Sababu zipo nyingi mkuu, lakini hiyo ni mojawapo kuondoa hofu ya uhamiaji haramu. Kuna sababu nyingine kama kuthibitisha safari yako kama ni ishu ya kutembelea familia, charity nk, lakini pia kuthibitisha muda wa kukaa, kuonyesha uhusiano wako na mwenyeji wako kama ni shirika, mtu binafsi nk, kwa kifupi hayo ndio baadhi ninayayafahamu mimi.
Mimi kuwa na barua ya mwaliko wa safari haiwezi kunizuia kuwa muhamiaji haramu huko niendako kama lengo langu ndio Hilo, kwani baada ya Mimi kuondoka hapa nchini watakuwa Wana ni monitor huko nilipo au?
Kimsingi tu hizo sababu ulizoziweka hapo hazina uzito wa kimantiki hata kidogo... Mbona mataifa mengine hapa Afrika hayana huu ujinga?
Hivi unajua kwamba unavyotoa easy Access ya watu kuondoka inchini hata serikali Inakuwa imepunguza mzigo kwa namna Fulani hivi?? Kuna inchi kama Nigeria Moja ya njia ya kupunguza mzigo mzito walionao kutokana na population yao serikali inawapa urahisi wa kuondoka inchini raia wake wakatufute fursa sehemu nyingine... Na ndio maana wanaijeria wametapakaa duniani kote Wana msemo wao wanasema
"if you visit any part of this world and you don't find Nigerian, oga the place you visited is not meant for human being.
Leo hii ukienda nchi kama USA hili ukutane na mtanzania basi lazima kwanza uwe umeshakutana na wanaijeria kama 200 na wakenya kama 50 kisha ndio unakuta na mbongo Sasa... Yaani watanzania hawapo kabisa huko duniani na sababu Moja wapo ni Mambo kama haya ya ugumu wa kupata kwanzia passport.
Mwaka Jana Kuna report niliiona ikielezea idadi ya wanafunzi wanaotoka afrika waliko kwenye vyuo vikuu vya Canada.
Wanaijeria walikuwa 20,000, Waghana 11,000 wakenya wako 8,000 halafu wanafunzi wa kitanzania wako sijui 1,200.
Unaweza ukaona jinsi gani sisi Bado tumejifungia humu ndani tukidanganyana eti nchi yetu ni ya Maziwa na asali huku fursa mbali mbali za kielimu na kiuchumi zikitupita sababu ya kuendekeza mambo ya kijima.
Ndio maana Kuna muda huwa naamini taifa hili limelaaniwa na Mungu maana Kuna mambo mengi sana ya ovyo