Tetty
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 26,355
- 21,422
Nipo hapa Dodoma. Nitakuwa hapa kwa majuma kadhaa. Nashuhudia Wabunge wanavyoacha kujiandaa kujadili Bajeti ya Serikali na kuanza kujadiliana na kuishi kwa 'machale'. Wabunge wanabaki na vitabu vyao; wanaogopeshwa na tabu zao. Tabu za adhabu. Adhabu kutoka wanakokuhisi.
Wabunge wanaacha kujiandaa na Bajeti, wanapenyezeana 'nyeti'. Nyeti za kuangusha miti na kuleta mtiti. Wabunge wanajazwa na kujazana hofu. Hofu isiyotamani hata minofu. Hata sehemu za waziwazi sasa kukaa ni kazi. Wabunge wetu wanasema kwa kuhema; wanahofu hadi vilivyo chini ya sakafu.
Nani anawatisha Wabunge wetu? Kwanini?
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Naona mmeamua kutumaliza ili mlete warundi/wanyarwanda??