Mimi mwenyewe nimeshangaa ana eti kupata passport lazima uwe na safari ambayo nayo inahitaji vithibitisho Kibao.... upumbavuu mtupu.That bullshit [hiyo sababu ya safari].
Hakuna kabisa mantiki ya kunyima watu hiyo hati kama hawana safari.
Kuna ubaya gani mtu kuwa nayo halafu awe nayo tayari endapo atapata safari?
Wakati mwingine hitaji la kusafiri hujitokeza kwa muda mfupi tu kutokana na sababu mbalimbali.
Sasa kama mtu tayari anayo pasipoti, anakuwa keshapunguza usumbufu wa kuitafuta.
Kwa nchi zingine wala huhitaji kuwa na safari ndo upewe.
Ukiomba tu unapewa. Madhali umetimiza vigezo vinavyohitajika.
Kuhusu pasipoti kutumiwa kimakosa, hiyo haina mashiko kabisa.
Na wakati Kuna viinchi kama Rwanda hapo kagame alishawaambia Kila raia inabidi awe na passport haijalishi kama ana mpango wa kusafiri au laah...
Anyway hili taifa la Wala vumbi ni la kipuuzi sana.