Kweli kabisa vijana wanapigwa sana kwasababu ya uvivuBashe yuko sahihi 100%. Kina Mr Kuku wametajirika kiujanja ujanja
Leo waziri wa kilimo Hussein Bashe amezungumza na waandishi wa habari amewasihi vijana wanaofikilia kulima kilimo kwenye mitanzandao ya kijamii waache mara moja
"Tunatoa uelewa acheni kulima kwa Twitter na WhatsApp, hakuna mtu anayeweza kukuambia lete milioni 10 na baada ya mwezi utapata 15 niwaombeni kwenye kilimo hakuna njia ya mkato kama una hela yako nenda kanunue ardhi, ajiri kijana wa chuo kikuu, halafu zalisha,"
Lakini pia hata kama unawapa vijana wakusimamie mashamba yako usisahau kutembelea shambani kila wiki ili kupata matokeo mazuri ya kilimo
Watanzania huwa hawajifunzi kabisaVannila international
Baada ya Kupiga Ela za Watu iringa,
Takukuru awamu ya magu wakaanza kuwawinda, walipotea mafichoni mazima
Sahv naona wamerud upya kwa Kasi,
Tena anajitangaza upya Kwny tv na kutoa upya semina za kilimo Cha vanilla kilo milioni.
Na hapa najua,
Kuna maboya wengine watapigwa upya[emoji38]
Ndio maana amesema kama una pesa ajiri watu wakusaidie na sio kufanya kilimo cha mtandaoni Lakini pia Katika kuleta mageuzi kwenye kilimo, Serikali ya Rais Samia Suluhu imetenga ekari 160,000 kwa ajili ya mashamba ya vijana, huku wakitaraji kugawa kwa vijana 40,000."Kama una hela nunua ardhi ajiri kijana wa chuo kikuu halafu zalisha".
Kwa pembejeo zipi na ruzuku zisizoeleweka. Hata kilimo cha mdomo kama anachokitoa yeye sio kilimo.
HahahhaLete pesa nikulimie nawe uje uchukue mavuno tu. Ni salama na nafuu
Tafuta shamba la karibu, mafanikio kwenye kilimo yanawezekana sanaTuseme una shamba Morogoro na unaishi Dar, utaweza kutembelea hilo shamba kila wiki? Hizo gharama za usafiri si ndio itakuwa faida yenyewe? Kwa mazingira yetu ni ngumu sana kufanikiwa kupitia kilimo. Changamoto za kilimo ni nyingi kupita kiasi. Ni nadra kuanza kuona mafanikio ya kilimo chini ya miaka 5.
Hata waziri amesema leo ukianza kulima usitegemee kesho uanze kupata faida haya ni malengo ya muda mrefu japokuwa wenye mitaji mikubwa wanapata sana faida maana usimamizi unakuwa wa hali ya juuTuseme una shamba Morogoro na unaishi Dar, utaweza kutembelea hilo shamba kila wiki? Hizo gharama za usafiri si ndio itakuwa faida yenyewe? Kwa mazingira yetu ni ngumu sana kufanikiwa kupitia kilimo. Changamoto za kilimo ni nyingi kupita kiasi. Ni nadra kuanza kuona mafanikio ya kilimo chini ya miaka 5.
Tafuta shamba la karibu, mafanikio kwenye kilimo yanawezekana sana
Sogea mbele ya Pugu kule bado kuna mashamba, sio lazima acre 40, hata 3 inategemea unalima nini, mazao kama vitunguu acre 4 zinaweza kuzidi faida mahindi acre 40 ukilima kiutaalamUkiwa hapa Dar shamba la karibu utapata wapi boss?
Hata waziri amesema leo ukianza kulima usitegemee kesho uanze kupata faida haya ni malengo ya muda mrefu japokuwa wenye mitaji mikubwa wanapata sana faida maana usimamizi unakuwa wa hali ya juu
sogea mbele ya Pugu kule bado kuna mashamba, sio lazima acre 40, hata 3 inategemea unalima nini, mazao kama vitunguu acre 4 zinaweza kuzidi faida mahindi acre 40 ukilima kiutaalam
Nimehadithiwa tuuMkuu umewahi kulima kitunguu au umehadithiwa?
Ishia hapo hapo mkuu. Ninajua ninachoongea. Kama una mtaji wa kujifunza changamoto ndani ya miaka 5, basi ingia kwenye hicho kilimo. Kinyume na hapo ni bora uuze spea za pikipiki hapa mjini utanishukuru.Nimehadithiwa tuu