Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Status
Not open for further replies.
Mkuu nisaamehe kama mepituka.

Ila kuna lugha nyingi mno za kuongea na mwanziwako.

Mie naliekezwa na Mwalimu wangu mstaabu mno na tokamana naye nalijaalika kujifunda tabia na mienendo yake na si kama ile ya "NDIYO" pasi na kuhoji.

Mfano mmoya katika mambo alonifunda ni "ONGEA NA MTU/WATU KWA KADRI YA AKILI ZAO".

Sasa nakuuliza weye ambaye busara zimekujaa, hivi ulikitaka nitukanwe na mie ninyong'onyee na kulalama kipembeni huoni ntaingia DHAMBINI....!?

Ile kanuni ya kupigwa shavu la kushoto na ati ugeuze na kulia mie kwa haki sina kabisa.

Ahsanta na nipo kipembeni hapa.

Shetani mkubwa wewe
 
Hata Mohamed Said ungepewa uraisi wa Tanzania, nakuhakikishia hutaweza kuinfluence mahakama ya kadhi igharamikiwe na serikali, ama kwa kupitia katiba, kwa sheria za nchi au hata kwa udikteta... hutaweza...

Mimi ni mpinzani mkubwa wa CCM, lakini nina uhakika kwa hili mnawaonea...

Tuko,
Umenitaja na kawaida yangu mtu akinitaja huwa namjibu kwani huo ndiyo
ustaarabu.

Mahakama ya Kadhi ilikuwapo Tanganyika toka enzi na enzi hadi mwaka
1963 na ikigharimiwa na serikali toka enzi za ukoloni.

Nani alizipiga marufuku na kwa kisa gani hili labda ndilo liwe swali lako
la kuuliza baada ya kunisoma.
 
FF mimi kutokua muislamu haimaanishi siupendi au naupinga uislamu maana katika mfumo wangu wa kuabudu sijawahi kuathiriwa na uwepo wa uislamu.Na maisha yangu naishi na waislamu na ndio marafiki zangu wakubwa.ndio maana nikasema hata ikianzishwa sidhani kama itaathiri imani yangu au mfumo wangu wa kimaisha.So ianze tu kwa sababu kama nyie mtakua Happy kwa uanzishwaji wa mahakama hiyo basi itakua ni neema kwa nchi yote.

uwezo wako wa kufikiri umeishia ku conclude eti mahakama.ya kadhi haita kuhusu. ikisha ingia kwenye katiba itakuhusu tena sana tu, kama huamibi jiulize simple question why wanaforce iingie kwenye katiba
 
Boko haram wanadai mahakama ya kadhi
Al shabaab wanaendesha mahakama za kadhi. na ni hivyo hivyo huko Niger, Algeria, mali, CAR nk wooote hawa wanadai mahakama za kadhi.
1. Hali za kiuchumi za wanaodai mahakama za kadhi ni mbaya
2. Uelewa wao juu ya mahakama za kadhi ni mdogo sana
3. Historia ya utekelezaji wa sheria katika nchi zinazoendesha mahakama ya kadhi ni mbaya

Bakwata sio wasemaji huru wa waislam, na Bakwata wanaongelea kundi moja tu la waislam na hawajui vizuri mahitaji na matakwa halisi ya waislam. Bakwata wants to become/look relevant kwa kuonyesha kwamba wao hawalali kitanda kimoja na CCM.

Ukweli ni kwamba Bakwata wanalala kitanda kimoja na CCM. Ni vigumu kwa BAKWATA kukubaliwa na vyama vya upinzani sababu BAKWATA ni taasisi ya CCM kama ilivyo UWT.
 
samahani nifahamishwe, kwani hii mahakama ya kadhi ndio ile inayoamrisha wakosaji wapigwe mawe hadi kufa? au wakatwe mikono kama wameiba?

Paluhengo,
Mahakama ya Kadhi inashughulika na mirathi, ndoa na talaka.

Hizi mahakama zipo India, Uingereza, Zanzibar, Afrika Kusini na kwengine
kwingi.

Hazikati wezi mikono wala wazinifu wahapigwi mawe.
 
Mi mkristo sioni tatizo kwa uwepo wa hito mahakama ila shida ni nani watahukumiwa na hizo mahakama .Kama ni ya kiislamu na kwa waislamu na kwa maswala maalumu yatakayoainishwa sioni tatizo

Msulibasi,
Mahakama ya Kadhi ni kwa ajili ya Waislamu.
 
Na sisi tunataka mahakama ya amri kumi za mungu kama Joseph Konyi
 
Boko haram wanadai mahakama ya kadhi
Al shabaab wanaendesha mahakama za kadhi. na ni hivyo hivyo huko Niger, Algeria, mali, CAR nk wooote hawa wanadai mahakama za kadhi.
1. Hali za kiuchumi za wanaodai mahakama za kadhi ni mbaya
2. Uelewa wao juu ya mahakama za kadhi ni mdogo sana
3. Historia ya utekelezaji wa sheria katika nchi zinazoendesha mahakama ya kadhi ni mbaya

Bakwata sio wasemaji huru wa waislam, na Bakwata wanaongelea kundi moja tu la waislam na hawajui vizuri mahitaji na matakwa halisi ya waislam. Bakwata wants to become/look relevant kwa kuonyesha kwamba wao hawalali kitanda kimoja na CCM.

Ukweli ni kwamba Bakwata wanalala kitanda kimoja na CCM. Ni vigumu kwa BAKWATA kukubaliwa na vyama vya upinzani sababu BAKWATA ni taasisi ya CCM kama ilivyo UWT.

Tetere,
Baraza hili si BAKWATA...

Soma tena tamko kwa uangalifu...
Hayo mengine mie sina haja ya kuyasemea labda wengine watakujibu.
 
Msulibasi,
Mahakama ya Kadhi ni kwa ajili ya Waislamu.

wawape hiyo mahakama .waislamu wa leo wameenda shule wata handle hiyo mahakama yao.Jambo jingine labda je ni waislamu wote wanaitaka hii mahakama?Je ni namna gani tutaweza kufahamu nani anataka nani hataki au waislamu watapiga kura?Unajua inaweza kuwa kundi linalosisitiza hii mahakama ni kundi lenye msimamo mkali au vipi
 
Kwani kuna dini au madhehebu gani ambayo imeomba mahakama ?!....kwa ajili ya kesi gani !?Hii ni njia moja wapo ya kukimbia ukweli kuhusu kuanzisha Taasisi hii !
teh tehee! Kumbe hamna ubavu hadi mdungwe ndoba na makafir wenzenu!
 
Mbona mapepo mnahangaika nayo Kanisani kila jumapili, yale mmesambaziwa na nani !? Jungle Warrior

Nyie ndo mnasambaza, halafu cjui yanawasaidia nini maana uchumi wenu duni, elimu duni, kazi kushinda kwenye vijiwe vya bao mkinywa gahwa na kashata halafu mnalalamika hovyo eti serikali ina mfumo Kristo.

Fanyeni kazi acheni kulialia hovyo.
 
Last edited by a moderator:
Hawa jamaa hata waende shule ndefu namna gani uelewa huwa down kabisa!! unalinganisha mahakama ya kazi, ardhi ambavyo ni vyombo vya serikali na kadhi ambacho ni chombo cha kidini!! Huyu mwamedi alikuwa na spirit ya kutoelewa kabisa!!
mbavu zangu mie....
 
nyie niwajinga kweli sijapata kuuona,yaana kiti cha urais ndio mlitegemea uwawekee mambo yenu kwenye katiba ya wananchi,basi teueni shelh agombee huo urais ndiye atawatimizia yote hayo
 
Hii nchi haina dini jamani. Kila dini/dhehebu likitaka mahakama yake tutafika wapi jamani? Ndugu Waislamu litafakari zaidi hili. Ndio maana hata kufungisha ndoa ni mamlaka ya dini husika na serikali haigharamii shughuli za ufungishaji ndoa za wakristo wala waislamu

Hata Mohamed Said ungepewa uraisi wa Tanzania, nakuhakikishia hutaweza kuinfluence mahakama ya kadhi igharamikiwe na serikali, ama kwa kupitia katiba, kwa sheria za nchi au hata kwa udikteta... hutaweza...

Mimi ni mpinzani mkubwa wa CCM, lakini nina uhakika kwa hili mnawaonea...

Kwanini watoe ahadi hewa sasa, kama suala haliwezekani basi watoe elimu kwa wananchi kwamba kwakua hakuna fungu lolote pesa linaloenda kwa wasio waislamu basi vivyo hivyo haitawezekana kwa waislam kutengewa fungu kisha wangetoa mawazo mbadala wa kufanikisha hili.
 
Last edited by a moderator:
chh
attachment.php

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM (T)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

17 Mfungo Sita 1436
9 Januari 2015

TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM TANZANIA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI KWA WATANZANIA WOTE, JUU YA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI NA. 02, WA MWAKA 2014, HUSUSAN KUHUSU SEHEMU YA MAREKEBISHO KWENYE SHERIA YA TAMKO LA SHERIA ZA KIISLAM

Awali ya yote tunapenda kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu, Ardhi na vilivyomo, na Rehma na Amani zimfikie Kiongozi wa Ummah Mtume Muhammad (SAW).

Ndugu wanahabari,
Assalam Alaykum Warahamatul llah Wabarakatuh.

Tumekuiteni hapa kwa lengo la kueleza kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 02, wa mwaka 2014 haswa kuhusu marekebisho kwenye sheria ya tamko la Sheria za Kiislamu. Tunafahamu kuwa kuanzia tarehe 13 hadi 23 Mwezi huu wadau mbalimbali wataitwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo yao, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania tukiwa sehemu ya wadau muhimu tunapenda kuwaeleza kuwa mtiririko wa mchakato wa marekebisho ya sheria kwa mujibu wa muswada huu unaokusudia kutambua Mahakama za Kadhi Tanzania bara una kasoro kubwa na kwa dhati unaonesha wazi kuwa serikali haina nia ya kweli ya kuunda Mahakama ya Kadhi yenye hadhi kamili ya kimahakama na uthabiti wa kuwepo kwake na kuwa muswada huu ni hadaa nyingine ya serikali hii ya CCM kwa Waislamu kwa sababu zifuatazo:-

1. Malalamiko juu ya Mahitaji ya Mahakama ya Kadhi yana historia ya kupindishwapindishwa na serikali hii inayoundwa na CCM.
Kwa mfano katika Ilani ya CCM mwaka 2005 iliahidi kuanzisha Mahakama ya Kadhi lakini kwa ghilba nyingi CCM haikutekeleza ahadi hiyo baada ya kuingia madarakani kwa hoja kuwa hili ni jambo la Kikatiba.

Hata hivyo mchakato wa Katiba mpya ulipokuja asilimia kubwa ya maoni ya Waislamu yalihitaji Mahakama ya Kadhi kuingizwa ndani ya Katiba, mapendekezo hayo yalikataliwa na Tume ya Jaji Warioba kwa hoja kuwa katiba inayotengenezwa ni ya Muungano na suala la Mahakama ya Kadhi si la Muungano hivyo lisubiri wakati wa kuandaa Katiba ya Tanganyika. Waislamu tukavumilia kuisubiri Katiba ya Tanganyika.

Lakini Bunge Maalum la Katiba likaikataa Katiba ya Warioba na kutunga Katiba Mpya Pendekezwa yenye mambo yote ya Muungano na yasiyo ya Muungano bila ya kuingiza Mahakama ya Kadhi kama ilivyoahidiwa na Tume ya Jaji Warioba. Bunge la Katiba lililokuwa linaundwa na wajumbe wengi wa CCM hawakuona umuhimu wa kutimiza ahadi yao ya kuweka Mahakama ya Kadhi katika katiba pendekezwa na kwa makusudi Mahakama ya Kadhi ikakataliwa na wajumbe wengi wa CCM walishangilia jambo hili ili hali wanajua dhahiri kuwa Waislamu hawakufurahishwa na uamuzi wao na pia kukiuka Ilani yao na ahadi kwa Waislamu.

Muswada huu ni sehemu nyingine ya hadaa kwa Waislamu kwani badala ya sheria kuanzisha Mahakama ya Kadhi kama ilivyo kawaida ya uanzishwaji wa mahakama zote duniani muswada huu umeliacha jukumu hilo kwa taasisi binafsi ili hali Mahakama ya Kadhi kama zilivyo mahakama zingine ni sehemu ya chombo cha dola katika mfumo wa Mahakama yaani "the Judiciary", hili limefanywa makusudi kutokana na kutokuwepo na nia ya dhati ya Serikali ya CCM kuanzisha na kuona Tanzania Bara kunakuwa na Mahakama ya Kadhi madhubuti na ya ukweli.

2. MUSWADA umempa mamlaka "Mufti" kuteua makadhi na kutengeneza kanuni za Uendeshaji wa Mahakama ya Kadhi ili hali Mufti sio chombo cha kisheria.
Hakuna sheria inayounda ofisi ya Mufti isipokuwa uwepo wake unategemea katiba ya BAKWATA. Maana yake ni kwamba Mahakama ya Kadhi uwepo wake utategemea uwepo wa Katiba ya Bakwata inayounda ofisi ya Mufti. Kukiwa na mgogoro wa kikatiba Bakwata athari yake itaikumba na Mahakama ya Kadhi. Hakuna duniani mtu ambaye ofisi yake haiundwi na sheria kisha sheria ikampa mtu huyo madaraka ya kuunda chombo chenye mamlaka ya kisheria kama mahakama. Serikali ya CCM inalijua hili lakini imefanya makusudi kwa kusukumwa na nia yake ya kutopenda kuona Waislamu wanakuwa na Mahakama ya Kadhi ya ukweli iliyo madhubuti.

3. Kama tulivyoeleza hapo juu MUSWADA umempa Mufti mamlaka ya kutengeneza kanuni za uendeshaji wa Mahakama za Kadhi hili ni jambo la ajabu sana kwa ofisi ambayo haiundwi na sheria kuwa na mamlaka ya kutengeneza kanuni za kuendesha chombo cha kisheria ambacho ni Mahakama ya Kadhi. Hili ni jambo ambalo haliwezekani.

4. Kwa madaraka makubwa aliyopewa Mufti sheria haielezi ni nani mwenye mamlaka ya kumuondoa kadhi na wala haiweki sifa za kadhi na wala haiweki vigezo vinavyoweza kumuondoa kadhi yote hii inadhihirisha nia ya serikali ya CCM kuunda Mahakama ya Kadhi legelege na kiini macho.

5. MUSWADA unaeleza Waziri anayehusika na mambo ya sheria kupewa mamlaka ya kutunga taratibu za kutekeleza hukumu za Mahakama za Kadhi bila ya kushauriana na wanazuoni wa Kiislamu.
Japo katika sehemu ya maelezo ya muswada Mwanasheria wa Serikali ameeleza kuwa Waziri atashauriana na wanazuoni maelezo hayo ni hewa kwani si sehemu ya sheria.

6. MUSWADA umetoa hiyari kwa mtu kufungua shauri katika Mahakama ya Kadhi.
Jambo hili limekusudiwa kuifanya Mahakama ya Kadhi iwe butu na kutoa mwanya wa kutokea mgongano baina ya Mahakama ya Kadhi na mahakama za kawaida ikiwa kila upande katika mgogoro utaamua kufungua shauri katika mahakama tofauti. Hili lisingewezekana kama serikali ingekuwa na nia ya kweli ya kuunda Mahakama ya Kadhi madhubuti.

7. MUSWADA kuitaka Mahakama ya Kadhi ijiendeshe yenyewe:

MUSWAAD huu unaitaka Mahakama ya Kadhi ijiendeshe yenyewe badala ya kuendeshwa na serikali jambo ambalo halijawahi kutokea sehemu yeyote duniani chombo kama mahakama kujiendesha chenyewe.

Mahakama ya Kadhi itafanya jukumu la serikali katika kutafsiri sheria za Kiislamu ambazo ni sheria halali kutumika Tanzania hakuna mantiki yoyote kwa chombo hicho kujiendesha chenyewe kama ambavyo serikali ya CCM inataka kufanya.

Isitoshe uwepo wa hii Mahakama ya Kadhi kutaipunguzia serikali mzigo na msongamano wa kesi katika mahakama za kawaida jambo ambalo serikali inapaswa kugharamia uwendeshwaji wake. Serikali kukataa kuigharamia hii Mahakama ya Kadhi ilihali katika nchi hii upande wa Zanzibar serikali inaiendesha Mahakama ya Kadhi kunadhihirisha kuwa kuna nia ya kuidhoofisha mahakama hii ishindwe kujiendesha na kuwa na mahakama isiyokuwa na maana yoyote.

Zipo mahakama za makundi ya watu maalumu ambazo zinaendeshwa kwa pesa za serikali ambazo ni kodi za Watanzania wote. Mfano ni kama vile Mahakama ya Kazi, Ardhi, Biashara n.k. ni kwanini mahakama itakayotafsiri sheria za Kiislamu iwe nongwa?

8. UTAFITI unaonyesha kuwa suala la Mahakama ya Kadhi huletwa kila unapokaribia Uchaguzi Mkuu bila ya utekelezaji linazidi kutupa wasiwasi kwani inaonesha serikali ya CCM imeshazowea kuwacheza shere na kuwalaghai Waislamu na Watanzania kwa ujumla kwa maslahi yao ya kisiasa.
Tabia hii ni hatari sana kwa mustakabali na ustawi wa taifa letu.

Hitimisho
Ndugu wanahabari, kwa maelezo yaliyobainishwa katika taarifa hii, tunahitimisha kwa kusema:

a) Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) zimeukataa na kupinga mapendekezo ya marekebisho kwenye sheria ya tamko la Sheria ya Kiislam kama lilivyo katika MUSWADA wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali na. 02 wa mwaka 2014, mpaka utakapo andaliwa upya kwa kuhusishwa wanazuoni wa Kiislamu, wanasheria wa Kiislamu waliobobea na kwa kuzingatia maslahi ya Waislamu na taifa kwa ujumla na pia Mahakama ya Kadhi ni lazima iingizwe katika Katiba ili kuipa uthabiti.

b) Kwa kuwa katiba inayopendekezwa haitambui Mahakama ya Kadhi na inapinga sheria yoyote inayokwenda kinyume na katiba hiyo ikiwemo Sheria za Kiislamu kwa kauli moja na kwa nguvu kubwa Jumuia na Taasisi za Kiislamu (T) zitawahamasisha Waislamu na Watanzania kwa ujumla kuikataa kwa KUPIGA KURA YA HAPANA katiba inayopendekezwa muda utakapofika wa kuipigia kura.

Ndugu waandishi wa habari,
Ahsanteni sana kwa ushirikiano mliotupa.

Tunawatakia kazi njema katika ujenzi wa taifa letu.

Kaimu Katibu
………………………….

Jumuiya na Taasisi za Kiislam (T)


cheki pozi lao,wamekaa kiubwabwa ubwabwaaa!hapo chini lazima wana mijeledi
 
Kwa lugha nyepesi ni kwamba nchi yetu na watu wake wana dini na imani tofauti,tofauti, na ukweli serikali imeweka utaratibu wa watu kuendesha shughuli hizo.

Kusema Tanzania haina dini, ila watu wake wanadini, hii sielewi maana yake. Kwangu naona ni lugha ya kuwachanganya watu, tu, bila hao watu unao waita watanzania, ambao ndio wanadini, huwezi kuwa na tanzania. Ila nikweli tuna taratibu za kuziendesha.
 
sasa kwa nn msikubaliane wenyewe tu,mkawa mnajisurubu wenyewe misikitini??sasa mnachotaka kutoka serikalini n nn???

Hiyo Mahakama uishaambiwa ilikuwepo na ilitambulika hata na Serikali ya Kikoloni hadi mwaka 1963.

Suali ni je, nani aliiondosha na kwa malengo gani na kama pana badali ya ile Mahakama /Chombo cha kusimamia mambo /masuala ya Waislaamu ni kipi na kiliekwa na nani....!?

Ahsanta huenda /labuda weye baadaye ukajafahamu kama ukajiepusha na mazogo /ushabiki.

Nipo kipembeni hapa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom