Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Status
Not open for further replies.
Sasa hivi nadhani BAKWATA wamejifungia wanaandaa Tamko kuwapinga hawa jumuiya za kiislam na wataunga mkono hoja,Mapendekezo au mswada unaopendekezwa... Si Mufti amepewa mamlaka ya kuteua hao Makadhi..!!!
THE BIG SHOW FaizaFoxy poleni kwa Dilemma hii!!

BACK TANGANYIKA



Utamuona yule kibaraka wa CCM anaejiita shehe mkuu wa mkoa wa dar akipinga hili tamko huku povu likimtoka
 
Last edited by a moderator:
bado tamko la makafiri! kazi ipo!
kura ya hapana ya katiba...tulishavurugwa kitambo..iwe ndio au hapana bado watawala wameshinda.
Muhimu tujipange na watakao kuja...maana ndio wataweza kuokoa nchi na tukawa na dira!
kwangu kuhaidiwa/kupewa mahakama ya kadhi ili utoe kura ya ndio, HIYO NI RUSHWA.
 
kumbe na mufti hapatikani kisheria maana ofisi yake haiundwi kisheria.
hapo ndo utata unapoanza!
halafu nilishangaa kuona watu wanaingiza interest za dini ili hali awali ilifafanuliwa taifa kutokuwa na dini!
na tena muungano hautavunjwa tujadili namna ya kuboresha!
ujinga ni maradhi-nyerere
 
wapi alama yoyote kuenyesha kuwa waraka/tamko hili limetoka sehemu tajwa? japo jina na signature ya mwandishi? au japo kijimuhuli cha taasisi tajwa? hofu yangu isije ikawa nimeandika mimi na kuwasingizia waislamu wenzangu. nawasilisha.
 
Ndugu zangu waislamu ulazima wa serikali kugaramia hiyo mahakama yenu unatoka wapi ili hali mnajua haitahudumia kundi Fulani la walipako kodi acheni ubinafisi bana
 
Isijekuwa tu hawa baraza kuu la Waislaam wanatumiwa na watu fulani fulani, maana sijawahi kuona jema lao hawa.

Al Alama Mohamed Said, Ritz, THE BIG SHOW, na Waislam wengine humu jF, hebu tuwekane wazi kidogo, tuungane nao hawa au kuna kamchezo hapa tusikokajuwa?

Maana hii taasisi ilianzishwa na Nyerere hii ambae si Muislam na hakuwa na jema kwa Waislam.

Kuna hoja inakupita kushoto hapa bibie..,!!!

Nikwamba Tamko hili limetolewa na JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM (T)

Kimsingi vyombo hivi ni tofauti ingawaje vyote ni vya Kiislam. Nadhani umepotoshwa na kichwa cha habari cha kaka Mohamed Said tuombe mods wabadirishe hicho kichwa cha habari. Lakini ni lini mtaacha kumlalamikia Nyerere juu ya uanzishwaji wa hilo BAKWATA?

Mbona basi ninyi mliohai hamchukui hatua zozote kuliondoa? Au mnataka Nyerere afufuke kutoka katika wafu aje awaondolee hilo Zimwi? Na mbona basi bado mwahitaji serikali ileile ambayo ilikuwa ikiongozwa na Nyerere wakati huo na ikaanzisha hii BAKWATA, mnataka sasa iwaanzishie Mahakama ya Kadhi? Mbona mi sielewi kitu hapa?? Kipi ni kipi bibie hebu funguka kidogo.

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Kwa hili la kupinga mahakama ya kadhi CCm naaunga mkono 100%. Nchi hii haina dini, ole yake serkali itakoyothubutu kukubaliana na jambo hili gumu linalovunja umoja wa nchi yetu.
 
msitutanie nyie iyo kitu haiwezi kua apa Tz ata Rais angekua sh simba
 
attachment.php

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM (T)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

17 Mfungo Sita 1436
9 Januari 2015

TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM TANZANIA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI KWA WATANZANIA WOTE, JUU YA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI NA. 02, WA MWAKA 2014, HUSUSAN KUHUSU SEHEMU YA MAREKEBISHO KWENYE SHERIA YA TAMKO LA SHERIA ZA KIISLAM

Awali ya yote tunapenda kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu, Ardhi na vilivyomo, na Rehma na Amani zimfikie Kiongozi wa Ummah Mtume Muhammad (SAW).

Ndugu wanahabari,
Assalam Alaykum Warahamatul llah Wabarakatuh.

Tumekuiteni hapa kwa lengo la kueleza kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 02, wa mwaka 2014 haswa kuhusu marekebisho kwenye sheria ya tamko la Sheria za Kiislamu. Tunafahamu kuwa kuanzia tarehe 13 hadi 23 Mwezi huu wadau mbalimbali wataitwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo yao, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania tukiwa sehemu ya wadau muhimu tunapenda kuwaeleza kuwa mtiririko wa mchakato wa marekebisho ya sheria kwa mujibu wa muswada huu unaokusudia kutambua Mahakama za Kadhi Tanzania bara una kasoro kubwa na kwa dhati unaonesha wazi kuwa serikali haina nia ya kweli ya kuunda Mahakama ya Kadhi yenye hadhi kamili ya kimahakama na uthabiti wa kuwepo kwake na kuwa muswada huu ni hadaa nyingine ya serikali hii ya CCM kwa Waislamu kwa sababu zifuatazo:-

1. Malalamiko juu ya Mahitaji ya Mahakama ya Kadhi yana historia ya kupindishwapindishwa na serikali hii inayoundwa na CCM. Kwa mfano katika Ilani ya CCM mwaka 2005 iliahidi kuanzisha Mahakama ya Kadhi lakini kwa ghilba nyingi CCM haikutekeleza ahadi hiyo baada ya kuingia madarakani kwa hoja kuwa hili ni jambo la Kikatiba.

Hata hivyo mchakato wa Katiba mpya ulipokuja asilimia kubwa ya maoni ya Waislamu yalihitaji Mahakama ya Kadhi kuingizwa ndani ya Katiba, mapendekezo hayo yalikataliwa na Tume ya Jaji Warioba kwa hoja kuwa katiba inayotengenezwa ni ya Muungano na suala la Mahakama ya Kadhi si la Muungano hivyo lisubiri wakati wa kuandaa Katiba ya Tanganyika. Waislamu tukavumilia kuisubiri Katiba ya Tanganyika.

Lakini Bunge Maalum la Katiba likaikataa Katiba ya Warioba na kutunga Katiba Mpya Pendekezwa yenye mambo yote ya Muungano na yasiyo ya Muungano bila ya kuingiza Mahakama ya Kadhi kama ilivyoahidiwa na Tume ya Jaji Warioba. Bunge la Katiba lililokuwa linaundwa na wajumbe wengi wa CCM hawakuona umuhimu wa kutimiza ahadi yao ya kuweka Mahakama ya Kadhi katika katiba pendekezwa na kwa makusudi Mahakama ya Kadhi ikakataliwa na wajumbe wengi wa CCM walishangilia jambo hili ili hali wanajua dhahiri kuwa Waislamu hawakufurahishwa na uamuzi wao na pia kukiuka Ilani yao na ahadi kwa Waislamu.

Muswada huu ni sehemu nyingine ya hadaa kwa Waislamu kwani badala ya sheria kuanzisha Mahakama ya Kadhi kama ilivyo kawaida ya uanzishwaji wa mahakama zote duniani muswada huu umeliacha jukumu hilo kwa taasisi binafsi ili hali Mahakama ya Kadhi kama zilivyo mahakama zingine ni sehemu ya chombo cha dola katika mfumo wa Mahakama yaani “the Judiciary”, hili limefanywa makusudi kutokana na kutokuwepo na nia ya dhati ya Serikali ya CCM kuanzisha na kuona Tanzania Bara kunakuwa na Mahakama ya Kadhi madhubuti na ya ukweli.

2. MUSWADA umempa mamlaka “Mufti” kuteua makadhi na kutengeneza kanuni za Uendeshaji wa Mahakama ya Kadhi ili hali Mufti sio chombo cha kisheria.
Hakuna sheria inayounda ofisi ya Mufti isipokuwa uwepo wake unategemea katiba ya BAKWATA. Maana yake ni kwamba Mahakama ya Kadhi uwepo wake utategemea uwepo wa Katiba ya Bakwata inayounda ofisi ya Mufti. Kukiwa na mgogoro wa kikatiba Bakwata athari yake itaikumba na Mahakama ya Kadhi. Hakuna duniani mtu ambaye ofisi yake haiundwi na sheria kisha sheria ikampa mtu huyo madaraka ya kuunda chombo chenye mamlaka ya kisheria kama mahakama. Serikali ya CCM inalijua hili lakini imefanya makusudi kwa kusukumwa na nia yake ya kutopenda kuona Waislamu wanakuwa na Mahakama ya Kadhi ya ukweli iliyo madhubuti.

3. Kama tulivyoeleza hapo juu MUSWADA umempa Mufti mamlaka ya kutengeneza kanuni za uendeshaji wa Mahakama za Kadhi hili ni jambo la ajabu sana kwa ofisi ambayo haiundwi na sheria kuwa na mamlaka ya kutengeneza kanuni za kuendesha chombo cha kisheria ambacho ni Mahakama ya Kadhi. Hili ni jambo ambalo haliwezekani.

4. Kwa madaraka makubwa aliyopewa Mufti sheria haielezi ni nani mwenye mamlaka ya kumuondoa kadhi na wala haiweki sifa za kadhi na wala haiweki vigezo vinavyoweza kumuondoa kadhi yote hii inadhihirisha nia ya serikali ya CCM kuunda Mahakama ya Kadhi legelege na kiini macho.

5. MUSWADA unaeleza Waziri anayehusika na mambo ya sheria kupewa mamlaka ya kutunga taratibu za kutekeleza hukumu za Mahakama za Kadhi bila ya kushauriana na wanazuoni wa Kiislamu.
Japo katika sehemu ya maelezo ya muswada Mwanasheria wa Serikali ameeleza kuwa Waziri atashauriana na wanazuoni maelezo hayo ni hewa kwani si sehemu ya sheria.

6. MUSWADA umetoa hiyari kwa mtu kufungua shauri katika Mahakama ya Kadhi.
Jambo hili limekusudiwa kuifanya Mahakama ya Kadhi iwe butu na kutoa mwanya wa kutokea mgongano baina ya Mahakama ya Kadhi na mahakama za kawaida ikiwa kila upande katika mgogoro utaamua kufungua shauri katika mahakama tofauti. Hili lisingewezekana kama serikali ingekuwa na nia ya kweli ya kuunda Mahakama ya Kadhi madhubuti.

7. MUSWADA kuitaka Mahakama ya Kadhi ijiendeshe yenyewe:

MUSWAAD huu unaitaka Mahakama ya Kadhi ijiendeshe yenyewe badala ya kuendeshwa na serikali jambo ambalo halijawahi kutokea sehemu yeyote duniani chombo kama mahakama kujiendesha chenyewe.

Mahakama ya Kadhi itafanya jukumu la serikali katika kutafsiri sheria za Kiislamu ambazo ni sheria halali kutumika Tanzania hakuna mantiki yoyote kwa chombo hicho kujiendesha chenyewe kama ambavyo serikali ya CCM inataka kufanya.

Isitoshe uwepo wa hii Mahakama ya Kadhi kutaipunguzia serikali mzigo na msongamano wa kesi katika mahakama za kawaida jambo ambalo serikali inapaswa kugharamia uwendeshwaji wake. Serikali kukataa kuigharamia hii Mahakama ya Kadhi ilihali katika nchi hii upande wa Zanzibar serikali inaiendesha Mahakama ya Kadhi kunadhihirisha kuwa kuna nia ya kuidhoofisha mahakama hii ishindwe kujiendesha na kuwa na mahakama isiyokuwa na maana yoyote.

Zipo mahakama za makundi ya watu maalumu ambazo zinaendeshwa kwa pesa za serikali ambazo ni kodi za Watanzania wote. Mfano ni kama vile Mahakama ya Kazi, Ardhi, Biashara n.k. ni kwanini mahakama itakayotafsiri sheria za Kiislamu iwe nongwa?

8. UTAFITI unaonyesha kuwa suala la Mahakama ya Kadhi huletwa kila unapokaribia Uchaguzi Mkuu bila ya utekelezaji linazidi kutupa wasiwasi kwani inaonesha serikali ya CCM imeshazowea kuwacheza shere na kuwalaghai Waislamu na Watanzania kwa ujumla kwa maslahi yao ya kisiasa. Tabia hii ni hatari sana kwa mustakabali na ustawi wa taifa letu.

Hitimisho
Ndugu wanahabari, kwa maelezo yaliyobainishwa katika taarifa hii, tunahitimisha kwa kusema:

a) Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) zimeukataa na kupinga mapendekezo ya marekebisho kwenye sheria ya tamko la Sheria ya Kiislam kama lilivyo katika MUSWADA wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali na. 02 wa mwaka 2014, mpaka utakapo andaliwa upya kwa kuhusishwa wanazuoni wa Kiislamu, wanasheria wa Kiislamu waliobobea na kwa kuzingatia maslahi ya Waislamu na taifa kwa ujumla na pia Mahakama ya Kadhi ni lazima iingizwe katika Katiba ili kuipa uthabiti.

b) Kwa kuwa katiba inayopendekezwa haitambui Mahakama ya Kadhi na inapinga sheria yoyote inayokwenda kinyume na katiba hiyo ikiwemo Sheria za Kiislamu kwa kauli moja na kwa nguvu kubwa Jumuia na Taasisi za Kiislamu (T) zitawahamasisha Waislamu na Watanzania kwa ujumla kuikataa kwa KUPIGA KURA YA HAPANA katiba inayopendekezwa muda utakapofika wa kuipigia kura.

Ndugu waandishi wa habari,
Ahsanteni sana kwa ushirikiano mliotupa.

Tunawatakia kazi njema katika ujenzi wa taifa letu.

Kaimu Katibu
………………………….

Jumuiya na Taasisi za Kiislam (T)



Msalani uko wapi uje uitete ccm
 
Ikiwa ndiyo msimamo wa Waislam, basi naam, kura yangu itakuwa ni hapana, siwezi kwenda kinyume na Waislam wenzangu hata siku moja, kinachotuunganisha Waislam ni kamba ya Mwenyeezi Mungu.

Hiyo katiba siioni ina maana gani kama haitambui kuwa kuna Waislam na wana haki zao za msingi.

Kesho bakwata itakuja na kauli ya kupinga hili tamko wewe utakuabwapi
 
Acha kupotosha. kura ya hapana haimaanishi tunarudi kwenye katiba ya 1977. bali tunakwenda kurekebisha iyo katiba ya ccm

Pindi yanapofanyika hayo marekebisho tunakuwa tunatumia katiba ipi? Hata hivyo ikukae akilini kuwa hata yafanyike marekebisho mara hamsini, mahakama ya kadhi haiwezi kuwemo kwenye katiba. Mnavyofikiria nyie kupiga kura ya hapana ili kulazimisha Mahakama ya kadhi basi ndivyo wakristu tutakavyopiga kura ya hapana pindi mahakama ya kadhi itakapowekwa.
 
Siipendi CCM, lakini kwa suala la Mahakama ya kadhi, naiunga mkono CCM 100%.
 
Mahakama ya Kadhi kuanzishwa nchi hii haitatokea,Waislamu tafuteni mambo mengine ya msingi ya kudai kwasababu hili la mahakama ya kaadhi haliwezekani.
 
sielewi hapa

huelew nin nchi hii haina dini ila watu wake wana dini kwa mana ya kwamba uko huru kuabudu unavyojua ww na wala hutaingiliwa sasa unapotaka hela ya serikali itumike kwa mambo yenu ya dini hapo ndipo unapoleta matatizo
 
Mimi si muislamu na sitaki kuamini kua uanzishaji wa mahakama ya kadhi hapa Tanganyika utakua na athari kwa taifa.Mi nadhani ianzishwe tu mbona nchi nyingine wana mfumo huo na hakuna shida?.Mwaka huu msikubali ahadi.

Mahakama ya Kadhi ina athari kwa Kanisa na Nchi kwa sababu ni IBADA.Kazi ya ibada ni ya dini husika hivyo serikali haipaswi kujiegemeza kwenye Dini moja na kueneza Hadithi za Mtume.Kikanisa ina athari kwa sababu Kodi ya Mkristo aliyotoa baada ya kuuza Kitimoto itatumika kueneza Ibada ya Dini ya Kiislamu.Hiyo ni sawa na kushiriki kueneza Dini ya Kiislamu ambayo kimsingi sio Mungu wao anayotaka wayaishi;Kumbuka wakristo wanaaswa na Mungu wao kutokuabudu Miungu mingine.
 
Isijekuwa tu hawa baraza kuu la Waislaam wanatumiwa na watu fulani fulani, maana sijawahi kuona jema lao hawa.

Al Alama Mohamed Said, Ritz, THE BIG SHOW, na Waislam wengine humu jF, hebu tuwekane wazi kidogo, tuungane nao hawa au kuna kamchezo hapa tusikokajuwa?

Maana hii taasisi ilianzishwa na Nyerere hii ambae si Muislam na hakuwa na jema kwa Waislam.

Taasisi ipi, jumuiya ya waislam au bakwata?

Kwa kukusaidia bakwata imeasisiwa na nyerere na ndio muhimili mkubwa CCM kwa maswala ya uchaguzi
 
Last edited by a moderator:
Isijekuwa tu hawa baraza kuu la Waislaam wanatumiwa na watu fulani fulani, maana sijawahi kuona jema lao hawa. Al Alama Mohamed Said, Ritz, THE BIG SHOW, na Waislam wengine humu jF, hebu tuwekane wazi kidogo, tuungane nao hawa au kuna kamchezo hapa tusikokajuwa? Maana hii taasisi ilianzishwa na Nyerere hii ambae si Muislam na hakuwa na jema kwa Waislam.
Kumbe na wewe hujui mwelekeo, yaani upo upo tu, ndiyo maana umesema utafuata watakachosema waislamu nilifikiri utafuata misingi ya dini ya kiislamu.
Ikiwa ndiyo msimamo wa Waislam, basi naam, kura yangu itakuwa ni hapana, siwezi kwenda kinyume na Waislam wenzangu hata siku moja, kinachotuunganisha Waislam ni kamba ya Mwenyeezi Mungu. Hiyo katiba siioni ina maana gani kama haitambui kuwa kuna Waislam na wana haki zao za msingi.
 
Huu uzi utafungwa muda si mrefu.

Naam,na ufungwe maana hauna tija.Hapa tunajadili mambo ya kitaifa na sio ya vikundi.Hatuwezi kukaa hapa kujadili Mahakama ya Kiislamu kwa niaba ya wenye mahakama yao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom