Bashar Assad akwepa mtego wa Kuiingiza Syria katika Vita ya wenyewe kwa wenyewe, Hongera Urusi na Iran kwa ushauri mzuri


Kwani mngesemaje mashabiki wa Urusi na vita?
 
We jamaa bhana.....

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vipo Syria toka mwaka 2011,
 
We jamaa bhana.....

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vipo Syria toka mwaka 2011,
Vilikuwepo lakini havikufanikiwa kumtoa madarakani ila safari hii ilikua lazima Aidha akubali kumwaga damu au apishe kwa amani. Amechagua amani wenye Hila na fitina wameshindwa
 
Mkuu mtu mdini siyo mpaka aseme yeye ni mvaa kobazi au Mkristu/Mkristo, angalia hata mada zako nyingi unazoleta humu lazima mtu atajua tu kuwa wew ni mvaa kobazi. Anyway kama ulivyosema tuishie hapa nisiharibu uzi wako au kukukwaza
Kwasababu naipinga Israeli au napingana na marekani unaweza kuniitia hivyo na kwasababu nawaunga mkono wapalestina una Haki ya kuniona ni mdini ila ni mtazamo wako tu .Mimi ni shabiki mkubwa wa nchi zinazopingana na marekani na washirika wao. Mimi nawasapoti Korea kaskazini, urusi , china na wengine wanaofanana na hao. Ila siwezi kukuona wewe ni mkristo kwa kuwa upo upande wa Israel au Marekani hilo ulijue.
 
Ngoma ngumu alishazidiwa. Kama angetaka kuachia madaraka angeachia siku ya kwanza kwa hiari si kwa kufurushwa ikulu na kukimbia pasipojulikana....
Ngoma haijawa ngumu kwasababu Assad hakuamua kupigana maeneo yote waasi walipofika aliamuru Majeshi yake yaondoke yasipigane kwahiyo hakuna vita iliyopiganwa kumuondoa ikulu .
 
Ameen Sheitwyan..
 
Hajaleta upinzani wowote kwa waasi na jeshi alikua nalo kwahiyo namsifia kwa kuchukua uamuzi wa busara kuepusha mapigano na kuwaachia nchi Yao salama . Unaonaje kama angechukua uamuzi wa kupigana ?
 
Kushindwa au kushinda ni matokeo ya vita lakini mbaya zaidi ilikua anatakiwa kupigana na wananchi wake hujauona mtego huo? Ingekua wanaopigana nae wametoka nje ya Syria sidhani kama angeruhusu jeshi lake lisijibu mashambulizi. Ameepusha nchi yake na vita ya wenyewe kwa wenyewe inayochochewa na wenye Hila na fitina waliopo nje ya nchi yake.
 
Mtu aliyeshindwa ni mtu aliyepigana. Lakini Assad hakupigana Kila mji walioingia waasi aliamuru Majeshi yake yaondoke huo siyo uwoga ni Hekima .
 
Bro syria haitakuwa kama Libya trust me. Pale hesabu zote zishapigwa ni shia na Iran tu zile ushawishi wake hawautaki. Lakini hakuna kinachokwenda kuharibika. Pale Uturuki yupo asilimia 100 ndio injinia na hatakubali tena migrants.
Tuwaombee amani maana kwa sasa makundi ya waasi yapo zaidi ya 6 na Kila Moja Lina malengo yake.kumbuka hawa walioingia Damascus wanaungwa mkono na uturuki ambaye anawapinga wakurdi ambao nao wamo humo humo Syria.
 
Kama ni suala la busara na kuiepusha Syria na madhara makubwa, kwa nini Assad hakutumia busara hiyo mwaka 2011 na kuiepusha Syria na vita ya miaka 13?

Hujajibu swali hili.
Wakati ulikua Bado.hivi sasa ameona wakati umefika. Nadhani Busara Haina muda maalumu wa kutumika
 
Yani mtu kashindwa kusoma alama za nyakati tangu 2011 halafu umsifie kwa kusoma alama za nyakati mwaka 2024 wakati nchi ishachakazwa na watu wasiohesabika washakufa na kuumizwa?
Kwani Kuna sheria ya kusoma alama za nyakati? Kwamba usiposoma hizo alama mwaka Fulani ukija kuzisoma mwaka unaofuatia utakua umekosea.?
 
Asante kwa kuchangia
 
Hajui chochote huyu. Hajui hata kuna wakati kama sikosei Assad alitumia mabomu ya sumu kuua watu wake. Huenda ameanza kufuatilia vita hivi siku za karibuni.
Suala la kiongozi kuuwa Wananchi wake Aidha kisiasa au kwa namna yeyote ile haikubaliki na hii siyo kwa Syria tu nchi zote serikali zinauwa watu wake. Assad kuangushiwa zigo la lawama na kutafutiwa sababu za kuachia ikulu zipo wazi marekani lengo lake ni kuweka utawala anaoutaka yeye kama alivyofanya kwa sadam Hussein kule Iraq. na hata hivyo marekani ameingia kibabe Syria mpaka sasa Kwa hiyo Assad kwa kulitambua hilo alikua anajua anapambana na nani. Kama ulikua hujui basi ndio ufahamu hivyo. Watu siyo wajinga
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Punguza hasira mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…