Baraza la Mtihani (NECTA) kushughulikia suala la Mwanafunzi aliyebadilishiwa namba ya Mtihani

Baraza la Mtihani (NECTA) kushughulikia suala la Mwanafunzi aliyebadilishiwa namba ya Mtihani

Hii ilishatokea kwa mdogo wangu. Baada ya kukataa kutoa rushwa kwa mwalimu, alibadilishiwa namba akamfanyia aliyetoa rushwa.

Dogo langu alikuwa anaongoza darasa lakini matokeo waliofaulu ni wale mbumbumbu kabisa na yeye kapiga chini.

Nilikuja kujua muda umeenda sikuwa na jinsi ila iliniuma sana.
Nilimpeleka dogo private na sasa ni bosi sehemu.

Yuke mwalimu aliyefanya hivyo huwa na aibu sana akikutana na mimi au dogo maana tulimwambia live.

Japo kastaafu ila Mungu anamwadhibu
 
Daah aisee kuja watu wakatiliii sana huwa hawafikirii juu ya hatma ya maisha ya wenzao kabisaa...!! Huyo mwalimu ni shetani
 
aisee!!! hili jambo linatisha sana.
inaonekana walimu wakuu wanacheza dili na wazazi ambao watoto wao ni vilaza, kwa kucheza na namba za mitihani za wanafunzi ambao wana uwezo na wale wasio na uwezo ili kuwafaulisha.

unakuta mtoto ambaye rekodi yake ya kufaulu ni nzuri halafu unashangaa mtihani wa darasa la saba anafeli!! halafu yule mwenye rekodi mbovu anafaulu kupitia udanganyifu kama huu!!!

Ushauri kwa BARAZA NECTA;
katika kusahihisha mitihani hii waangalie rekodi za nyuma za mitihani ya Taifa haswa mtihani wa Darasa la nne 4, matokeo ya darasa la 4 yataonyesha uwezo wa mtoto tangu mwanzo, kama kuna udanganyifu wowote basi utabainika kupitia kumbukumbu za ufaulu wa nyuma.
 
Hii ilishatokea kwa mdogo wangu. Baada ya kukataa kutoa rushwa kwa mwalimu, alibadilishiwa namba akamfanyia aliyetoa rushwa.

Dogo langu alikuwa anaongoza darasa lakini matokeo waliofaulu ni wale mbumbumbu kabisa na yeye kapiga chini.

Nilikuja kujua muda umeenda sikuwa na jinsi ila iliniuma sana.
Nilimpeleka dogo private na sasa ni bosi sehemu.

Yuke mwalimu aliyefanya hivyo huwa na aibu sana akikutana na mimi au dogo maana tulimwambia live.

Japo kastaafu ila Mungu anamwadhibu
Whaat?poleni sana jamani!haya mambo lini yataisha,watu hawaogopi Mungu jamani kaahh!
Na Mungu anawaadhibu Mara nyingi hawafikagi mbali hao dhulumati
 
Hapo jamaa wanangoja per diem za kukaa kikao cha kuliangalia hili suala. Tena wanaweza kusafiri kbsa kwenda hoteli kubwa nje ya mji kudiscuss hiki kitu
Ni sawa. Mimi nipo kwenye vitengo kama hivi. Kuna mambo inabidi mka discuss nje ya nchi akili inakuwa fresh na pia mnawaalika na wataalamu wa huko wawape uzoefu. So kwa hili suala nadhani wanaweza watu kulifanyia uchunguzi na upembuzi yakinifu hata China hapo. Then wanaleta majibu. Ni kawaida tu ili kuwe na ufanisi mzuri.
 
Script iliandikwa vizuri, akapewa msomaji.

Swali je kwenye mtihani aliandika namba ngapi?
 
Mtahiniwa Iptisum Suleiman Slim kutoka shule ya Msingi Chalinze Modern Islamic amesema wakati akifanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) Oktoba 5-6, 2022 alipangiwa namba 40 lakini jina lake lilikuwa namba 39 kwenye katarasi ya kusaini.

Anasema alifanya mitihani 5 kwa namba 40 lakini mtihani wa 6 msimamizi akamwambia arudi kwenye namba yake ambayo ni 39, alipohoji kuhusu mabadiliko hayo Msimamizi alimjibu watalifikisha suala lake Baraza la Mitihani (NECTA).

Leo Oktoba 14, 2022 Baraza la Mitihani (NECTA) limetoa taarifa ya kupokea malalamiko ya mwanafunzi huyo na kueleza kuwa linafanyia kazi suala hilo kuhakikisha anapata haki yake.

View attachment 2386751
Hii inawezekanaje? Kwa kawaida mwanafunzi anakaa kwenye dawati lililobandikwa namba yake. Je ina maana alipoambiwa atumie namba 40 badala ya 39 alihama dawati kabisa? Na aliyekuwa amekaa kwenye dawati hilo alipelekwa wapi, au walibadilishana? Huyo ndiye suspect wa kwanza.
 
Hii umeitoa wapi mchochezi wewe!!??
Huo uharifu misingi yake ni nini? Japo alihoji akaishia kupewa vitisho, hakuogopa kutafuta haki yake. Huyu atakuwa na damu ya mu-Iran, ni mwanaharakati by nature
 
Hii inawezekanaje? Kwa kawaida mwanafunzi anakaa kwenye dawati lililobandikwa namba yake. Je ina maana alipoambiwa atumie namba 40 badala ya 39 alihama dawati kabisa? Na aliyekuwa amekaa kwenye dawati hilo alipelekwa wapi, au walibadilishana? Huyo ndiye suspect wa kwanza.
Umehamisha goli? suspect wa kwanza amekuwa mwanafunzi badala ya mwalimu?
 
  • Thanks
Reactions: Cyn
kumbe kufaulu darasa la Saba imerudi kuwa dili …mie najua hata wasiojua kusoma na kuandika huwa wanafaulu siku hizi

enzi zetu ndio ilikuwa dili …nakumbuka hadi leo Matokeo yangu yaliyonisisimua kwa furaha zaid katika maisha yangu ni matokeo yangu ya darasa la saba kwa kuwa ilikuwa ni mtikisiko wa eneo kubwa kwa kuwa mna faulu watatu katika ya 100 na inawapa heshma kubwa sana Wazee wako

kwanini Mwalimu hakumsaidia anaetaka kumsaidia kwa kumpa majibu badala ya kumpa mwingine amuandikie ?

inaweza ikawa kweli lakini pia inaweza ikawa vita vya kibiashara vya shule na shule
 
Ninavyoijua nchi hii vitawekwa vikao kutafuta mchawi na ma allowance kede kede. Kumbe hapo Ni kumuita msimamizi wa mtihani aliyembadilishia mtoto namba, mwalimu mkuu wa shule husika na kiongozi wa msafara wa wasimamizi.

Mchawi mbona anajulikana inakuwaje halmashauri na wizara zote elimu na tamisemi mna tapa tapa kwa kupenda semina,. Warsha na vikao???
 
Haha...ila huyo mkuu ndezi+kiroboto...hivi alifkiri itakuwa rahisi tu kumfanyia mtihani mwanafunzi mwingine? Serikali naomba hilo mlisimamie kidete na hatua kali zichukuliwe.
... Mungu mkubwa; hayo yametokea ....

Mtahiniwa Iptisum Suleiman Slim kutoka shule ya Msingi Chalinze Modern Islamic

... lau yangetokea St. Francis Mbeya au Mary Goret Moshi! Daaah!
 
Bint alishaandaliwa mazingira afeli aolewe, ameruka viunzi vya kidini dhidi ya elimu kwa mtoto wa kike, Mwenyezi amsaidie atimize ndoto zake
Mzazi angempeleka private kma alikuwa na lengo hilo?
 
Nimeskia uchungu sana kama mwanangu, mwalimu mkuu anafanya hujuma za namna hii. Inaonekana mwalimu mkuu amekula mlungula ili yule mtoto anayeshika nafasi za chini abebwe kwa matokeo ambayo amefanyiwa na mtoto mwingine . Pole sana comrade iptsam slim.
Ni kweli kabisa, lengo ilikuwa kumbuka huyo mwingine .
 
Hata hivyo baraza wamezingua, kwanini hawajaunda tume? Wamejibu kana kwamba wana uhakika ni tukio la bahati mbaya tu.
Wenyewe wanatimu Yao ya kiuchunguzi na uzuri ishu dogo kaieleza vizur kuunda tume ufujaji wa pesa
 
Mzazi angempeleka private kma alikuwa na lengo hilo?
Una uhakika huyo binti anasomeshwa na mzazi? Kumbuka pia hizi shule ni charity based, wanasomesha watoto kutoka familia zisizo na uwezo mkubwa. Kutokana na kujua kuwa ni maskini ndo maana walimuandalia hujuma hiyo. Kama angekuwa kwao mambo safi na kwa ufaulu huo hakuna ustadhi angejaribu kucheza na akili yake.
 
Back
Top Bottom