Bashiru Ally ameongoza mazishi ya watoto walioungua moto huko Kyerwa Kagera kama nani?

Bashiru Ally ameongoza mazishi ya watoto walioungua moto huko Kyerwa Kagera kama nani?

ITV imemuonyesha Katibu Mkuu wa CCM ndugu Bashiru Ally akitajwa kuwa mgeni rasmi kwenye mazishi ya watoto 10 waliozikwa leo huko Kagera, sina shida na mtu yoyote kuhudhuria mazishi yoyote popote lakini kumpa cheo cha kuongoza mazishi mtu asiye na cheo chochote kwenye Serikali yetu ni dharau kubwa sana kwa wananchi na marehemu wao.

Kuleta kampeni za kishamba kwenye misiba isiyo ya kisiasa haikubaliki na hali hii ikiachwa iko siku itakuja kuleta machafuko kwenye misiba na kuharibu shughuli za watu, fanyeni siasa zenu majukwaani.

Napinga CCM chama kilichokongoroka kujaribu kutumia majanga kujinadi, marehemu hao ambao walikuwa watoto hawakuwahi kuwa na kadi za CCM, za chipukizi wala za UVCCM, hii haikubaliki hata kidogo.
Bashiru ni mpumbavu. Hakuna lugha inayomfaa zaidi ya hii. He is a misguided missile. Hatari kwa ccm na taifa.
 
Back
Top Bottom