Bashe: Wananchi acheni kulima kwa Twitter na WhatsApp

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Leo waziri wa kilimo Hussein Bashe amezungumza na waandishi wa habari amewasihi vijana wanaofikilia kulima kilimo kwenye mitanzandao ya kijamii waache mara moja

"Tunatoa uelewa acheni kulima kwa Twitter na WhatsApp, hakuna mtu anayeweza kukuambia lete milioni 10 na baada ya mwezi utapata 15 niwaombeni kwenye kilimo hakuna njia ya mkato kama una hela yako nenda kanunue ardhi, ajiri kijana wa chuo kikuu, halafu zalisha,"

Lakini pia hata kama unawapa vijana wakusimamie mashamba yako usisahau kutembelea shambani kila wiki ili kupata matokeo mazuri ya kilimo
 
Lete pesa nikulimie nawe uje uchukue mavuno tu. Ni salama na nafuu
 
Vannila international
Baada ya Kupiga Ela za Watu iringa,
Takukuru awamu ya magu wakaanza kuwawinda, walipotea mafichoni mazima

Sahv naona wamerud upya kwa Kasi,
Tena anajitangaza upya Kwny tv na kutoa upya semina za kilimo Cha vanilla kilo milioni.

Na hapa najua,
Kuna maboya wengine watapigwa upya[emoji38]
 
Leo waziri wa kilimo Hussein Bashe amezungumza na waandishi wa habari amewasihi vijana wanaofikilia kulima kilimo kwenye mitanzandao ya kijamii waache mara moja

"Tunatoa uelewa acheni kulima kwa Twitter na WhatsApp, hakuna mtu anayeweza kukuambia lete milioni 10 na baada ya mwezi utapata 15 niwaombeni kwenye kilimo hakuna njia ya mkato kama una hela yako nenda kanunue ardhi, ajiri kijana wa chuo kikuu, halafu zalisha,"

Lakini pia hata kama unawapa vijana wakusimamie mashamba yako usisahau kutembelea shambani kila wiki ili kupata matokeo mazuri ya kilimo

Tuseme una shamba Morogoro na unaishi Dar, utaweza kutembelea hilo shamba kila wiki? Hizo gharama za usafiri si ndio itakuwa faida yenyewe? Kwa mazingira yetu ni ngumu sana kufanikiwa kupitia kilimo. Changamoto za kilimo ni nyingi kupita kiasi. Ni nadra kuanza kuona mafanikio ya kilimo chini ya miaka 5.
 
Vannila international
Baada ya Kupiga Ela za Watu iringa,
Takukuru awamu ya magu wakaanza kuwawinda, walipotea mafichoni mazima

Sahv naona wamerud upya kwa Kasi,
Tena anajitangaza upya Kwny tv na kutoa upya semina za kilimo Cha vanilla kilo milioni.

Na hapa najua,
Kuna maboya wengine watapigwa upya[emoji38]
Watanzania huwa hawajifunzi kabisa
 
"Kama una hela nunua ardhi ajiri kijana wa chuo kikuu halafu zalisha".
Kwa pembejeo zipi na ruzuku zisizoeleweka. Hata kilimo cha mdomo kama anachokitoa yeye sio kilimo.
Ndio maana amesema kama una pesa ajiri watu wakusaidie na sio kufanya kilimo cha mtandaoni Lakini pia Katika kuleta mageuzi kwenye kilimo, Serikali ya Rais Samia Suluhu imetenga ekari 160,000 kwa ajili ya mashamba ya vijana, huku wakitaraji kugawa kwa vijana 40,000.
 
Tuseme una shamba Morogoro na unaishi Dar, utaweza kutembelea hilo shamba kila wiki? Hizo gharama za usafiri si ndio itakuwa faida yenyewe? Kwa mazingira yetu ni ngumu sana kufanikiwa kupitia kilimo. Changamoto za kilimo ni nyingi kupita kiasi. Ni nadra kuanza kuona mafanikio ya kilimo chini ya miaka 5.
Tafuta shamba la karibu, mafanikio kwenye kilimo yanawezekana sana
 
Tuseme una shamba Morogoro na unaishi Dar, utaweza kutembelea hilo shamba kila wiki? Hizo gharama za usafiri si ndio itakuwa faida yenyewe? Kwa mazingira yetu ni ngumu sana kufanikiwa kupitia kilimo. Changamoto za kilimo ni nyingi kupita kiasi. Ni nadra kuanza kuona mafanikio ya kilimo chini ya miaka 5.
Hata waziri amesema leo ukianza kulima usitegemee kesho uanze kupata faida haya ni malengo ya muda mrefu japokuwa wenye mitaji mikubwa wanapata sana faida maana usimamizi unakuwa wa hali ya juu
 
Ukiwa hapa Dar shamba la karibu utapata wapi boss?
Sogea mbele ya Pugu kule bado kuna mashamba, sio lazima acre 40, hata 3 inategemea unalima nini, mazao kama vitunguu acre 4 zinaweza kuzidi faida mahindi acre 40 ukilima kiutaalam
 
Hata waziri amesema leo ukianza kulima usitegemee kesho uanze kupata faida haya ni malengo ya muda mrefu japokuwa wenye mitaji mikubwa wanapata sana faida maana usimamizi unakuwa wa hali ya juu

Mkuu wenye mitaji mikubwa pia wanabiashara nyingine, ndio backup ya hicho kilimo. Lakini kama unategemea kilimo pekee tegemea kuchanganyikiwa. Mkuu nimelima najua ninachoongea. Ni nadra sana kutoboa chini ya five years. Je ni wangapi wenye uvumilivu wa zaidi ya miaka mitano. Na hata kama una uvumilivu, baada ya hiyo miaka mitano utakuwa bado na mtaji?
 
sogea mbele ya Pugu kule bado kuna mashamba, sio lazima acre 40, hata 3 inategemea unalima nini, mazao kama vitunguu acre 4 zinaweza kuzidi faida mahindi acre 40 ukilima kiutaalam

Mkuu umewahi kulima kitunguu au umehadithiwa?
 
Back
Top Bottom