Pre GE2025 Baraza Kuu la CHADEMA laidhinisha Wagombea wa Juu wa Uongozi wa Chama hicho, kwahiyo Kipute kiko pale pale

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lakini wajumbe wamekatwa kutokana na misimamo yao! Mbowe ni mtu mbaya zaidi ya CCM
Mbowe angekuwa Mbaya hao Tundu Lissu na Heche wasingeteuliwa pia. Tunaomba muweke wazi majina yote ya Walioomba huo ujumbe na mtuainishie kila mmoja alikuwa akimuunga Mkono nani ili tuzungumze kwa data na si ushabiki.
 
Kwahiyo siku zote walikuwa hawajawapitisha kwanini..?
 
Chonde chonde wana CHADEMA. Ushauri wa bure kwa Viongozi wakuu CHADEMA. Ili kuto kigawa chama na kukifanya kionekana dhaifu mbele ya Watz na dunia nzima. Nashauri Mhe. MBOWE na Mhe. LISSU wakubaliane kuachiana nafasi ya Mwenyekiti Taifa. Mbowe aruhusiwe kuendelea na Uenyekiti lakn iwe ni awamu yake ya mwisho. Lissu aachiwe kuendelea na Umakamu Mwenyekiti kwa sharti kwamba atakuwa MGOMBEA WA URAISI KWA TIKETI YA CHADEMA MWAKA HUU WA 2025.
 
Kwakuwa CCM ni chama cha Rwanda ?
Watanzania bhana..

Wagombea wangekuwa 10,000 wangepitishaa wote ili kujitofautisha na CCM? Hilo tu?
Yes, hata wangekuwa laki moja, bado wote wana haki ya kugombea ikiwa wana sifa stahiki.

Njia pekee ya kuchuja uwingi wa wagombea inabakia kwa wapiga kura pekee. Wewe ni nani mpaka uingilie haki za wapiga kura?
 
Kwa kuwa Chadema ipo kwa mujibu wa Sheria.
Vyombo vya ulinzi TZ, vipo macho katika uchaguzi huo.
Atakayeanzisha vurugu atajuta kuzaliwa kesho hiyo.
Kwa serikali hii ya CCM? Elewa tu kinachoendelea hapo vyombo vya Ulinzi na Usalama viko taýari kuchochea vurugu ili kuwafurahisha CCM wanao subiri kwa hamu anguko la CHADEMA!!!
 
Yes, hata wangekuwa laki moja, bado wote wana haki ya kugombea ikiwa wana sifa stahiki.

Njia pekee ya kuchuja uwingi wa wagombea inabakia kwa wapiga kura pekee. Wewe ni nani mpaka uingilie haki za wapiga kura?

Hicho kibri tunakifyekelea mbali.. Nendeni DP ya Mtikila
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…