Bashiru Ally: Heshima ya nchi yetu imeshuka, tunadhalilika kwa njaa

Bashiru Ally: Heshima ya nchi yetu imeshuka, tunadhalilika kwa njaa

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
"Njaa inadhalilisha heshima na uhuru wa nchi, inatweza utu wa binadamu kwahiyo tatizo la mfumuko wa bei za vyakula ni tatizo ambalo tutake tusitake lazima tuongeze kiwango cha ubunifu kukabiliana nalo, hakuna ukomo wa ubunifu, wananchi wanakibiliana na tatizo hili.

"Nilikuwa nazungumza na wananchi mmoja amesema chakula cha asubuhi na mchana kinaunganishwa kwenye saa 5 na 6, mlo wa usiku unaunganishwa kati ya saa 11 na 12, hawasubiri kujadili mambo ya Ukraine na tabianchi, wameanza kuchukua hatua.
 
Mh....Watu mnapita na ku like post ila hamchangii?

Okay mi mchango wangu ni, vyakula kupanda bei ni kutokana na ukame wa mwaka jana.

Japo serikali ilihifadhi chakula kingi kwenye maghala hadi maximum yake ya tani laki 2 bado chakula hicho hakikutosha

Swala hili halina suluhu ya muda mfupi, suluhu ya uhakika ni kutengeneza mifumo ya kilimo cha umwagiliaji ambayo itachukua muda na gharama

Ama kama tuagize mahindi ya bei rahisi kutoka Brazil na Argentina? Tukifanya hivyo jua wakulima wetu mahindi yao hayatauzika
 
Huyu mtu ana asili na uzoefu katika masuala ya taaluma, lkn pia ni mtu aliyekopwa kwa ajili ya sababu za kiutendaji za kisiasa. "Analysis" yake inaaminika na pia yenye mantiki, kwa mazingira na muktadha wa kijamii na kiuchumi tunayoyapitia kama taifa.

Baniani mbaya, ila kiatu chake ni dawa. Huyu ni mtu mwenye uaminifu wa milengo ya siasa za kijamaa, ila ni mtu mwenye msimamo wa kile alichoaminishwa na kukiamini.
 
Mkitanguliza mbele masilahi mapana ya Raia, sidhan kama mnaweza kuitisha waandishi wa habari na vihoja uchwara kumjibu Bashiru.

Ni Kwamba Bashiru ni Kiongozi, Udaktari wake ni wa uhakika , Kichwa chake kakijaza mema, busara na Hekima kiasi kwamba anachowaza ni WANANCHI TU.

Maajabu Kuna Chawa ,shule ndogo, akili kiduchu wenye utupu kichwan, kwakua tu ni machawa , basi yanalazimika kusema neno ili Matumbo yao yashibe .

Changamoto yake ni moja tu, hivi sasa akubaliki na wahafidhina ndani ya chama, kosa lake linaoneka linatokana na zoezi alilolisimamia kwa uadilifu mkubwa wa kuhakiki mali za chama tawala. Ukweli wake umemponza, uongo na unafiki wake ungalimuokoa.
Hana alichopoteza. Subiri utajionea.
 
Kuna jambo sijawahi kulielewa nchi hii na hili limekuwa linatokea mara kwa mara. Kama tuko kwenye kipindi ambacho watu hawana pesa, bidhaa si zinatakiwa zipungue bei na si kuongezea? Watu wakiwa hawana pesa, inamaanisha wanunuzi wa bidhaa wanapungua, na hilo linafanya wauzaji kupunguza bei.

Nini huwa kinatokea kinafanya hii kanuni ya uchumi isiwe inafanya kazi?
 
Mkitanguliza mbele masilahi mapana ya Raia, sidhan kama mnaweza kuitisha waandishi wa habari na vihoja uchwara kumjibu Bashiru.

Ni Kwamba Bashiru ni Kiongozi, Udaktari wake ni wa uhakika , Kichwa chake kakijaza mema, busara na Hekima kiasi kwamba anachowaza ni WANANCHI TU.

Maajabu Kuna Chawa ,shule ndogo, akili kiduchu wenye utupu kichwan, kwakua tu ni machawa , basi yanalazimika kusema neno ili Matumbo yao yashibe .

Chawa hawa ni wa hovyo sana, walishindwa kumkemea mchovya asali mzee asiye na busara Makamba alivyokejeli vifo vya waliotangulia mbele za haki lakini kwa Bashiru wanakuja mbio mbio kila mmoja akijipendekeza kama amnamsemea mkuu sijui sielewi mkuu kama yeye anashindwa kujibu hoja za msingi akiwategemea chawa/kunguni wanyonya asali.
 
Huyu mtu ana asili na uzoefu katika masuala ya taaluma, lkn pia ni mtu aliyekopwa kwa ajili ya sababu za kiutendaji za kisiasa. "Analysis" yake inaaminika na pia yenye mantiki, kwa mazingira na muktadha wa kijamii na kiuchumi tunayoyapitia kama taifa.

Baniani mbaya, ila kiatu chake ni dawa. Huyu ni mtu mwenye uaminifu wa milengo ya siasa za kijamaa, ila ni mtu mwenye msimamo wa kile alichoaminishwa na kukiamini.
Tatizo lipo linaanzia hapo alipokopwa na mfumo na bahati mbaya mkasahau utendaji wake mkamuingiza kwenye kapu moja na wasiofaa.

Mfano CCM ilipaswa kumtunuku heshima kiutendaji kutokana na kufuatilia mali zote za chama zilizokuwa mikononi mwa watu na zilizotaifiashwa zifahamike, ila mwisho mkamuona ndiyo wale wale, tupa kule!.
 
Mkitanguliza mbele masilahi mapana ya Raia, sidhan kama mnaweza kuitisha waandishi wa habari na vihoja uchwara kumjibu Bashiru.

Ni Kwamba Bashiru ni Kiongozi, Udaktari wake ni wa uhakika , Kichwa chake kakijaza mema, busara na Hekima kiasi kwamba anachowaza ni WANANCHI TU.

Maajabu Kuna Chawa ,shule ndogo, akili kiduchu wenye utupu kichwan, kwakua tu ni machawa , basi yanalazimika kusema neno ili Matumbo yao yashibe .

Nasikia anajipanga ili 2025 agombee uraisi kupitia ACT wazalendo.
 
Back
Top Bottom