Nimeshindwa kukaa kimya nimeamua na mimi kusema ya moyoni
ni kweli zama zinabadilika tulikuwa na mwl Nyerere tumepita kote huko kwa sasa tumeangukia hapa tulipo
kutokana na uzoefu wangu wa kuijua idara ya usalama ni idara imara sana katika taifa letu na hata watumishi wake walijengwa kwa misingi ya uzalendo na uadilifu..........enzi za mwl nyerere mpaka anaachia madaraka
akaja mzee mwinyi akasindikizwa na Mkapa pia idara ilisimama katika mizani ileya mwalimu Nyerere.
sio kwamba mambo yanayofanyika sasa yalikuwa hayafanyiki lakini yalikuwa yanafanyika kwa kiwango kikubwa cha uadilfu na usiri pamoja na umakini mkubwa sana na pia hapakuwa na matukio mengi kiasi hiko kama hivi sasa maana idara ilijikita zaidi katika maswala ya intel.
nashindwa kuelewa vijana wa kipindi hiki wamepatiwa mafunzo ya namna gani......??????? je ni kweli wameingia hukokwa mioyo yao yote.............???je ni kweli hawa wanalijenga Taifa au wanafata matwaka yao binafsi......??
swala hili limechangiwa sana na viongozi wa juu kuingiza watu katika idara na majeshi yetu watu wao wanaowajua wao kama ndugu, jamaa, na marafiki zao.
miaka ya 1995 mpaka 2001 afisa wa idara anastaafu hana hata gari au hana hata pikipiki lakini wanastaafu wakijua wamelitumikia taifa lao.....
leo unakuta watu wa idara wanauza intel nje ya systemili wapate hela au wanabadilishana intel na watu wasio wa system hii nikukosa weledi na uadilifu.
- embu angalia leo CIA haipo Democratic wala Republican na wanafanya kazi kama taaluma zingine kwa maslahi ya taifa lao. wanafanya uchunguzi na wanasemahata kama utamuuma trump wao hawajali hilo.
2.jeshi la polisi wajifunze kwa majeshi ya nje namna ya kufanya kazi kiweledi
OMBI KWA VIONGOZI WA IDARA HII KWA SASA IDARA IMEKUWA KAMA CHAMA CHA SIASA KWA KUWA KUNA MAKOSA MENGI YAMEFANYIKA AWALI
1. idara na vyombo vya usalama wamelala na wanawahusudu sana wanasiasa kuliko taifa lao
2. idara na vyombo vya dola wapitie katiba yetu upya na kwa umakini na pia wapitie viapo wanavyopewa wakati wa kuapishwa na hii itasaidia kwa watu kujitambua nini wafanye kwa maisha ya watoto wetu na vizazi vyao.
3. leo hii ccm wakifanya mkutano au vikao kuna wanausalama zaidi ya 2000 pale lakini haki hii inapaswa wapatiwe na vyama vingine kwa ajili ya kulinda maisha ya wananchi lakini ndio kwanza leo wanaenda kuvuruga na kupiga watu bado tunakazi kubwa ya kuwakumbusha WHO YOU ARE....???
kwa mfano kuna watu nimefanya nao kazi MWANZA, nikaja kuwakuta MORO mpaka wanakuja kuhamia DAR kuja kustaafu ndio najua kuwa ni usalama na hapo nimefanya nao kazi katika makampuni binafsi kwa muda wa miaka 25
hawa ndio walikuwa wanausalama japokuwa 2 kati yao wameshafariki ila kila wakati huwa sichoki kuwakumbuka.
NAJUA WAPO VIONGOZI WANAOFATILIA MIJADALA HUMU TAFADHALI MWANGALIENI YULE MKUU WA MAJESHI WA GAMBIA ALIMWAMBIA RAISI JAMMEH KUWA HATUINGIZA VIJANA WAKE VITANI KWA KUWA ANAWAPENDA SANA
IGENI HUU MFANO KUWENI WA KWANZA KUKOSOA VITENDO AMBAVYO VINAWADHALILISHA KUFIKIA MPAKA KUJADILIWA BUNGENI KWA IDARA YENU KWA MARA YA KWANZA MKIWA MNASEMWA KWA SKENDO ZA KIJINAI.
BADILIKENI FANYENI SCOUTING KAMA ZAMANI VERY DEEP KABLA YA KUAJIRI WATU WENU MSIINGIZE MAMLUKI WANAOTEKA WATU NA KUUA KWA KUPEWA FEDHA ZA SUPU YA PWEZA.
NAJUA MPO WAHUSIKA NA NAJUA KWA WAKONGWE MMENIELEWA IPO SIKU MTAFIKA PALE WATANZANIA WANAPOTAKA MFIKE.