Barua ya mwaliko ili kupata passport

Sawa na kitambulisho cha NIDA
wageni wanapata kiurahisi ila watz sasa
 
Vipi na sisi ambao tunateseka tukiwa hapa hapa kwenye hii nchi yenu ya Maziwa na asali, mbona hatuoni huo msaada wao???
Huku unaweza kuonana na wajomba, shangazi n.k wakakusaidia ata viazi vya kuchemsha.
Sasa huko ugenini kama huna shughuli ya maana, utaonekana kama uchafu unaotembea na kuchafua mazingira.
 
Roho zinawauma wakiona mtu anataka kutoka wanajua ataenda kutusua wakati wao wanataka watu wateseke hapa hapa Bongo
Hili linaukweli kwa 100% yaani pure facts.

Kikawaida mtanzania ni mtu mwenye roho mbaya sana na si mkarimu kama ambavyo huwa tunajinasibu.... Na mbaya sana hiyo roho mbaya mara nyingi huwa tunaionesha kwa watanzania wenzetu, ila kwa mgeni huwa ni full kujipendekeza.

Umeongea ukweli kabisa, mtanzania huwa anafurahi sana kuona mtanzania mwenzake anaishi kwa taabu wakati huo yeye ana auheni ya maisha.

Wale maafisa uhamiaji huwa wanafurahi sana kuona umekwama kuondoka hapa nchini, maana wanaamini kinachokukimbiza huku ni Hali ngumu ya kimaisha na ukifanikisha kuondoka pengine utaenda kuishi vizuri huko uendako kuliko wao wanavyoisha hapa nchini, hivyo kuondoka kwako roho lazima ziwaume hasa kama destination yako ni first world country.
 
Wqpi nimemwambia adanganye? Huelewi unachokisoma?

Mbona wao wanamdanganya mpaka apeleke barua ya mwaliko?

Lakini kwa JF ya siku hizi, inaweza kuwa mleta mada kajitungia tu.
Sijajitungia ni ukweli
 
Upo sahihi kabisa.
 
huyu jamaa hajawahi kusafiri nje ya nchi hizo mambo za barua ya mwaliko na copy ya passpot ya unaye enda kumtembelea huko nje ya nchi hii ni kwa maombi ya VISA ila mtoa mada kaandika passport badala ya Visa waliomuelewa watamsaidia
Boss, ni ishu ya passport baada ya kulipia 20k inayohitajika ilikupakua form online baada ya kumaliza kujaza taarifa nikaenda ofisini ndio nimekutana na hiyo ishu ikabidi niwe mpole nikarudi na makablasha yangu
 
Kwamba hii ndio sababu kubwa ya wao kuweka hicho kigezo cha ovyo???

Kwamba nikialikwa na mtu ndio siwezi kuzamia huko baada ya muda wangu wa kustay kuwa umeisha au?

Mbona sababu ni nyepesi na ya kipuuzi sana?
Sababu zipo nyingi mkuu, lakini hiyo ni mojawapo kuondoa hofu ya uhamiaji haramu. Kuna sababu nyingine kama kuthibitisha safari yako kama ni ishu ya kutembelea familia, charity nk, lakini pia kuthibitisha muda wa kukaa, kuonyesha uhusiano wako na mwenyeji wako kama ni shirika, mtu binafsi nk, kwa kifupi hayo ndio baadhi ninayayafahamu mimi.
 
Naomba ni pm connection ya kishoka Kama unayo
 
Sasa siuwaambie naenda afcon mambo yasiwe mengi unapewa mbona makampuni kubao yanasafirisha watu kwenda kutizma michuano mbalimbali kimataifa
 
Swali lilikuwa unamtu unakoenda kufikia nikasema ndio, mjamaa akasema basi tuletee barua ya mwaliko na picha ya passport yake ili tuambatanishe
Waambie unaenda msibani. Mimi ilikuwa 2022 hakukuwa na hizo mambo za barua, labda mambo yamebadilika. Je kama wewe huna passport lakini unapata mgeni kutoka huko nje, so atazuiliwa huko atokako kwa sababu wew huna passport? Wanamaanisha mwenyeji naye lazima awe na passport ili kupata mgeni? Invitation letter sawa.
Hizi huwa ni mambo ya kutaka visa
 
Naomba ni pm connection ya kishoka Kama unayo
Ni check mimi pm tuyajenge. Wewe utakaa home tu mpaka siku ya kuja kuweka finger print. Muhimu sana NIDA au Namba yako ya NIDA. Hizo docs nyingine zinapatikana steshenary na pale pale uhamiaji
 
Ila kama unaenda South Sudan, fast unapewa uende ukafe huko
 
Wewe nielimisha hapa hapa japo kwa kifupi tu...

Mimi nimekuwa nikifahamu nchi hii hairuhusu uraia pacha, ila wewe umeni surprise kwamba mtoto wa miaka 18 anaruhusiwa kuwa na urai pacha, Sasa ndio nataka unifahamishe zaidi kuhusiana na Hilo...
Mtoto wa mtanzania aliyezaliwa kwenye nchi inayotoa uraia wa kuzaliwa mara mmoja (bila kujali asili ya wazazi, mfano Marekani), anakuwa na uraia pacha, mpaka atakapofikisha miaka 18. Baada ya hapo, atachagua uraia mmoja anaotaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…