Bashe: Kuna kikundi ndani ya Idara ya Usalama (TISS) kinahusika na utekaji. Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa

Bashe: Kuna kikundi ndani ya Idara ya Usalama (TISS) kinahusika na utekaji. Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa

Haina tatizo, atamfuata babake rostam aka lowassa chadema!
Unapo kuwa unajiita wewe msema kweli pia kubali pia kuambiwa ukweli Kama wewe ulivyosema ukweli nyie CCM mtu akisimamia ikweli mnamwita msaliti.
Dhambi hii IPO siku itawatafuna na kuwamaliza
 
Wewe ni kiona mbali aisee! Bashe, Napegwa yatawakuta yaliyomkuta Shy-rose Banji EALA!
 
Haina tatizo, atamfuata babake rostam aka lowassa chadema!
Vitu vingine muwe mnakaa kimya kwani nayo ni busara sio kila kitu lazima uchangie wewe. Zungumza hoja za msingi kwani Lowasa na Rostam ni baba zake Bashe? Wewe lete hoja zenye mashiko kumpinga Bashe sio kuzungumza vitu visivyo na msingi.
 
Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe, ameomba mwongozo kuahirishwa kwa Bunge ili kutoa nafasi ya Wabunge wote kujadili matukio ya utekaji watu yanayoendelea.
Akiomba Mwongozo kwa Naibu Spika, Hussein Bashe amedai kuwa amefahamishwa na baadhi ya Mawaziri kuwa ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa kuna kikundi ambacho kinahusika na utekaji wa watu. Amedai kuwa kuna Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa na kuondolewa uhai. Mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie

"Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie. Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana".

​


Kwa hapa tulipofika, ni wazi kuwa JPM ajitafakari na baadhi ya watu wanaomzunguka.Kuna hali ya tahayari katika Taifa.

Jana nimeongea na Askofu mmoja wa Kikatoliki, nimeona dalili ya uhusiano wa JPM na Kanisa kudorora kwa namna anavyoendesha mambo ya Nchi.

Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana'

Wasalaam

Ukweli lazima usemwe
 
Eagle wing chini ya Bashite..badala ya kumpa nguvu Rais ndio inamuweka mbali na raia
 
ndugu mwenyekiti wa ccm usipo jenga ufa utajenga ukuta inaonekana huyu kijana anakupanda kichwani

Bwana huyu alianza matatizo yake tu pale vodacom walipoambiwa wajisajili kwenye soko la hisa alibishana na serkali mpaka basi bungeni

Na bwana huyu kidogo historia ni mmoja wa wale watu waliokuwa ubavuni mwa mafisadi sasa huyu yupo maalumu kukukwamisha na kutoa siri za chama

Ndugu mwenyekiti anza kumdhibiti mapema ikiwezekana aanze kufuatiliwa mali zake ni halali na amezipataje

Yeye ni nani mpaka aseme kwa wazee wa kitengo kuna kikosi cha kutesa watu,anataka kutuvunja imani ikiwezekana mfukuze aende kule anakotaka anayo magwanda ndani huyo
Asiharibu chama

msema kweli daima!
 
jamani haya mambo ya utekaji tusijapuuze wala kuyachukulia kiutani ni very serious hali si shwari hata kidogo. mbona kipindi cha Kikwete mambo haya hayakuwepo kwanini sasa? nimeshangazwa sana wiki iliyopita wakati Lema akichangia na kuhoji suala la kupotea kwa Ben Saanane kuna baadhi ya wabunge walikuwa wakicheka kwa kebehi utadhani huyo aliyepotea ni mbuzi au mende. Mungu awalaani wote mnaokebehi mambo haya hasa baadhi ya wabunge waliokuwa wakicheka. Bunge unganeni tupate solution ya suala la utekaji lililoibuka nchini. Yuko wapi BEN SAANANE? Mtanzania mwenyenzetu, ni binaadamu kama walivyo wengine ana haki ya kuishi!

Kwa swala la Ben 8 oclock jaribuni kuulizia waliokuwa msumbiji isije kuwa alibaki huko.
 
Hata hivo Rais Jpm ni mvumilivu, hivi kweli angekuwa dictator Bashe, nepi, wangethubutu kumuattack openly hivo?
 


Akiongea Bungeni leo mbunge wa Nzega alitaka shughuli za bunge ziahirishwe kwa ajili ya dharura ya kujadili watu kutekwa
Anadai yeye mwenyewe pamoja na wabunge akiwepo Msukuma, Malima, kwenye mkutano wa CCM
Pia amegusia Roma kutekwa na Ben Saanane na hawa ni watu wanaofahamika tu
Pia amepokea taarifa kutokakwa mawaziri wakimuonya kuwa akikaa vibaya barabarani anaweza kupoteza maisha
Anadai kikundi hicho kipo usalama wa taifa na kinaharibu sifa ya CCM pamoja na taifa, ameomba iundwe kamati na bunge kushughulikia tatizo hilo kwani limejadiliwa sana na hakuna statement serikalini
 
hii ni tuhuma nzito sana kwa idara muhimu ya usalama wa taifa letu. kama ni kweli idara hii iundwe upya. hili sio jambo dogo hata kidogo.
 
Sana atuambie waziri gani kamwambia na hapo ndo tunapoanzia na uchunguzi kujua hawa niwakina nani na inakuwaje waziri kaijua hii je kaijuaje... Je waziri list kaitoa wapi that's easy Bashe mtaje huyo waziri watu waanze na uchunguzi
Na hawa mawaziri duuh nawaonea huruma???
 
Back
Top Bottom