Nandagala One
JF-Expert Member
- Aug 19, 2020
- 1,913
- 2,286
MOja kwa moja kwenye mada,siku za karibuni kumekuwa na zoezi la serikali kutoa pesa kuchangia makanisa.
Makanisa mbalimbali likiwemo Kanisa Katoliki, Takatifu la Mitume, ambalo makanisa yake yamepokea pesa za serikali ya CCM.
Nataka kuchukua mfano
Jimbo la Zanzibar hasa ambalo limepokea fedha toka Serikali ya Zanzibar kwa ajili ya ukarabati wa kanisa kiasi Cha milioni 200.
haijulikani kama wao Jimbo Mhashamu Agustino Shao wa Holly Ghost Father's aliomba, au wao serikali waliombwa wachangie, au sijui serikali ilijuaje kama Kuna uhitaji.
Ni aibu nijuavyo hasa tunapoelekea uchaguzi mkuu kupokea fedha toka wanasiasa.
Siamini kwamba Jimbo la Zanzibar halina namna ya kupata fedha kukarabati kanisa.
Nijuavyo Project manager wa jimbo au administrator anao uwezo kwa ruhusa ya Askofu kuandika project Ulaya ikajibu, namfahamu padre mmoja wa Jimbo la Zanzibar aliyekaa sana Ulaya Marekani , Siamini Padre Damas Mfoe wa jimbo la Zanzibar angalishindwa ,kama angaliombwa kuandika, badala yake Jimbo limepokea fedha za mwanasiasa Dr Hussein Mwinyi.
Baadhi ya majimbo hasa ya Kusini maparoko na wamama wakuu wa mashirika ya kitawa wanao uwezo wa kuandika project za shule ya chekechea, miradi ya akina mama, vituo vya watoto yatima zikajibu.
Ilikuwaje Askofu bwa Zanzibar apokee pesa Toka kwa mwanasiasa???
Pili Zanzibar kama eneo la utalii, kila kitu kilichoko Zanzibar ni utalii, makanisa na historia ya ukristu kwa wamisionari wa Holly Ghost Father's na wamisionari Wa Benedictine waliingia kwanza Zanzibar.
kwa mantiki hiyo ukarabati wa kanisa hata ingeandikiwa UNESCO wangejibu na kupata fundus fund kuliko pesa za wanasiasa wenye hila na mikono yenye dalili za damu na ambao kuingia Kwao madarakani Kuna shaka.
Mfano wa pili matibabu ya operesheni ya Askofu mkuu wa Jimbo kuu DSM Jude Thaddeus Ruwaich Ofm Cap yalifadhiliwa na Hayati Magufuli,haikuwa sahihi hata kidogo Jimbo kuu DSM Lina mapato ya kutosha Toka vyanzo mbalimbali, mfano mzuri Tegemeza Jimbo sio chini ya billion 1.5 kwa mwaka achilia vyanzo vingine.
Ilikuwaje mkubali serikali iingilie kati matibabu??
Wakati wa aliyekuwa Askofu msaidizi Kilaini Methodius naye alilipiwa matibabu India na JK.
Tumeona pia Arusha zaidi ya milioni 500 Jimbo katoliki Arusha limepokea bila kujali mazingira ya jambo husika.
Mlipata wapi ujasiri wa kukemea kwa njia ya waraka juu ya mkataba hovyo wa DP 🌍 Word kupewa Bandari zetu za BARA na Leo mmekuwa majasiri wa kupokea pesa Toka hao hao waliouza Bandari zetu mkitumia msemo
"I HATE PORK,BUT I LIKE IT'S SOUP"
Nielekee kuhitimisha, pesa hizi zinazoanza kusambazwa kwa njia ya hisani, kuchangia vitu,zina viashiria vyote ni pesa chafu, ya rushwa kwa Kanisa katoliki na Viongozi wa Kanisa.
Lengo la pesa hizi ni ku brain 🧠 wash Viongozi, na waumini, ni compromat,ili munyamaze kimyaa, msikemee matendo bya kishenzi ya Serikali ya CCM.
Week chache zilizopita Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Mwanza amenukuliwa ametoa maneno ya wazi yenye dalili za UCHAWA ndani yake kuhusu Serikali ya chama kuwa,
" Kama huoni maendeleo yaliyoletwa muulize mamako"
Sijui kauli hiyo ilikuwa yake au ni out of his emotional?? Haijulikani, haikumbukwi mahali popote pale ambapo aljaribu kuongelea rushwa, utekaji wa watu na kuuwawa kwa watu na utawala bora kiujumla.
Ninapoandika haya najua wazi kuwa muundo wa kanisa Katoliki kila Askofu Local ordinary wa Jimbo ana mamlaka yake ya kutoingiliwa na Jimbo lingine.
Lakini katika Hali tuliyonayo kama Taifa Maaskofu wakae waangalie kwa Tahadhari namna ya kukaa mbali na pesa chafu zinazomwagwa kama njugu, na ambazo vyanzo vyake havijulikani, yaani zimetika katika bajeti ipi??
Sekeseke la pesa za ESCROW Maaskofu kadhaa walikuwa wanufaika Tena pesa zao ziliingizwa katika personal account, na transaction nyingi zilifanyika kupitia Benki ya Kanisa katoliki Mkombozi Bank, hatukujifunza kupitia kosa hilo???
Rai kwa Baraza la Maaskofu TEC mintarafu Mhashamu Askofu Wolfgang Pissa OFM Cap wa Jimbo katoliki, tafuta namna ya ku address hizi pesa zinazoingia kwenye majimbo, parokia Toka wanasiasa hasa wakati huu tunakoelekea uchaguzi mkuu ili Kanisa Katoliki lisichafuke kwa hizi pesa chafu.
"Roma Locuta Causa Finita "
Niwatakie siku njema.