Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Status
Not open for further replies.
Ni lazima Serikali iwaambie waislam ukweli. [size=+2]Lazima tukubali kwenye nchi ambazo zina serikali za ki-secular kama ya kwetu ni ngumu kuwa na Mahakama ya Kadhi yenye nguvu kama za Saudi Arabia au Kuwait.. Hata huko Zanzibar mtu akiiba hawampeleki kwa kadhi ila Jamhuri ndiyo inamfungulia mashtaka....

Lazima tufahamu sheria zimegawanyika katika mafungu mawili makubwa..

(i) Public Law.. Hizi zinalinda maslahi mapana ya umma kwa maana ya Jamhuri, Mfano sheria za jinai nk. Hapa mtu akifanya kosa anashtakiwa na Jamhuri... yule uliyemdhuru anabaki kuwa shahidi tu.. hapa hakuna dini, kabila, utamaduni wala rangi ya mtu.. Kama umefanya kosa lazima utashakiwa kwa kuvunja sheria za nchi na kwa minajili ya kulinda maslahi mapana ya taifa..

(ii) Civil/private Law.. Hizi zinasimamia maslahi ya mtu mmoja mmoja.. Mfano sheria za mikataba, ndoa nk. Hapa ni mtu vs mtu.. na sheria itakayotumika ni ile ambayo kosa limeangukia.. Kama ni mgogoro wa ndoa basi mgogoro utatatuliwa ama kwa kutumia sheria za kimila kama ndoa ni ya kimila, kama ni ya kiislam itabidi utumike utaratibu wa kiislam vivyo hivyo kwa ndoa ya kikristo..

KWANINI MAHAKAMA YA KADHI NI VIGUMU KUFANYA KAZI TANZANIA.??

Mahakama ya Kadhi inaendeshwa kwa kutumia Sharia Law, kwa maana ya kitabu kitakatifu cha Quran, Hadithi za Mtume nk. na lazima utambue kuwa Uislam ni mfumo uliokamilika kwa maana ya taratibu, sharia, mira, desturi, imani/dini vyote vinakwenda kwa pamoja. Sasa [size=+2]ili Mfumo huu uweze kufanya kazi kwa ukamilifu wake unahitaji watu wenye tamaduni, mila, desturi imani/dini moja.. Hivyo Sheria zake zinakuwa rahisi kusimamiwa na Serikali kwa sababu watu wote ni wa Mfumo mmoja..[/size]

[size=+2]Lakini kwa nchi kama ya kwetu yenye mchanganyiko wa sio tu dini, bali pia tamaduni, desturi mila na kadharika ni ngumu ku-impliment Sharia Law.. Na kwa sababu tunaishi katika Jamhuri mmoja lazima kuwepo na mfumo ambao utaweza ukawajumuisha watu wenye imani, dini na tamaduni tofauti.. yaan Secular state...[/size]

Kwa mchanganyiko wa jamii yetu.. kuwa na Mahakama ya Kadhi yenye nguvu ni ndoto za mchana na lazima Waislam wakubali ukweli huo.. Chukulia Mkristo kaibiwa na Muislam.. au Muislam kaibiwa na Mkristo utatumia Sheria gani hapo ili kutenda haki????

Lazima ukweli ubaki ukweli!! Tatizo limeletwa na CCM kwa kuwapa Waislam matumaini makubwa yasiyotekelezeka ili wajipatie kura..

Niwashauri tu ndugu zangu waislam lazima tujitahidi kujenga Taasisi zetu zenye nguvu, ueledi na fedha ili kuwatumikia waislam kwa yale mambo ya kiimani na kijamii tu. La sivyo hakuna kitu hapo..

[/SIZE]

Umenena vema mkuu!
 
Hapo hakuna dilemma, hapo tunawaonesha namna ya kudai haki zetu Kiusalama kabisa.

Na Waislam waliwengi tukiamua kura ya hapana basi ujuwe katiba pendekezwa haipiti.

Na sasa hatutaki ahadi, na wakati wa kura za Urais na ubunge, uzi ni hohuo. Mpaka watu watie akili.

Baraza Kuu tuko pamoja, naunga mkono hoja.
inabidi muwe na msimamo huo huo kura ya hapana na muwakumbushwe waislam mwaka 2010 jk aliwandanganya hivyo sasa hivi msidanganyike 2015 ccm ikataliwe na katiba kura ya hapana
 
Huwezi kupata mahakama ya kadhi ambayo inagharamiwa na watu wa dini tofauti, hilo halitawezekana sio Tanzania hii anza kulielewa na kulikubali. Ulivyoambiwa nchi haina dini maana yake ni kwamba hakuna mahakama ya kadhi elewa hilo.

Wewe umepotoka au pombe zinakusumbua, hakuna nchi ulimwenguni ambayo ina waislamu hata kwa asilimia 40% kusiwe na Mahkama ya kadhi ambayo inatambuliwa kikatiba ili kuweza kikidhi matatizo na waislamu kupata haki zao. Tanzania Bara peke yake waislamu hawawezi kupungua asilimia 60% si kwambii Zanzibar ambao ni 99% waislamu.

Waislamu tunaelewa ukishakuwa mkiristo basi ata haki unaweza kuikataa na kupinga kupinga tu mana ndivyo ukiristo. Ivi wewe ulitegemea waislamu haki zao zikatatuliwe na mahakama zenu za ki-mission ambazo hawana taaluma juu uislamu?.

Ivi nyinyi Nyerere munamchukuliaje kama nabii ama mtu aliyekuwa na sifa ya kipekee tofauti na mwanadamu wa kawaida kwamba amesema Tanzania haina dini na nyinyi munatii tu.

Dunia inakuwa wakati wa Julius Nyerere sio wakati wa sasa, sasaivi kuna mambo mbali mbali yanahitaji ufumbuzi waislamu wameona kuna haja ya kuwa na Mahkama ya kadhi tena itambuliwe kikatiba ili matatizo yao yaweze kuwa solved kwa mujibu wa dini yao ilivyotaka, Kama ukiristo haukufundisha nyinyi kuwa na mahkama, Uislamu kwa mujibu wa Quran inafahamisha ivyo kwanini munaleta porojo porojo ambazo hamna elimu nazo?.

Waislamu walio Tanzania nao ni Watanzania hawana sehemu nyengine ya kwao ila Tanzania kwanini wanyanyaswe?
 
Umetumia ad hominen arguments ie argument by character assassination. Mambo ya pombe yanatoka wapi? Sitakujibu, ndio nyinyi "waislamu" mnaozungumzia mahakama ya ardhi, labour court and the like being equivalent and Kadhi's court!

Ndo mana tunasema kwamba kama mumeweka pamba za masikio hamuelewi Mahkama ya Kadhi, waislamu tunafanya kampeni nchi nzima kuzuia Katiba mpya
 
Nimesoma comments nyingi za wachangiaji, kuna kitu wanachanganya ama laah mtoa uzi ndio amewapotosha! Kuna vyombo viwili ambavyo vya Waislam ambavyo vinasigana!
  1. Kuna BAKWATA! Hawa ndio wale pale makao makuu kinondoni Muslim. Ndio hawa wanaodaiwa kuwa na nasaba na CCM, kwamba wana uhusiano mzuri pia na serikali, wengine wanaenda mbali zaidi, wanasema BAKWATA pia ina uhusiano mzuri na vyombo vya wakristo! Mkuu wake ni Muft Shaaban Simba! Hawa sio waliotoa tamko linalotajwa hapa!
  2. Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu, hawa ndio wapinzani wakubwa wa BAKWATA, na moja wa kiongozi wao ni Sheikh ISSA PONDA!

Hii maana yake nini, BAKWATA hawana muda wala mpango wa kulaani lolote lile ambalo limefanywa na serikali, na kwa hiyo siku zote wako na mgogoro na hao namba 2, ambao kwao CCM na Serikali wote ni adui wa uislam Tanzania. Tamko tajwa hapo juu, limetolewa na kundi hili namba 2 (kwa mujibu wa mtoa uzi)
 
With all due respect, hivi kweli mahakama ya kadhi inaweza kuwa sawa na mahakama ya ardhi, biashara etc?

Yale yale ya Ubalozi wa Vatican ni sawa na OIC!

Kwa hoja hizi sioni kiongozi yeyote yule aliye makini to give a damn shit
 
Alafu na sisi waislamu bwana tuna shida sana, bado hatuna uelewa wa pamoja katika maswala yetu. Maana tunapoisema CCM imekataa, maana yake tunamuweka wapi mwenyekiti wa CCM, ambaye ni mwenzetu katika hili. Ni nini msimamo wake katika swala hili. Maana sijawahi hata siku moja kumsikia akionesha msimamo wake hadi sasa miaka yake 10 inakwisha, angekuwa ni mgalatia tungesema wakristo wanatukwamisha, lakini mmmmhhh!!

alishawaruhusu waanzishe huko ila isiwemo ndani ya katiba huo ndo ulikuwa msimamo wake ukiwasikiliza ma ustaz wao wanataka iwepo kikatiba na kupewa nguvu kama mahakama zingine jk yy alitaka ijitegemee.
 
Isijekuwa tu hawa baraza kuu la Waislaam wanatumiwa na watu fulani fulani, maana sijawahi kuona jema lao hawa.

Al Alama Mohamed Said, Ritz, THE BIG SHOW, na Waislam wengine humu jF, hebu tuwekane wazi kidogo, tuungane nao hawa au kuna kamchezo hapa tusikokajuwa?

Maana hii taasisi ilianzishwa na Nyerere hii ambae si Muislam na hakuwa na jema kwa Waislam.
Hakuna kutumiwa hapa mama FaizaFoxy. Huu ni msimamo wa Waislam wote wanaojielewa wajibu wa kuletwa kwao hapa Duniani.

Aliyoanzisha Nyerere ni Bakwata ambalo tofauti na lilikotoka tamko hili. Hao uliowataja juu wote, wanaiheshimu taasisi hii ya Jumuiya na Taasisi za Kiislam kuliko hawa wahuni bakwata. Bakwata kamwe hawawezi kutoa tamko la namna hii. Wako busy kuuza viwanja na majengo ya wakfu pamoja na kuandaa mechi za mpira za kuleta amani. Tuungane-Kwa kamba ya Allah!
 
Last edited by a moderator:
Huwezi kupata mahakama ya kadhi ambayo inagharamiwa na watu wa dini tofauti, hilo halitawezekana sio Tanzania hii anza kulielewa na kulikubali. Ulivyoambiwa nchi haina dini maana yake ni kwamba hakuna mahakama ya kadhi elewa hilo.

Hivi ni upungufu wa ufahamu wako ama bado tukugeiye muda huenda ikawa khalafu ukajafahamu pole pole kwa kuwa yarukhusika sio....!?

Zile alizo idhinisha yule Mmasai na jopo lake ziende kwenye ati Spitali za Makanisa na Skuli zake (MoU) zile hazina tatizo kwakuwa zachangiwa na "KODI" za Wakristo pekee sio....!?

Hizo dhihaka na kujivika kwenyu upogo kwa upande mmoya wa Watanzania(WAISLAAMU) wenzenyu sasa tamati ndo yakuijieni kwa kwasi.

Ahsanta na nipo kipembeni hapa.
 
Hatulitambui Baraza kuu la waislam Tanzania.Chombo cha kuwasemea waislam ni kimoja tu hao wengine wanapoteza muda buree.BAKWATA ndio chombo rasmi cha kuwasemea waislam wote Tanzania.
 
Hivi ni upungufu wa ufahamu wako ama bado tukugeiye muda huenda ikawa khalafu ukajafahamu pole pole kwa kuwa yarukhusika sio....!?

Zile alizo idhinisha yule Mmasai na jopo lake ziende kwenye ati Spitali za Makanisa na Skuli zake (MoU) zile hazina tatizo kwakuwa zachangiwa na "KODI" za Wakristo pekee sio....!?

Hizo dhihaka na kujivika kwenyu upogo kwa upande mmoya wa Watanzania(WAISLAAMU) wenzenyu sasa tamati ndo yakuijieni kwa kwasi.

Ahsanta na nipo kipembeni hapa.


Mkuu naomba kukuuliza hizo hospitali na skuli zinahudumia wananchi wa dini zipi? Je zianahudumia wananchi wa dini nyingine na hata wasiokuwa na dini? Hizo mahakama za kadhi zitahudumia wananchi wa dini ipi? Je zitahudumia wananchi wote hata wa dini nyigine na wasiokuwa na dini?
 
Hapa ndipo ninaposhindwa kuwaelewa waislamu.
★kwanza,unawezaje kulinganisha maakama ya kadhi na mahakama ya ardhi au biashara?! Mimi James nikichukua ardhi ya Juma basi Juma atanishtaki mahakama ya ardhi,na mwishowe Juma atapata haki yake! Sasa je Juma akiamua kunipeleka mahakama ya kadhi,mm James nitaridhika vpi kama kuna haki imetendeka?
★Au tufanye Anna ameolewa na Haji then Haji akafariki..na ndugu zake Haji wakataka mirathi igawiwe na mahakama ya Kadhi!unadhani mahakama itawatambua watoto na mama yao kama warithi halali?!
★Pili sifa zakuajiliwa kwenye hiyo mahakama zitakuwa zipi!kitakachotokea ni waislam tu ndio watakao pata ajira huko!sasa hii itawafanya wakristo wakose hizo ajira kabla hata haijatangazwa wakati wao pia huchangia kulipa mishahara ya hao wafanyakazi wa mahakama ya kadhi.

Mfano mimi girlfriend wangu ni dada FF na imethibitishwa kuwa tunagegedana, je yeye atapigwa mawe mpaka afe na mimi nitakula mikwaju 100,?
 
niliwahi kuandika humu kwamba waislam wasitegemee kujengewa mahakama ya kadhi na serikali ya ccm watakuwa wanajidanganya wenyewe.nimejifunza kitu ingekuwa ni wakirsto tungekuwa tunataka hizo mahakama tungejenga wenyewe sasa nyie mnasubiri kujengewa na ccm mtasubiri sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom