Barua ya wazi kwa dada Halima Mdee

i
ingekua kashinda mbowe na wakina lema wala wengine isingekua big deal
 
Naunga mkono hoja
P
 
Pascal Mayalla hili suala sijui kwanini linawagusa sana CCM kuliko hao wapinzani wenyewe

Wakati Halima na wenzake wanavunjwa mikono wakitumia haki zao za kikatiba si CCM wala wapiga debe waliosimama hata kukemea. Leo CCM wale wale wanataka sana idadi ya wanawake na kumshauri Mdee !

Ukweli ni mmoja, kutokuwepo kwa kambi ya upinzani kuna madhara kwa Bunge na taswira ya nchi.
Jitihada zote ni kutaka waende ili kuhalalisha kilichofanyika, Pascal unajua na kila mtu anajua

Idadi ya Wabunge wa CCM inatosha kabisa na sidhani akidi haitimii kwa kukosa wabunge 19 au 20.

Wabunge wa CCM, Spika na NEC wajikite kujadili kuwaletea wananchi maendeleo kwa Bunge la CCM na sidhani uwepo au kutokuwepo kwa watu 19 ni tatizo kwao.

Suala la Wapinzani kwenda au kutokwenda liachwe kwao wenyewe waamue , si suala la kitaifa ni la vyama.

Wapinzani wana haki ya kukubali fadhila dhidi ya Haki au kukataa fadhila ili kuitetea Haki, ni wao si suala la kitaifa na wala lisiwe mjadala wa Taifa. Waacheni wakae Ufipa na kuamua.

Mnavyozidi kushawishi mnaondoa hata shaka iliyokuwepo! nimejiuliza kwanini kuna ushawishi kiasi hiki?

JokaKuu Mag3 tindo Sky Eclat
 
Ccm mna shida gani mbona nawaona mkihangaika sana na Chadema????
Mliwaibia wenyewe sasa mnaleta story hapa! Si baba yenu aliwaambia policcm na Necccm wasimchanganyie???
Alitaka abaki na ccm tu!
Sasa mnalia nni???
 
Wapinzani Bungeni waliishi kama watoto yatima. Wakitaka kutoa hotuba ni lazima kwanza iende kwa speaker ihaririwe. Wakitaka kutoa hoja wanapewa dakika tano za kujieleza na katika hizo dakika tano kuna watakao ziingilia katika .. Utashangaa sasa hivi muda wa kutoa hoja ikawa dakika 15.
Tumewaachia Bunge wawe na amani.
 
Nelson Holishasha Madiba Mandela alipewa ''offer' na makaburu ya kuachiwa lakini aachane na siasa, akae kimya.
Mandela alikataa kwa hoja moja, hawezi 'ku-trade' haki yake na Fadhila za Makaburu, aligoma hadi alipotoka huru

Kuna hoja kwamba 'kwasababu ni wanawake ' ndiyo maana wanaume huko kwenye chama chao wanaogoma.
Hoja hii ni mfu au kwa lugha nyingine DOA( Dead on arrival). Sababu ni hii hapa:

Wanawake wa Chadema wakiongozwa na Halima na akina Bulaya walipokwenda kumpokea Mwenyekiti wao aliyebaki magereza walikutana na kundi la askari wanaume (si wanawake).
Akina Halima wakapondwa pondwa mikono na miguu na askari wanaume nusura ya kuwatoa roho

Leo ninaposoma CCM na akina Paskali wanasema hoja ni wanawake, nawauliza mbona hatukuwasikia wakiwatetea wakati wanavunjwa vunjwa miguu na mikono na wanaume!
Huu wema wa Bungeni umeanza lini na kwanini?

CCM wajisikie fahari, hawana bughudha tena Bungeni, wanaweza kufanya lolote na chochote bila kuulizwa

Kutokuwepo wanawake wa Upinzani si tatizo la CCM na wala si tatizo la kitaifa, ni tatizo la Chadema

Chadema na kundi la wanawake waachwe walumbane hapo Ufipa, wapime faida na hasara

Waitafakari jana, waitathmini leo na waibashiri kesho, na kama kuna sababu za ku trade fadhila na haki au kuitetea haki kwa gharama za fadhila, waachwe wenyewe waamue.

JokaKuu Mag3
 
Ni wazi kuwa Watanzania tulio wengi hatuelewi siasa. Siasa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, kodi tunazolipa ndiyo zinaiendsha serikali. Wengi tunafahamu kuwa upinzani ni uadui. Ukiangalia utaona hii ndiyo sababu iliyofanya Askari magereza kuwapiga wabunge wanawake wa Chadema walipokwenda kumpokea Mbowe.
 
wabunge wa viti maalum 19 hawaendi kwa matakwa ya CCM Wala chadema, wanaotakiwa kwa mujibu wa Sheria.
Lazima ujue neno mujibu wa sheria . Neno hilo lina maana uwepo wao ni takwa la kisheria! kwa maana kuwa wakienda ni sheria inayowalinda, lakini si takwa la lazima kwao kwenda.

Uwepo wao unalindwa na kuhesabika kisheria, lakini wao kwenda au kutokwenda hawafungwi na sheria

Hakuna Mbunge anayeshtakiwa kwa kutokwenda Bungeni, lakini, uwepo wake kisheria unakoma kwa masharti yaliyoainishwa kisheria .
Ila wasipoenda itakuwa ni kwa matakwa ya chadema hasa hasa Mbowe na genge lake wanaoonea wivu wanawake hasa wale small houses.
Well, kundi la wanawake linatokana na Chama. Hivyo, hakuna tatizo kama chao kitakuwa na maamuzi hayo.
Huu ndio msingi wa kupoteza Ubunge ukifukuzwa katika chama.
 
Mkuu Nguruvi3 , kwanza mtu kuwa kada wa chama chochote, hakuondoi haki yake kutoa mawazo yake kama Mtanzania mwingine yoyote, hivyo kwenye hili la Chadema kususia viti maalum, tusinyoosheane vidole kuwa linawagusa CCM sana kuliko wapinzani, linawagusa Watanzania wote regardless vyama vyao.

Vyama vya siasa Tanzania ni public parties vya wananchi na sio private parties vya wanachama, japo vinaanzishwa privately na wanachama na kuongozwa na wanachama, but the moment vinaanza kupokea ruzuku ya serikali, they automatically turn into public parties, because they receive taxpayers money, and hence the taxpayers have an interest and they deserve to serve the interest of the public and not of its its members, hivyo maamuzi yote ya chama, lazima yazingatie na kutanguliza mbele public interest, maslahi ya taifa kwanza.

Jee uamuzi huu wa Chadema kususia viti maalum umezingatia public interest?. Una maslahi kwa Chadema?. And in so doing, what do they expects to achieve?.


P
 
Pascal kama unaamini vyama vya siasa ni viko kwa public interests, huoni kama ni muhimu kuwa na fair game kati ya chama tawala na vyama vya upinzani?
 
Mkuu Nguruvi3 , kwanza mtu kuwa kada wa chama chochote, hakuondoi haki yake kutoa mawazo yake kama Mtanzania mwingine yoyote
Ni kweli kabisa ! na wala si kosa kuwa kada wa chama chochote
, hivyo kwenye hili la Chadema kususia viti maalum, tusinyoosheane vidole kuwa linawagusa CCM sana kuliko wapinzani, linawagusa Watanzania wote regardless vyama vyao.
Hapana! TL alipoondolewa Bungeni hatukusikia watetezi wa haki za vyama.
Kwa hili la wanawake, CCM wanahangaika sana, wewe kama kada unajua kwanini

Halima alipofukuzwa Bungeni hatukisikia maneno ya kumtetea.
Leo CCM wamaupata wapi wema tunaouona !
Vyama vya siasa vilipopigwa marufuku ya siasa mbona hatukuwasikieni mkilalamikia kodi za wananchi?

Wabunge walipo 'nunuliwa'' na kusababisha chaguzi za marudio na wao kurudi mjengo na mavazi ya kijani mbona hatukuwasikia akina kada na CCM.

Kodi zipi mnazodhani ni bora?
Ruzuku ni kodi lakini manunuzi na gharama za chaguzi ndogo ni haki na sawia! eh

Mkuu hoja yangu hapa ni moja, suala la kuwa wanaamua nini ni lao na pengine wanachama wa Chadema

Tunapoona wema wa CCM, NEC, Spika na Makada kuna maswali, kulikoni?

Yaani uone simba na Chui wana mashada wakihudhuria birthday ya swala! real!
 
Hakuna tija hizi ni blaa blaa tu waliopo bungeni wanatosha watatuletea maendeleo hii michezo yakujificha nyuma ya haki za wanawake ni stori tu wanatutosha haohao
 
Ni wazi kuwa Watanzania tukio wengi hatuelewi siasa. Siasa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, kodi tunazolipa ndiyo zinaiendsha serikali. Wengi tunafahamu kuwa upinzani ni uadui.
Na shaka ya uadui iliyojengeka ndiyo inazidi kurindima watu wanaposikia eti '' CCM, NEC, Bunge la CCM'' wanataka sana mchango wa wanawake wa Chadema! Siasa zimegeuka kuwa uadui sijui haya yanatokea kwanini na kwa faida ya nani.
Ukiangalia utaona hii ndiyo sababu iliyofanya Askari magereza kuwapiga wabunge wanawake wa Chadema walipokwenda kumpokea Mbowe.
Halafu 'bunge lina wa-miss'' aisee!
 
Serikali inataka kuwatumia wabunge wa Bawacha ku justify makosa yao kwa jumuia ya kimataifa.
 
Wananchi hawahitaji kushawishiwa juu ya CDM. Ipo mioyoni mwao
Mbona barabarani hawaendi?
Mbona Hao wanainchi hawajapinga matokeo ya uchaguzi kuwa amechaguliwa mtu ambae wao hawakumpigia kura?

Au ww unazungumzia wanainchi wa dunia gani
 
Thank you brother
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…