Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 267
- 1,014
Vyama vya Siasa 18 vyenye usajili wa kudumu vimeshiriki mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na kufanyika mjini Morogoro, huku CHADEMA ikiwa haijashiriki mkutano huo.
Akizungumzia mkutano huo leo Februari 11, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, amesema pamoja na mambo mengine, vyama hivyo vimejadili umuhimu wa kuzingatia masuala ya jinsia katika siasa ili kuhakikisha wanawake wanapata nafasi sawa ya kushiriki katika siasa, hatua itakayosaidia utekelezaji bora wa majukumu yao.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Juma Haji Hatibu, amesema lengo ni kla mkutano huo ni uboresha na kupanga sheria pamoja na kanuni za Uchaguzi.