Bashe: Kuna kikundi ndani ya Idara ya Usalama (TISS) kinahusika na utekaji. Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa

Bashe: Kuna kikundi ndani ya Idara ya Usalama (TISS) kinahusika na utekaji. Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa

Kwanini watu wasiamini kuwa Bashe ni mmoja wa watu wanaocheza hii Kombolela ya kuteka watu? Na kama hana hatia awataje hao mawaziri.
Huna hekima yoyote unadhalilisha hekima yenyewe. Mtu katoa taarifa kuwa kapewa taarifa na waziri, wewe kwa upeo mdogo unataka WAZIRI atajwe ili auawe yeye? Ni wajibu wa aliyeambiwa (spika) kuchukua hatua kwa kuishauri serikali nini cha kufanya au kuunda tume ya kibunge kuchunguza tuhuma na kuleta majibu. Wanaotekwa ni wananchi na wabunge ni wawakilishi wa wananchi walioiweka serikali madarakani. Akili nyingine zinatosha kufunga maandazi tu!
 
Ni ujinga na upumbavu kudai kajawa na hofu wakati mifano halisi inaonekana dhahiri. mpaka atekwe ndugu yako ndo ushituke na kupaza sauti ya kupinga?
 
Muweke wazi waziri huyo vinginevyo utakuwa unafiki huo Bashe!
 
Hii habari mbona sio kamili? Naibu Spika alijibu vipi huo mwongozo wa Bashe?

Vv
 
Mimi naona kila mtanzania akae makini na asilale bila sime au mkuki

Kama mtu hana hati ya kukukamata usikubali kuondoka nyumbani au ulipo,fanya fujo watu wajae mpaka kieleweke

Kuna mtu jana alishauri hao jamaa wakija ni kupiga kelele za mwizi tu,watu wajae
Ndugu yangu sime na bastola wapi na wapi. Weka sime watu wanaweka bunduki. Dawa kukaa na mabomu yenye expiry date ya mwaka 2099. Siku ilipogunduliwa ile kitu nyeusi ndipo mstari wa heshima ulipochorwa rasmi.
 
Huwezi kumkamata yeyote ndani ya Bashite Forces chini ya himaya ya dikteta uchwara. Invisible kikosi kwa jina lao maarufu.

Clouds media ilivamiwa na askari wenye silaha za moto, wakiambatana na gavana wa Dar.....

Aliyeunda Tume kuchunguza tukio hilo kafukuzwa kazi.......

Nape alitishiwa na bastola akizuiwa asiongee na waandishi wa habari pale Protea Hotel........

Msanii Roma na wenzake watatu wametekwa nyara siku chache zilizopita na baadaye tukamsikia Mkuu wa mkoa wa Dar akituhakikishia kuwa Roma na wenzake watapatikana kabla ya Jumapili na kwa hakika Roma akapatikana Jumamosi, one day before ya deadline akapatikana......


Kamanda Sirro anasema anaendelea na uchungizi wa matukio hayo.........

Waziri Mwigulu Nchemba tulimsikia akimuagiza IGP ahakikishe yule aliyemtolea bastola Nape asakwe na akamatwe na afikishwe kwenye vyombo vya sheria, lakini hadi leo yule jamaa hakamatiki.........

Huo ni uthibitisho tosha kuwa kumbe 'Bashite Forces' iko juu ya vyombo vyote vya dola hapa nchini!

Sasa tujiulize ni kwa nini hao 'Bashite Forces' wawe UNTOUCHABLES!?????
 
Huyu Bashe anajistukia tu, kwanini asijilipue kabsa kwa kutaja wahusika maana anajijua kabsa hayupo CCM tokea kipindi kile lowassa amekatwa hivyo nafsi yake haina amani kabsa kuendelea kuwepo CCM ila tu anajilazimisha, kujilazimisha huko kuna mkuta anazungumza mambo ya ajabu kabsa ya kumchafua Rais. Chunguzeni kwanini wale team Lowassa wote kama bashe,msukuma,malima ndio wapiga kelele kila siku? Kwanini Wao tu?

Hivi usalama gani wa taifa ukawa na kikundi cha utekaji na tena utekaji wa kipuuzi kabsa kama tunaouona sasa? System ikitaka kukuua inakuondoa tu haisubiri kukuteka.

Hizi ni chuki tu za baadhi wa wabaya wa Magufuli maana kama kuyabana majizi ni kweli kayabana kwa hiyo tusitegemee mteremko kwa Magufuli hata siku moja.Watu wenye pesa chafu watahonga sana hawa whistleblower kumchafua Magufuli.

Watamsingizia mengi mno huyu mzee na ndio kwanza picha inaanza.
kuna MAJITU MENGINE HUMU wao chuki zao ni mbele tu HATA KWENYE UWONGO YANAKUBALI TU.....utasikia mtu anasema ETI MAGUFULI nchi imemshinda....SASA hao ambao nchi haikuwashinda walitufikisha wapi???mbna still mlikuwa mna piga kelele???
Afadhali ya huyu amabaye mnasema nchi imemshinda lakini pesa za walipa kodi zipo salama si kwenye mikono ya wachache.......
ACHA TU atunyooshe HII MIAKA 10 AKILI ZIKAE vizuri kichwani......THEN 2025 tutaamua je tunataka RAIS aina ya KIKWETE au MAGUFULI.....tutajaji hili kupitia MAHALI alipotufikisha JPM na mahali alipotuacha JK......

Hela zipi za walipakodi ziko salama,pesa ambazo anajipangia yeye na binamu yake doto matumizi ndo ziko salama?hakuna kipindi hela zetu zimkuwa hatarini kama sasa maana ukoo mmoja ndo una maamuzi nazo,Leo tujenge airport chato na TENDA apewe mtoto wa kaka,haya kesho tujenge TRA chato na TENDA apewe mke hasara,ndo system mpya ya uongozi wa kifalme
 
Huyu Bashe anajistukia tu, kwanini asijilipue kabsa kwa kutaja wahusika maana anajijua kabsa hayupo CCM tokea kipindi kile lowassa amekatwa hivyo nafsi yake haina amani kabsa kuendelea kuwepo CCM ila tu anajilazimisha, kujilazimisha huko kuna mkuta anazungumza mambo ya ajabu kabsa ya kumchafua Rais. Chunguzeni kwanini wale team Lowassa wote kama bashe,msukuma,malima ndio wapiga kelele kila siku? Kwanini Wao tu?

Hivi usalama gani wa taifa ukawa na kikundi cha utekaji na tena utekaji wa kipuuzi kabsa kama tunaouona sasa? System ikitaka kukuua inakuondoa tu haisubiri kukuteka.

Hizi ni chuki tu za baadhi wa wabaya wa Magufuli maana kama kuyabana majizi ni kweli kayabana kwa hiyo tusitegemee mteremko kwa Magufuli hata siku moja.Watu wenye pesa chafu watahonga sana hawa whistleblower kumchafua Magufuli.

Watamsingizia mengi mno huyu mzee na ndio kwanza picha inaanza.
kuna MAJITU MENGINE HUMU wao chuki zao ni mbele tu HATA KWENYE UWONGO YANAKUBALI TU.....utasikia mtu anasema ETI MAGUFULI nchi imemshinda....SASA hao ambao nchi haikuwashinda walitufikisha wapi???mbna still mlikuwa mna piga kelele???
Afadhali ya huyu amabaye mnasema nchi imemshinda lakini pesa za walipa kodi zipo salama si kwenye mikono ya wachache.......
ACHA TU atunyooshe HII MIAKA 10 AKILI ZIKAE vizuri kichwani......THEN 2025 tutaamua je tunataka RAIS aina ya KIKWETE au MAGUFULI.....tutajaji hili kupitia MAHALI alipotufikisha JPM na mahali alipotuacha JK......
Huyu Bashe si aende tu huko CDM bosi wake ameshatangulia
 
Mi ni muumini mzuri tu wa CCM ila nilianza kuingiwa na ukakasi toka Bashite alipoanza kuwa na nguvu ndani ya taifa zaidibya hata VP tena mbaya zaidi kuwa juu zaidi ya PM Mh Majaliwa....
 
This issue is too sensitive, should not be ignored. Halafu tuepuke kuijadili kisiasa
 
This issue is too sensitive, should not be ignored. Halafu tuepuke kuijadili kisiasa
 
Naona tumeingia kwenye utawala kama wa Moi miaka ile ya 90's
 
Sasa umemwelewa Mkuu. Huyu ni mtu hatari sana kwenye Taifa letu huyu.

Mkubwa mmoja aliwahi kusema hivi hadharani "...Ningewapoteza wale wanaCCM waliokuwa wanaimba kuwa na imani na Lowassa "

Sikuweza kumwelewa alikuwa ana maanisha nini.
 
Hiki kikundi chenye aka ya 'Bashite Force' namna kinavyoteka watu wasio na hatia, hakina tofauti sana na kikundi kimoja kilichowahi kutoka kule Uganda miaka ile ya 70, kilichokuwa kinaongozwa na mtu mmoja ambaye alikuwa 'mshirika' mkubwa wa dictator Idi Amin, ambaye alikuwa anaitwa Malyamungu, ambacho kazi yake kubwa ilikuwa kuteka, kutesa na ikibidi kuwaua hao mateka wao.......

Kama tutaendelea kufumbia macho vitendo vya kikundi hiki cha 'Bashite Force' hatimaye kilio ndicho kitakachotuumbua........
 
Saivi ukitishiwa mapemaa posti mitandaoni kabisaa...
 
Back
Top Bottom