Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Status
Not open for further replies.

Hapo hakuna dilemma, hapo tunawaonesha namna ya kudai haki zetu Kiusalama kabisa.

Na Waislam waliwengi tukiamua kura ya hapana basi ujuwe katiba pendekezwa haipiti.

Na sasa hatutaki ahadi, na wakati wa kura za Urais na ubunge, uzi ni hohuo. Mpaka watu watie akili.

Baraza Kuu tuko pamoja, naunga mkono hoja.
 
Hapa siitetei CCM. Uislam kwanza kuliko kingine chochote.
Kwa mantiki hiyo unaungana na waisilamu kupinga mapendekezo yaliletwa na CCM kuanzia kwenye katiba hadi sheria hii? Unapaswa kunyang'anywa kadi ya 'chama' wewe!
 
Duuh kazi kweli kweli, naomba kuuliza "mbona Zanzibar 90% ni waislamu Lakini mahakama ya kadhi haipo kwenye Katiba.
 
Sijui hapa akina Faiza watakuwa upande gani?

Msome tu humu utamuelewa.

Kama Nyerere alikuwa kwanza Kanisa halafu ndiyo nchi basi FaizaFoxy kwanza Uislam kabla ya chochote kile.
 
Last edited by a moderator:
Kwahi kura yako ni HAPANA kwa katiba mpya?

Ikiwa ndiyo msimamo wa Waislam, basi naam, kura yangu itakuwa ni hapana, siwezi kwenda kinyume na Waislam wenzangu hata siku moja, kinachotuunganisha Waislam ni kamba ya Mwenyeezi Mungu.

Hiyo katiba siioni ina maana gani kama haitambui kuwa kuna Waislam na wana haki zao za msingi.
 
Kwa mantiki hiyo unaungana na waisilamu kupinga mapendekezo yaliletwa na CCM kuanzia kwenye katiba hadi sheria hii? Unapaswa kunyang'anywa kadi ya 'chama' wewe!

CCM ni watu na watu ndiyo sisi.
 
Kichwa cha habari 'Baraza Kuu la Waislamu' latoa tamko. Habari yenyewe 'Jumiya na Taasisi za Kiislamu (T)'. Kwa uelewa wangu hivi ni vyombo viwili tofauti. Kisheria Baraza Kuu la Waislam Tanzania BAKWATA ndicho chombo kinachotambulika kisheria na chenye mamlaka ya kuwakilisha waislam (kutokana na serikali). Nadhani kichwa cha habari kilikuwa na lengo ya kupata attention ya wasomaji. Tuendelee kusubiri kama BAKWATA hawatakanusha hili.
 
Hilo sidhani kama litafanikiwa coz madhehebu mengine nayo yatahitaji mahakama yao

Hapa hayaongelewi madhehebu hapa panaongelewa msimamo wa Waislam kutaka haki yao ya msingi.

Hutupi mahakama ya kadhi hatukupi kura. Chaguwa wewe sasa.
 

Mimi si muislamu na sitaki kuamini kua uanzishaji wa mahakama ya kadhi hapa Tanganyika utakua na athari kwa taifa.Mi nadhani ianzishwe tu mbona nchi nyingine wana mfumo huo na hakuna shida?.Mwaka huu msikubali ahadi.
 
Hapa siitetei CCM. Uislam kwanza kuliko kingine chochote.

Hivi wale waliokwenda kuhiji si waliipigia kura katiba pendekezwa kwa njia ya email, inamaama hawakujua kama mahakama ya kadhi haikuwepo! ama kweli ccm kiboko ya waislam!
 
Isijekuwa tu hawa baraza kuu la Waislaam wanatumiwa na watu fulani fulani, maana sijawahi kuona jema lao hawa.

Al Alama Mohamed Said, Ritz, THE BIG SHOW, na Waislam wengine humu jF, hebu tuwekane wazi kidogo, tuungane nao hawa au kuna kamchezo hapa tusikokajuwa?

Maana hii taasisi ilianzishwa na Nyerere hii ambae si Muislam na hakuwa na jema kwa Waislam.
 
Last edited by a moderator:
Mna maana wenzangu toka tuaidiwe hamjajua tunadanganywa mimi nishastuka mda murefu na kurudisha kakadi kao
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…