KADA wa CCM Hussein Bashe anatajwa kuwa ndiye chanzo cha kuvuruga Kikao cha Kamati Kuu kilichopangwa kufanyika leo cha kupitisha majina ya wagombea ubunge wa majimbo na viti maalum baada ya kubainika kuwa sehemu kubwa ya wagombea waliopitishwa na Kamati za Siasa za Wilaya na Mikoa ni Maelekezo ya Bashe na sio mahitaji ya wananchi wa majimbo husika.
Bashe anatajwa kuingilia mchakato wa uchujaji majina ngazi ya Wilaya na mikoa kuendesha kampeni kubwa ya kukata wagombea na kupanga safu ya majina ya wagombea anaowataka yeye kwa kila jimbo ili kutengeneza Bunge litakalokuwa upande wake hasa katika kuelekea mbio zake za kusaka urais mwaka 2030.
Hatua hiyo imewastua viongozi Kamati Kuu na kutaka kupata muda wa kufuatilia michakato ngazi zote za Wilaya na Mikoa na kupitia malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa na wanachama ili kubaini ukweli wa taarifa hizo.
Hadi sasa Mikoa ambayo inasemekana tayari Bashe amefanikiwa kuweka wagombea wake ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro, Mkoa wa Shinyanga, Mkoa wa Mtwara, Mkoa wa Arusha, Mkoa wa Simiyu, Mkoa wa Mwanza, Mkoa wa Kagera, Mkoa wa Tabora, Mkoa wa Morogoro, Mkoa wa Njombe, Mkoa wa Katavi na Mkoa wa Pwani ambapo wagombea hao amewasaidia fedha nyingi za kuwawezesha kushinda.