Mkuu Usalama wa Taifa ni taasisi pana sana.Na unaweza usijue ni nani amehusika iwapo kazi imefanyika "kitaaluma" sawasawa.Maana haiwezekani jambo limetendeka la kuhatarisha au ku-defame hadhi ya nchi halafu mtu wa idara anayehusika eneo Hilo akae kimya tu.Atashughulika tu kwa vyovyote Maana Ndio kazi yake.Na wa kujua labda atakuwa ni immediate boss wake tu. Sasa hao wengine wanachezea hadi "sharubu" za nchi.Mintarafu Hilo la uhusiano mbaya wa JPM Na Kanisa Katoliki, maoni ya huyo Askofu yanabakia tu Ni maoni yake binafsi Na sio lazima uwe Ndio msimamo wa Kanisa.Msimamo wa Kanisa hutolewa Na Baraza la Maaskofu kupitia Idara husika .
QUOTE="lebara, post: 20594541, member: 155516"]Akiomba Mwongozo kwa Naibu Spika, Hussein Bashe amedai kuwa amefahamishwa na baadhi ya Mawaziri kuwa ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa kuna kikundi ambacho kinahusika na utekaji wa watu. Amedai kuwa kuna Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa na kuondolewa uhai. Mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie
Kwa hapa tulipofika, ni wazi kuwa JPM ajitafakari na baadhi ya watu wanaomzunguka.Kuna hali ya tahayari katika Taifa.
Jana nimeongea na Askofu mmoja wa Kikatoliki, nimeona dalili ya uhusiano wa JPM na Kanisa kudorora kwa namna anavyoendesha mambo ya Nchi.
Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana'
Wasalaam