Bashe: Kuna kikundi ndani ya Idara ya Usalama (TISS) kinahusika na utekaji. Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa

Nadhani wiki ijayo atakaye tekwa ni Harmorapa, sababu hii ndio Kiki ya mwezi. Bashe na Nape kuweni makini sana, hao wanaowachekea na kuwapumbaza kuna siku watawaua kabisa ili kupata kiki kamili, kama waliweza kumuondoa Chacha Wangwe nyie ni mbwa tu kwao.
 
Huyu Bashe anajistukia tu, kwanini asijilipue kabsa kwa kutaja wahusika maana anajijua kabsa hayupo CCM tokea kipindi kile lowassa amekatwa hivyo nafsi yake haina amani kabsa kuendelea kuwepo CCM ila tu anajilazimisha, kujilazimisha huko kuna mkuta anazungumza mambo ya ajabu kabsa ya kumchafua Rais. Chunguzeni kwanini wale team Lowassa wote kama bashe,msukuma,malima ndio wapiga kelele kila siku? Kwanini Wao tu?

Hivi usalama gani wa taifa ukawa na kikundi cha utekaji na tena utekaji wa kipuuzi kabsa kama tunaouona sasa? System ikitaka kukuua inakuondoa tu haisubiri kukuteka.

Hizi ni chuki tu za baadhi wa wabaya wa Magufuli maana kama kuyabana majizi ni kweli kayabana kwa hiyo tusitegemee mteremko kwa Magufuli hata siku moja.Watu wenye pesa chafu watahonga sana hawa whistleblower kumchafua Magufuli.

Watamsingizia mengi mno huyu mzee na ndio kwanza picha inaanza.
hawa walikupa likes nao hamnazo, wazaramo wana msemo wao unaosema kusoma hujui basi hata picha huoni?
 
Bashe anajijua yuko mguu nje ccm ndo maana kila siku ni kumuandama Magufuli, swali la kitoto Mawaziri waliomwambia ndani ya TISS kuna kikundi kinateka watu kwanini walishindwa kumtajia hicho kikundi ili akitaje bungeni?
 
Tuache unafiki kiukweli mkuu nchi imemshinda
jamani haya mambo ya utekaji tusijapuuze wala kuyachukulia kiutani ni very serious hali si shwari hata kidogo. mbona kipindi cha Kikwete mambo haya hayakuwepo kwanini sasa? nimeshangazwa sana wiki iliyopita wakati Lema akichangia na kuhoji suala la kupotea kwa Ben Saanane kuna baadhi ya wabunge walikuwa wakicheka kwa kebehi utadhani huyo aliyepotea ni mbuzi au mende. Mungu awalaani wote mnaokebehi mambo haya hasa baadhi ya wabunge waliokuwa wakicheka. Bunge unganeni tupate solution ya suala la utekaji lililoibuka nchini. Yuko wapi BEN SAANANE? Mtanzania mwenyenzetu, ni binaadamu kama walivyo wengine ana haki ya kuishi!
 
Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe, ameomba mwongozo kuahirishwa kwa Bunge ili kutoa nafasi ya Wabunge wote kujadili matukio ya utekaji watu yanayoendelea.
Akiomba Mwongozo kwa Naibu Spika, Hussein Bashe amedai kuwa amefahamishwa na baadhi ya Mawaziri kuwa ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa kuna kikundi ambacho kinahusika na utekaji wa watu. Amedai kuwa kuna Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa na kuondolewa uhai. Mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie

"Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie. Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana".

Kwa hapa tulipofika, ni wazi kuwa JPM ajitafakari na baadhi ya watu wanaomzunguka.Kuna hali ya tahayari katika Taifa.

Jana nimeongea na Askofu mmoja wa Kikatoliki, nimeona dalili ya uhusiano wa JPM na Kanisa kudorora kwa namna anavyoendesha mambo ya Nchi.

Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana'

Wasalaam
WEWE NI MUONGO NA LENGO LENU NI KUIFANYA NCHI ISITAWALIKE KWA KUVIPAKA MATOPE VYOMBO VYA USALAMA - TUHUMA HIZO NI NZITO NA NI LAZIMA UZITHIBITISHE. TUHUMA HIZO ZINA KILA DALILI ZA UHAINI MAANA UNAMHUSISHA RAIS KATIKA JAMBO AMBALO HUNA USHAHIDI NALO NA LENGO LAKO NI KUMFANYA RAIS ACHUKIWE NA NCHI ISITAWALIKE - HUU NI UHAINI (TREASON - Kifungu cha 39 Penal Code) NA NI VYEMA KUJIANGALIA NA KUTAFAKARI KABLA YA KU POST MAMBO SENSITIVE KAMA HAYA: TUNAOMBA UTHIBITISHE PASIPO NA SHAKA KWAMBA TUHUMA HIZO.
 
Mbunge Hussein Bashe ameomba mwongozo kuahirishwa kwa Bunge ili kutoa nafasi ya Wabunge wote kujadili matukio ya utekaji watu yanayoendelea.
Akiomba Mwongozo kwa Naibu Spika, Hussein Bashe amedai kuwa amefahamishwa na baadhi ya Mawaziri kuwa ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa kuna kikundi ambacho kinahusika na utekaji wa watu. Amedai kuwa kuna Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa na kuondolewa uhai. Mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie

"Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie. Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana".

Kwa hapa tulipofika, ni wazi kuwa JPM ajitafakari na baadhi ya watu wanaomzunguka.Kuna hali ya tahayari katika Taifa.

Jana nimeongea na Askofu mmoja wa Kikatoliki, nimeona dalili ya uhusiano wa JPM na Kanisa kudorora kwa namna anavyoendesha mambo ya Nchi.

Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana'

Wasalaam
Idara ya usalama wa taifa kuteka ni moja ya majukumu yao, ila ni nani anaetekwa??? ni yule anaeonekana kuhatarisha usalama wa taifa. Sasa Bashe jipime kama unahatarisha usalama wa taifa unaeza ukawa miongoni. To me bashe bado hujafikia kiasi hicho cha wewe kutekwa, wewe ni wa kuvuliwa tu uanachama uka ungane na Lowassa wako. Usilete unazi wako.
 
Hiyo ni sayansi ya siasa !!

JPM, wabane washindwe kulala!

Si wanasema hamna hela za vikao sasa, bungeni wanafata nini na kuweka porojo kama hizi??
bungeni hawajatumwa na JPM, bungeni wametumwa na watu waliowapa kura na kuwaamini, hawakuteuliwa kama dada zako ambao hawajui shida za wananchi,
 
Bashe angetoa ushahidi wa hayo aliyoyasema tungemwelewa. Kusema tu haitoshi maana kwa sasa yanasemwa mengi. Na kama hana ushahidi anapaswa kuwa makini kutoa tuhuma za namna hiyo. Lakini pia, Bashe hayuko at ease kabisa, yaani hajaamini kama ameachwa wakati inajulikana kuwa alikuwa mshirika wa Lowassa
 
Idara ya usalama wa taifa kuteka ni moja ya majukumu yao, ila ni nani anaetekwa??? ni yule anaeonekana kuhatarisha usalama wa taifa. Sasa Bashe jipime kama unahatarisha usalama wa taifa unaeza ukawa miongoni. To me bashe bado hujafikia kiasi hicho cha wewe kutekwa, wewe ni wa kuvuliwa tu uanachama uka ungane na Lowassa wako. Usilete unazi wako.
daah hii nchi hii, inafikia kipindi mtu unaongea mpaka unakufuru, mtu anayetetea wanyonge mnamuona kama gaidi, lakini anayetukana, kudhihaki na kutesa wananchi mnamuona shujaa, daah, aisee
 
Bashe anajijua yuko mguu nje ccm ndo maana kila siku ni kumuandama Magufuli, swali la kitoto Mawaziri waliomwambia ndani ya TISS kuna kikundi kinateka watu kwanini walishindwa kumtajia hicho kikundi ili akitaje bungeni?
BASHE AKITAJE HICHO KIKUNDI NA ATHIBITISHE TUHUMA HIZO LA SIVYO KANUNI ZA BUNGE ZITAMMALIZA MAANA HAIPASWI KUTUMIA BUNGE KUTOA TUHUMA ZA UONGO DHIDI YA WATU AMBAO SIO WABUNGE - HII ITAMGARIMU
 
Huyu Bashe anajistukia tu, kwanini asijilipue kabsa kwa kutaja wahusika maana anajijua kabsa hayupo CCM tokea kipindi kile lowassa amekatwa hivyo nafsi yake haina amani kabsa kuendelea kuwepo CCM ila tu anajilazimisha, kujilazimisha huko kuna mkuta anazungumza mambo ya ajabu kabsa ya kumchafua Rais. Chunguzeni kwanini wale team Lowassa wote kama bashe,msukuma,malima ndio wapiga kelele kila siku? Kwanini Wao tu?

Hivi usalama gani wa taifa ukawa na kikundi cha utekaji na tena utekaji wa kipuuzi kabsa kama tunaouona sasa? System ikitaka kukuua inakuondoa tu haisubiri kukuteka.

Hizi ni chuki tu za baadhi wa wabaya wa Magufuli maana kama kuyabana majizi ni kweli kayabana kwa hiyo tusitegemee mteremko kwa Magufuli hata siku moja.Watu wenye pesa chafu watahonga sana hawa whistleblower kumchafua Magufuli.

Watamsingizia mengi mno huyu mzee na ndio kwanza picha inaanza.
Team Lowassa na Team Membe wanaturudisha nyuma sana. Magu akomae nao mpaka kieleweke.
 
Back
Top Bottom