Baraza la Mtihani (NECTA) kushughulikia suala la Mwanafunzi aliyebadilishiwa namba ya Mtihani

Baraza la Mtihani (NECTA) kushughulikia suala la Mwanafunzi aliyebadilishiwa namba ya Mtihani

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mtahiniwa Iptisum Suleiman Slim kutoka shule ya Msingi Chalinze Modern Islamic amesema wakati akifanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) Oktoba 5-6, 2022 alipangiwa namba 40 lakini jina lake lilikuwa namba 39 kwenye katarasi ya kusaini.

Anasema alifanya mitihani 5 kwa namba 40 lakini mtihani wa 6 msimamizi akamwambia arudi kwenye namba yake ambayo ni 39, alipohoji kuhusu mabadiliko hayo Msimamizi alimjibu watalifikisha suala lake Baraza la Mitihani (NECTA).

Leo Oktoba 14, 2022 Baraza la Mitihani (NECTA) limetoa taarifa ya kupokea malalamiko ya mwanafunzi huyo na kueleza kuwa linafanyia kazi suala hilo kuhakikisha anapata haki yake.

1665735230465.png
 
Hata hivyo baraza wamezingua, kwanini hawajaunda tume? Wamejibu kana kwamba wana uhakika ni tukio la bahati mbaya tu.
 
Hii issue inazunguka kwenye mitandao. Mitihani yote watumie namba ya mtihani na picha kuondoa hii kitu. Yawezekana kabisa kuna watu wanawafanyia watoto wengine. Kama huyu mtoto kabadilishiwa namba ni kweli inaumiza sana
 
Mtahiniwa Iptisum Suleiman Slim kutoka shule ya Msingi Chalinze Modern Islamic amesema wakati akifanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) Oktoba 5-6, 2022 alipangiwa namba 40 lakini jina lake lilikuwa namba 39 kwenye katarasi ya kusaini.

Anasema alifanya mitihani 5 kwa namba 40 lakini mtihani wa 6 msimamizi akamwambia arudi kwenye namba yake ambayo ni 39, alipohoji kuhusu mabadiliko hayo Msimamizi alimjibu watalifikisha suala lake Baraza la Mitihani (NECTA).

Leo Oktoba 14, 2022 Baraza la Mitihani (NECTA) limetoa taarifa ya kupokea malalamiko ya mwanafunzi huyo na kueleza kuwa linafanyia kazi suala hilo kuhakikisha anapata haki yake.

View attachment 2386751
Hii ndiyo Tanzania, wanayoyafanya wahuni wa chini ni matokeo ya wahuni wa juu
 
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema linafanyia kazi tuhuma alizozitoa mwanafunzi wa shule ya msingi Chalinze Modern Islamic, Mkoa wa Pwani, Iptisum Slim aliyedai kubadilishiwa namba yake ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi Oktoba 5-6, 2022.

Kupitia video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii mwanafunzi huyo mhitimu wa darasa la saba, 2022 amemuomba Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda kuingilia kati madai ya kufanya mtihani na namba ambayo si yake.

Leo Oktoba 14 kupitia taarifa iliyotolewa na Afisa Habari na Uhusiano Necta, John Nchimbi imeeleza baraza hilo linafanyia kazi taarifa hiyo ili mwanafunzi huyo apate haki yake.

“Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limeona taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mtahiniwa Iptisum Suleiman Slim wa Shule ya Msingi Chelinze Modern Islamic ‘Pre and Primary School akisema kwamba alibadilishiwa namba yake ya mtihani wakati akifanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi uliofanyika tarehe 5 na 6 Oktoba 2022.

“Baraza linaifanyia kazi taarifa hiyo kuhakikisha mwanafunzi huyo anapata haki yake,”imeeleza taarifa hiyo.
Iptisum kupitia video hiyo alionekana akiomba msaada huku akieleza, siku ya mtihani wa taifa alivyoingia darasani alipangiwa namba 40 na wakati karatasi ya kusaini ilivyopita alisaini namba 39.

Ameeleza kuwa baada ya kufanya mitihani mitano kupitia namba 40 ambayo si yake alihamishiwa namba 39 ambayo ni yakwake.

“Baada ya mtihani kuisha baadhi ya wanafunzi tuliitwa na mwalimu mkuu tukaambiwa yale yaliyotokea yasisikike sehemu nyingine yaishie palepale.
“Naomba msaada nisaidiwe kisheria kupata haki majibu yangu yarudi kwenye namba yangu kwa sababu mtoto niliyemfanyia mtihani anashika nafasi ya chini na mimi nashika nafasi za juu hata Mtihani wa Moko wilaya nilishika nafasi ya kwaza,”ameeleza mtoto huyo.

Pia kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima ameandika

“Mtoto wetu mpendwa sana, kwanza pole kwa mtihani, hongera kumaliza darasa la saba. Badala ya kumaliza upumzike wamekutengenezea jambo. Kwa nafasi yako kama mtoto iwapo hili limetokea nao ni ukatili kwa mtoto.
“Waziri wa Elimu na NECTA wapo pamoja na wewe mtoto mzuri kuchunguza hili Ili haki itendeke.

“wizara yenye dhamana na maendeleo ya watoto jicho letu, sikio letu na mguu wetu vipo walipo watoto wanaolalamika kwa chochote hivyo, katika hilo tunaungana na wizara ya Elimu hadi tuone mwisho wa hii hoja” Dk Gwajima

Source:Mwananchi
 
Hivi tuhuma kama hii inahitaji muda mrefu kuifanyia kazi. NECTA si ina namba ya mtahiniwa huyu! Suala si ni la wao mara moja tu kwenda kuhakikisha tu jambo hilo katika shule husika, na hatimaye kuja na majibu!.?

Suala kama hili kuchukua zaidi ya siku moja kulishughulukia ni uzembe. Uwepo wa tuhuma hii ya binti huyu inaleta taswira mbaya sana katika sekta ya elimu hapa nchini.

Vyuo vya elimu ya juu kuna tuhuma nyingi za ngono na ukilaza, huko TLS kuna lile linalofukuta hivi sasa, huko kwenye CPA na "other professional bodies" kuna maumivu yake japo hawanung'uniki hadharani. Sasa pia hata huku kwenye elimu ya ngazi za chini!?
 
Nimeskia uchungu sana kama mwanangu, mwalimu mkuu anafanya hujuma za namna hii. Inaonekana mwalimu mkuu amekula mlungula ili yule mtoto anayeshika nafasi za chini abebwe kwa matokeo ambayo amefanyiwa na mtoto mwingine . Pole sana comrade iptsam slim.
 
Hivi tuhuma kama hii inahitaji muda mrefu kuifanyia kazi. NECTA si ina namba ya mtahiniwa huyu! Suala si ni la wao mara moja tu kwenda kuhakikisha tu jambo hilo katika shule husika, na hatimaye kuja na majibu!.?

Suala kama hili kuchukua zaidi ya siku moja kulishughulukia ni uzembe. Uwepo wa tuhuma hii ya binti huyu inaleta taswira mbaya sana katika sekta ya elimu hapa nchini.

Vyuo vya elimu ya juu kuna tuhuma nyingi za ngono na ukilaza, huko TLS kuna lile linalofukuta hivi sasa, huko kwenye CPA na "other professional bodies" kuna maumivu yake japo hawanung'uniki hadharani. Sasa pia hata huku kwenye elimu ya ngazi za chini!?

Laweza chukua dakika 20, ila utaratibu ndo unatakiwa ufuatwe
 
Hapo jamaa wanangoja per diem za kukaa kikao cha kuliangalia hili suala. Tena wanaweza kusafiri kbsa kwenda hoteli kubwa nje ya mji kudiscuss hiki kitu
 
Back
Top Bottom