Bashe: Kuna kikundi ndani ya Idara ya Usalama (TISS) kinahusika na utekaji. Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa

Bashe: Kuna kikundi ndani ya Idara ya Usalama (TISS) kinahusika na utekaji. Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa

Acha kutisha watu mkuu
Hali inayoendelea inampoteza magufuli ktk siasa.
Angalia zile sifa magu alizokuwa anazopewa kimataifa sasa hivi zipo wapi?
Acheni kushauri ujinga, sie tunayempenda lazima tumwambie aangalie ni wapi alipokosea ili heshima yake irudi kama mwamnzo
Utapotea Wewe Kwanza Kabla ya Mkuu wa Nchi Kupotea Katika Siasa Kama Unavyosema. Wewe Jitwishe Tu Ujasiri wa Kipumbavu. Ukiingiza Mikono Kwenye Mashine ni Lazima UTASAGIKA TU
 
Sana atuambie waziri gani kamwambia na hapo ndo tunapoanzia na uchunguzi kujua hawa niwakina nani na inakuwaje waziri kaijua hii je kaijuaje... Je waziri list kaitoa wapi that's easy Bashe mtaje huyo waziri watu waanze na uchunguzi
Na hawa mawaziri duuh nawaonea huruma???

Wewe ndiye wa ajabu kabisa

Sasa unataka atuambie humu JF ili iweje ? Unamtakia mema kweli huyo waziri ??

Ndiyo maana Katoa ushauri wa kuundwa kwa kamati teule ya bunge ili hayo ayasemee huko chini ya kiapo pamoja na kumlinda huyo waziri aliyempa taarifa hizo nyeti !!

Kwa ushauri wako huu, haukubaliki kwani ktk tuhuma kama hizi hatuendagi hivi !!
 
Serikali inahusika hili halikwepeki!

Ivi kwa akili za kawaida jamani kwa upande wa Roma ni raia gani ana miliki pingu? Siraha za moto (smg)? Na waliovamia kituo cha clauds si walionekana na siraha kama zile za Roma?

Na Bashe na wabunge hao 11 bila shaka Lissu hapo hakosekani na Lema kama sio TISS toka muhimili ule ni nani muhusika?

Bashe kakumbushia kwenye kikao cha chama kuwa ilisemwa kauli kuwa kuna bwana yule alisema wale walioimba wanaimani na mzee yule alitamani awapoteze sasa atawapotezaje?

Hivi vichwa vya watanzania tunafugia nywele tu au tumeamua kunyamaza?

Kama waziri anadai hakusikia gavana wa Dar akisema Roma atapatikana Kabla ya Jumapili na akapatikana Jumamos hana taarifa kweli inaingia akilini? Akapewa ushahidi na akajitoa ufahamu ndo tutamwani kwa hili?

Kama la Nape lilikuwa mchana je la Roma la usiku je?
 
Hayo ni mambo ambayo kisheria angelikwenda moja kwa moja police afungue kesi Ile sheria ifanye kazi Mara moja kwani haina maana kulihadithia bunge wakati tayari keshapata ushahidi wa kuambiwa sasa anataka atumiwe na barua ndio aende kushtaki polisi?
Hebu ngoja nikuulize swali dogo tu.

Nape aliunda Tume ya kuchunguza tukio la kuvamiwa kwa Clouds Media na matokeo ya Tume hiyo akaahidi kuwa ataikabidhi kwa Rais.

Unajua nini kilimtokea Nape?

Alifukuzwa kazi kabla hata hiyo ripoti haijafika mezani kwa Rais!

Mbunge Nape alitishiwa kwa bastola pale Protea Hotel ili asiongee na waandishi wa habari, tunakumbuka jinsi Waziri wa mambo ya ndani alivyomuagiza IGP Mangu kuwa mtu yule aliyemtishia kwa bastola Nape akamatwe na afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Wote tunajua kuwa hadi leo huyo IGP wetu hajathubitu kumtia mbaroni yule jamaa aliyemtolea bastola Nape!

Sasa wewe unapomshauri Bashe aripoti tukio la kutishiwa kwake Polisi ni kuwa hujajua kuwa 'Bashite Forces' ni UNTOUCHBLES na haliguswi na chombo chochote cha dola hapa nchini!
 
Kuna mambo yanaendelea nyuma ya pazia, kwanza ijulikane ni nani yuko nyuma ya haya yote.
 
Tuishie tu kumwomba mungu maana maisha ya sasa hakuna anaejua kila kitu sasa ni ubstili mtupu hapana pakukimbilia kwan Mara matumain Mara hofu du, binafsi sijui jaman
 
Usalama ndy boss hawa wengine kama wapambe tu si lolote si chochote. Kwa matukio haya yanayaendelea nchini hakuna qa kuyazuia maana hao wanaosemekana wanahusika hakuna mwenye uwezo wa kuhoji juu yao.
 
Kinachotakiwa Bashe athibitishe maelezo yake pasi na Shaka.

Hakuna haja ya kuonea huruma mawaziri kama walichomwambia Bashe ni kweli.
Kama kuna watu nyuma ya Bashe wanainjinia mpango huu ili kuupaka matope utawala wa Magufuli, ajue imekula kwake.

Hili hatukubali lipite hivihivi kwa kuuingiza usalama wa taifa kwenye hii scandal ya utekaji na uuaji.
Ajipange kulithibitisha Hili tamko lake
 
Bashe hana kabisa akili hata ya kudanganya, hebu jiulize kweli TISS iteke watu 11??

Wabunge / Mawaziri uteke Kweli 11 hapo dunia itakuwa imeisha labda hao 11 wakawa wamekosea kuingia pepo!!

Na pia asituletee siasa , za kisomalia ambapo hadi wabunge kujitoa mhanga ni kawaida.

Ila nailaumu sana ccm kwa kumpitisha wakati wakijua kuwa uria wake tangia azaliwe ni wa kutatanisha hadi majina yake.

Uhamiaji wanafanya nini? Kumbe Hussein Bashe si Raia!
 
Can you please, with your shining form four certificate, address yourself specifically to the issues raised in the comment?
Ukiendelea kubishana na mm ntakutaja and I will desclose your identity, wewe nakujua form four ulipata zero na Leo unadegree yako ya education, huna tofauti na BASHITE.
 
Afadhali ya huyu amabaye mnasema nchi imemshinda lakini pesa za walipa kodi zipo salama si kwenye mikono ya wachache......
Afadhali fedha zilipokua kwa watu wachache tulikua tunaziona mtaani sasa hivi zinafungiwa hazina TUNAISOMA NAMBA
 
Wakuu bila shaka tunazishudia hoja mbalimbali zinazotolewa na mh bashe kuhusu vitu mbalimbali vinavyofanywa na serikali ya magu. Je mh bashe akipewa uwaziri sasa hiv ataendelea kuipinga serikali ya magu? Au atakuwa kama mwakiyembe aliyefunga mdomo wake ili kunganga njaa yake?
 
Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe, ameomba mwongozo kuahirishwa kwa Bunge ili kutoa nafasi ya Wabunge wote kujadili matukio ya utekaji watu yanayoendelea.
Akiomba Mwongozo kwa Naibu Spika, Hussein Bashe amedai kuwa amefahamishwa na baadhi ya Mawaziri kuwa ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa kuna kikundi ambacho kinahusika na utekaji wa watu. Amedai kuwa kuna Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa na kuondolewa uhai. Mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie

"Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie. Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana".

​


Kwa hapa tulipofika, ni wazi kuwa JPM ajitafakari na baadhi ya watu wanaomzunguka.Kuna hali ya tahayari katika Taifa.

Jana nimeongea na Askofu mmoja wa Kikatoliki, nimeona dalili ya uhusiano wa JPM na Kanisa kudorora kwa namna anavyoendesha mambo ya Nchi.

Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana'

Wasalaam

Huyu ana akili kweli ,bunge lijadili upuuzi wake eti kwa kuwa kaambiwa kuna kundi la watekaji TISS yeye ni kiongozi na anajua wapi kwa kupeleka hizo tuhuma za uzushi,halafu bado anaendelea na uongo wake eti kaongea na Askofu mmoja wa katoliki na kaona dalili za kudorora kwa uhusiano ,huu si upumbavu kwa mbunge anayejifanya msomi na muelewa kwa hiyo uhusiano wa wa JPM na kanisa ukidolola ndio nchi itakufa,na hajui kwamba nchi haina dini huu ni jinga na uchonganishi na ni kutaka kupata huruma ya kanisa,sijui ni kwa lengo lipi,wengine wana kwao sisi hatuna kwetu zaidi ya hapa Tanzania,Bashe aache kutumika kwa ajenda zake za kipuuzi pamoja na kundi lake,kutwa ni kulalama tu kwa mambo ya kipuuzi sijui huko ndio kuwaletea maendeleo wana Nzega.Kama watu wamekutumia ujumbe upeleke mahala panapo husika na si bunge liache kujadili mambo ya maana na lianze kujadili habari za kutunga,waoneeni huruma walipa kodi,hamukwenda bungeni kutengeneza majungu.Unatia aibu Bashe.
 
Huyu Bashe anajistukia tu, kwanini asijilipue kabsa kwa kutaja wahusika maana anajijua kabsa hayupo CCM tokea kipindi kile lowassa amekatwa hivyo nafsi yake haina amani kabsa kuendelea kuwepo CCM ila tu anajilazimisha, kujilazimisha huko kuna mkuta anazungumza mambo ya ajabu kabsa ya kumchafua Rais. Chunguzeni kwanini wale team Lowassa wote kama bashe,msukuma,malima ndio wapiga kelele kila siku? Kwanini Wao tu?

Hivi usalama gani wa taifa ukawa na kikundi cha utekaji na tena utekaji wa kipuuzi kabsa kama tunaouona sasa? System ikitaka kukuua inakuondoa tu haisubiri kukuteka.

Hizi ni chuki tu za baadhi wa wabaya wa Magufuli maana kama kuyabana majizi ni kweli kayabana kwa hiyo tusitegemee mteremko kwa Magufuli hata siku moja.Watu wenye pesa chafu watahonga sana hawa whistleblower kumchafua Magufuli.

Watamsingizia mengi mno huyu mzee na ndio kwanza picha inaanza.
kuna MAJITU MENGINE HUMU wao chuki zao ni mbele tu HATA KWENYE UWONGO YANAKUBALI TU.....utasikia mtu anasema ETI MAGUFULI nchi imemshinda....SASA hao ambao nchi haikuwashinda walitufikisha wapi???mbna still mlikuwa mna piga kelele???
Afadhali ya huyu amabaye mnasema nchi imemshinda lakini pesa za walipa kodi zipo salama si kwenye mikono ya wachache.......
ACHA TU atunyooshe HII MIAKA 10 AKILI ZIKAE vizuri kichwani......THEN 2025 tutaamua je tunataka RAIS aina ya KIKWETE au MAGUFULI.....tutajaji hili kupitia MAHALI alipotufikisha JPM na mahali alipotuacha JK......
Kama uvccm wanasajiliwa Tic unategemea nini hapo ktk kukipigania chama kisianguke na serikali?
 
Back
Top Bottom