Baraza la Mitihani lakanusha Mtwara kushika nafasi ya mwisho matokeo kidato cha nne, yataka wananchi kupuuza taarifa hizo

Baraza la Mitihani lakanusha Mtwara kushika nafasi ya mwisho matokeo kidato cha nne, yataka wananchi kupuuza taarifa hizo

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Baraza la mitihani nchini NECTA limekanusha taarifa zilizozagaa mitandaoni kwamba mkoa wa Mtwara umeshika nafasi ya mwisho matokeo ya kidato cha nne.

Necta imewataka wananchi kupuuza taarifa hiyo kuwa shule 9 kati ya 10 zilizoshika nafasi za mwisho (umbwigi) zinatoka mkoani Mtwara.

Source: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

===
NECTA YAKANUSHA SHULE MTWARA KUBURUZA MKIA
Baraza la Mitihani nchini (NECTA) limekanusha taarifa za kuwa shule tisa kati ya kumi zilizoburuza mkia katika matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana zinatoka Mkoa wa Mtwara.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Habari na Uhusiano wa baraza hilo, John Nchimbi imebainisha kuwa taarifa hizo zililenga kuuchafua mkoa huo na kuwaomba wananchi kuzipuuzia taarifa hizo.

“Baraza linapenda kuujulisha umma kuwa taarifa hizo ni za uongo na zinalenga kuupotosha umma, kuleta taharuki na kudhalilisha Mkoa wa Mtwara.” Amesema Nchimbi

Nchimbi amefikia kutoa kauli hiyo mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa mapema hii leo kulitaka baraza hilo kutoa ufanuzi juu ya taarifa hiyo.

Taarifa: habarileo_tz
 
Siasa tupu hadi kwenye mambo ya msingi, serikali iliyopo madarakani imeifanya hii nchi iwe ya kuchekesha kupita maelezo.

Sasa nawashauri hao NECTA, next time mkitoa matokeo yenu msituambie shule kumi bora ni zipi, wala wanafunzi kumi bora kitaifa ni wepi, kwasababu imegundulika "mitandao" huwa inatoa taarifa za uongo.
 
Yesu na Mariamu! Kwahiyo shule hizi zipo Somalia au

View attachment 1679167
Bongo move wamekosa kazi sababu serikali imeamua kubeba jukumu la kuigiza movie 😄😄
Kwanini lakini kila kinachotokea Mtwara hawataki tujue?
No zipo Mtwara ila hizo shule zina matokeo mazuri zaidi ya shule zingine nyingi kimkoa na kitaifa. Ndio maana mkuu wa mkoa wa Mtwara alihoji ufafanuz juu ya hilo.

May be Necta walikurupuka kutoa hayo matokeo right now, na kama hilo limebainika waz, maana yake kuna madudu makubwa ndan ya matokeo yenyewe. Et ufaulu umeongezeka 5% wakt madudu tupu.

Hii ndo tz ya kasi😁
 
Nasikia ni typing eras
Watakuwa wakisha type huwa wanakimbilia tu habari maelezo kutoa taarifa, hawafanyi proof reading!.

Sasa watuambie hizo shule zimetoka sayari ya Mars, au nayo itakuwa inasingiziwa na "mitandao", basi tufanye Jupiter kwasababu ndio kubwa zaidi.
 
No zipo mtwara ila hizo shule zina matokeo mazr zaid ya shule zingine nying kimkoa na kitaifa. Ndo mana mkuu wa mkoa wa Mtwara alihoji ufafanuz juu ya hilo. May be Necta malikurupuka kutoa hayo matokeo right now, na kama hilo limebainika waz, maana yk kuna madudu makubwa ndan ya matokeo yenyewe. Et ufaulu umeongezeka 5% wakt madudu tupu.

Hii ndo tz ya kasi😁
Basi hata walioongoza kwa ufaulu sio kweli!

Kwa maelezo haya hii mitihani inatakiwa urudiwe nchi nzima
 
Basi watuwekee hizo shule top -10 ili kukata mzizi wa majungu
Wasipo tuwekea tutajua ni hizihizi na wanaogopa kutumbuliwa
 
Siasa tupu hadi kwenye mambo ya msingi, serikali iliyopo madarakani imeifanya hii nchi iwe ya kuchekesha kupita maelezo.

Sasa nawashauri hao NECTA, next time mkitoa matokeo yenu msituambie shule kumi bora ni zipi wala wanafunzi kumi bora kitaifa ni wapi, kwasababu imegundulika "mitandao" hua inatoa taarifa za uongo.
... approach iliyotumika kwa COVID-19 itumiwe na NECTA ili kulinda hadhi ya elimu yetu.
 
Back
Top Bottom