Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Status
Not open for further replies.
MAHAKAMA ZA ARDHI Za Kibiashara Kila Mwananchi Ananufaika Nazo. Mfano, Ikitokea Mtu Kaamua Kujenga Barabarani Na Kuziba Njia Ambayo Inapitwa Na Huyo Mpangaji Atapitia Wapi? Haya Mahakama Ya Biashara Ikitokea Mfanyabiashara Kauziwa Vitu Feki Nae Akaja Kuwauzia Wananchi Bidhaa Feki Unazani Wananchi Wasio Wafanya Biashara Hawataathirika? Ndo Msingi Wa Kuwepo Mahakama Hizo.LAKINI MAHAKAMA YA KADHI NI IMANI YENU YA DINI NA INAMANUFAA KWENU Tofauti Kabisa Na Mahakama Ya Ardhi Ambayo Inafaida Kwangu Hata Ikija Tokea Mtu Kajenga Eneo La Wazi Naweza Mfungulia Kesi Bila Kujali Dini Yake,pia Ikitokea Nimeuziwa Kiwanja Hewa Naweza Kwenda Huko,nikiuziwa Bidhaa Feki Naweza Enda Mahakama Ya Biashara Tofauti Na MAHAKAMA YA KADHI KWETU SISI WAKRISTO ASILANI ABADANI HAITOTOKEA IWE NA FAIDA KWANGU HATA SIKU MOJA.Ndiyo Maana Tunawaambia Anzisheni Kwa Pesa Zenu.
 
Inashangaza kuona mada ikiwa jambo la waislam/uislam basi kila mtu atakuwa mchangiaji hata kama uelewa juu ya hilo jambo. Ningeomba ndugu zangu wasio waislam waifaham kwanza mahakama ya kadhi na shughuli, nchi vipi zinafuata huo mfumo na athar zipi wamezipata kwa kuwa na mahakama ya kadhi. Lkn kinachoonekana hapa ni kejeli na matusi bila kufanya mjadala kwa hoja.
 
 
Swala sio kuifahamu ama kutoifahamu mahakama ya kadhi, mjadala ni Kodi ya mkristo(kafiri) kugharamia ibada ya Imani nyingine.
 
Swala sio kuifahamu ama kutoifahamu mahakama ya kadhi, mjadala ni Kodi ya mkristo(kafiri) kugharamia ibada ya Imani nyingine.

He! Kumbe waislamu hawalipagi kodi! Wakamatwe mara moja!
 
Swala sio kuifahamu ama kutoifahamu mahakama ya kadhi, mjadala ni Kodi ya mkristo(kafiri) kugharamia ibada ya Imani nyingine.

Mbona kodi za waislam zinagharamia uezeshwaji wa MOU.
Mbona kodi ya muislam imeliwa na ASKOFU KILAINI kupitia MKOMBOZI BANK ,banki ya kifisadi inayomilikiwa RC.
 
ndugu zangu waislam, hili suala la mahakama ya kadhi kuwa sehem ya chombo cha dola ili hali kinalenga kuhudumia kundi flan tu yaan waislam, siyo halali hata kidogo kuendeshwa kwa gharama ya serikali ili hali walipa kodi ni watanzania wote( wakristo na waislam na wapagani). siyo halali kuendeshwa na serikali. mkitaka hiyo mahakama muiendeshe wenyewe kwa ghaarama zenu. wakristo hatuwezi kukubali fedha zetu ziende kuendesha mahakama ya kadhi badala ya kuboresha huduma za kijamii yaan shule, afya na maji na miundombinnu. ni hayo tu!
 
Hawa waislam mbona mnasahau mapema hivyo,mnakumbuka wakati wakristo wanataka kufungua ubalozi wa vatican nchini tena kwa gharama zao wavatican mlivyoweka ngumu na kuja juu??????Leo hii mnataka kadhi tena kwa kodi za wote,haikubaliki hata kidogo.Anisheni utaratibu wa kuchanga fedha zenu ikahudumie mahakama hizi,mnataka kujitengenezea ajira kiulaini namna hiyo,no way.Mahakama ya kadhi kwa tz mtasubiri sana.
 
sioni tatizo juu ya kodi,kama kodi zinatumika kwa mtanzania kwa nin tuanze kuangalia ni mtanzania wa itikadi gani? kama kweli mngekuwa na hasira na kodi msingekaa kimya viongoz wanapoiba mihela yetu, lakin naona hapa tatizo ni uislam.isitoshe hyo mahakama itasaidia kupunguza mlundikano wa kesi kwenye mahakama za kawaida hivyo mkristo nae atafaidia kwa kesi yake kusikilizwa haraka kwenye mahakama za serikali kwan kesi za mirath na ndoa ni nyingi mno! pamoja na mambo yoote 2kumbuke sisi ni watanzania!
 
sio kila kitu kuiga ya mwenzio,nchi nyingine kuna ndoa za jinsia moja na ni halali,mbona hatujaiga?we do what is in our best interest,..wakristo na wapagani wengi wanapinga hii mahakama kuingizwa serikalini,tusilazimishe tukaja kuleta vurugu huko mbeleni...mbona kuupinga ushoga tumekubaliana kwa pamoja!kama taifa,hakuna consesus kwenye mahakama ya kadhi kuanzia mitaani hadi bungeni,surprisingly hadi ikulu ilipinga hili swala.
 
stop generalization,unaposema nyingi mno maana yake nini?tutajie kesi ngapi ziko mahakamani..
 
SWALI KWA MOHAMED SAID & JAMIIFORUMS MEMBERS:

Hivi BAKWATA si ni NGO kama NGO zingine?

Lini BAKWATA ilipewa mandate ya kuwakilisha waislam wote Tanzania?

Lini Waislam wa Tanzania waliwapa mandate BAKWATA iwawakilishe?

What if Musilam hataki kuwafuata hawa BAKWATA je serikali itamshitaki au?
 

Vurugu ya bhana! Vurugu itokee Tanzania pekee eti kwa sababu ya Mahakama ya Kadhi? Itokee Tanzania pekee kwa uwepo wa Mahakama ya Kadhi ila Kenya, Uganda na kwingineko isitokee? Whats so special with Tanzania! Hii ni sawa na Propaganda zingine ambazo hazina mashiko kuwa mfumo wa vyama vingi ni vita, mara ukichagua wapinzan ni vita! Uongo mtupu!
 

Mimi mkristo historia ya Dini yako hainihusu,hapa tunaangalia uanzishwaji wake utanufaisha watu wote au la.Mbona mlipinga uanzishwaji wa ubalozi wa vatican tanzania?????Nani awakubalie,someni ramani,hata JK mwenyewe kawachinjia baharini.
 
Naomba aya kwenye Quran inayosema kuwa Mahakama za Kadhi LAZIMA ziingizwe kwenye Katiba au zigharamiwe na Serikali!


Kwani kuna aya katika dini yeyote ulimwenguni inayofahamisha katika katiba ya nchi kuwe na kipengele cha Sanaa pamoja na uigizaji?? Kwani mulipotunga katiba yenu mulizingatia kila kilichotajwa katika Quran kwa mujibu wa aya zilivyokuja?

Mbona Quran inafafanua haki za kila mwanamme na mwanamke kwa misingi yake maalum nyinyi mukaweka 50-50 kama kweli mulizingatia Quran?

Hapa Waislamu tumedai hii Mahkama ya Kadhi lengo tupate chombo kinachotambulika kikatiba na katika dola ya nchi ili kiweze kuzisimamia hizi haki ambazo tayari zimetajwa na kufafanuliwa katika Quran. Na wasimamizi wa chombo hiki lazima wawe ni waislamu ambao wamebobea katika kuchambua, kusimamia na kutoa haki kwa Waislamu.

Hata kama munakosa elimu ya utambuzi wa haya mambo lakini rudi katika nadharia ya kawaida utaweza kujifunza na kujuwa hasa Waislamu hapa wanachotaka ni kitu gani.
 
Ni sehemu ya ibada za kiislam wapewe ni haki yao vinginevyo damu itamwagika
 
Umenikuna sana kwa pointi yako mkuu naomba unithibitishie kama kweli katiba ya zanzibar haitaji mahakama ya kadhi ili niseme neno tafadhali karibu mkuu
Ni kweli kabisa mkuu, kama katiba ingesema ingekuwa lahisi kunukuu ibara ya.... Kilichofanyika mambo ya mahakama ya kadhi yameandikiwa sheria. Viongozi wengi wameshindwa kuwa wawazi kwamba jambo la kiimani kuliingiza kwenye Katiba ni hatari kuliko hatari yenyewe. Na hata hao viongozi wa DINI wanaotetea wanajipambanua kuwa ni watu wa binafsi na wenye fikra DUNI. kama ambavyo Plato alianzisha elimu ya chuo kikuu kuwajengea uwezo watu wa kufikiri kwa mantiki, tunapaswa kufikiri kwa mantiki ktk suala hili.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…