoangaliwa ni ufanisi katika kutekeleza ilani na utendaji.

Hata kama wangeteuliwa watu wa hiyo dini na jinsia unayotaka bado mwingine angelalamika kuwa nchi ina makabila 120 hivyo theluthi mbili za makabila hawamo hivyo haiakisi demography ya nchi. Haya mambo yakiendekezwa ndiyo yanasababisha mlipa kodi kutwishwa mzigo mkubwa wa kodi ili kugharimia baraza kubwa la mawaziri ambalo limesheheni makabila yote. Rejea baraza la Sudani kusini kwa mfano, nchi ndogo masikini inakuwa na baraza kubwa sababu ya kuendekeza upuuzi wa ukabila, dini au jinsia.

Badala ya kukosoa tu hebu eleza mazuri ya JPM au kwa uelewa wako hajawahi kufanya zuri hata moja?
 
Kwani baraza la mawaziri la H. Mwinyi lina wakristo wangapi? Acheni ujinga huu wa udini.
Mbona kuna mtu alijaza waislamu kwenye taasisi nyeti?
 
Back
Top Bottom